USHAURI: Rais Samia suluhisho pekee kwa Bandari Tanzania ni hili

USHAURI: Rais Samia suluhisho pekee kwa Bandari Tanzania ni hili

Amani iwe nanyi
Leo Rais wa JMT amemtumbua Mkurugenzi wa Bandari Ndug Erick Hamis.

Pamoja na kumtumbua Rais Samia amelalamika juu ya efficiency ya Mamlaka yetu ya Bandari na kusema kuwa Mamlaka hii ingekuwa inafanya kazi vizuri ingeweza kuchangia hata nusu ya mapato ya Bajeti yetu. Ni kweli kabisa naungana na Rais Samia kwenye hili!

Mfupa wa Bandari ni mfupa uliowashinda Marais karibu wote waliowai kutawala Tanzania! Hii imekuwa kawaida kila Rais mpya akiingia au Waziri Mkuu mpya akiteuliwa sehemu ya kwanzq kwenda kulalamika na kutumbua imekuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Kwa kumbukumbu zangu kuanzia kwa Mkapa, Kikwete, Magufuli hadi sasa Samia, Bandari hapajawai kupoa.

Hoja yangu kuu kwenye hili ni kwamba inawezekana sana bado hatujajua shida ni nini hasa pale Bandarini na kwa uelewa wangu mdogo napenda leo nimshauri Mhe Rais mambo ya kufanya na naamini kama nilivyoshauri kuhusu Ngorongoro na ikafanyika na sasa imefanikiwa basi nashauri juu ya hili la Bandari na naamini ikifanyika itafanikiwa

1. Lazima tukubali kuwa Bandari ya DSM haiwezi kuwa efficient kwa sababu imekuwa finyu kuhimili idadi ya mizigo, Meli na Magari kiushindani

2. Lazima tukubali kuwa Serikali haiwezi kuendesha bandari kwq ufanisi tunaoutaka katika dunia hii ya ushindani. Bandari kubwa zote duniani na zinazofanya vizuri kwenye soko la ushindani kuanzia Dubai, Hong Kong, Singapore, New York na nyinginezo, zinaendeshwa either kwa sehemu kubwa na private sector au kwa ubia baina ya Serikali na Private Sector

Hivyo ili kufanikiwa kupata ufanisi hapa Tanzania kwenye sekta ya Bandari , Lazima tutake tusitake, tufanye yafuatayo

a. Kwa haraka sana, Ijengwe Bandari ya Bagamoyo ambayo iwe na Gati zisizopungua 40. Bandari hii iendeshwe na Private sector with exception kwenye masuala ya Ulinzi, Usalama na Kodi

b. Sekta binafsi wapewe pia fursa ya kujenga Miundombinu ya Reli na barabara kuunganisha Bandari ya Bagamoyo na Jiji la Dar es Salaam ikiwemo reli ya kati SGR na TAZARA

c. Bandari za DSM, Tanga, Mwanza na Kigoma na Mtwara ziendeshwe kwa ubia na Private sector. Serikali isimamie masuala ya kodi , ulinzi na usalama tu!

d. Barabara ya Mandela Road( dsm) itanuliwe kuwekwa njia 8 kutokea Bandarini hadi Ubungo na utanuzi wa njia 6 uendelee kutoka Kimara hadi Ubungo. Hii ni ili kuleta ufanisi wa usafirishaji mizigo katika Jiji la Dsm. Ikiwezekana Private sector washirikishwe kwenye hili.

e. Kulikuwa na Mpango wa Kujenga Barabara ya Malori kutokea Bandarini hadi Chalinze. Mpango huu ufufuliwe na barabara hii ijengwe hata kwa kutumia Private sector! Fedha zitarudi haraka sana hata kwa toll tax!

Nchi kubwa duniani ziliona hili na wakaamua kufanya! Hata kwa Tanzania Serikali iking'ang'ania kuendesha bandari kila siku mtaishia kushikana uchawi na kutumbuana!

Ni suala la kuamua tu na wakati ni sasa
Inasemekana chama Cha kijani kinaweka makada wake huko bandarini kwa maslahi ya kichama wakitaka mpunga wanaupata kirahisi can
Hiki chama uwepo wake Ni hatari kwa maendeleo ya Tanzania.
 
Inawezekana! Singapore wanafanya kwa nini isiwezekane Tanzania?
... ndio maana nikasema kuna mahali tunakosea! Bila kurekebisha, kufikia level za Singapore ni ndoto za alinacha! Tutaendelea kuota ndoto za maendeleo miaka nenda miaka rudi.
 
Na suala la utitiri wa Clearing and forwarding agents uangaliziwe.
Siku hizi kumekuwa na utitiri wa Clearing and forwarding agency companies na zingine ni za mifukoni kabisa kwa sababu ya urahisi wa kuzìanzisha na huku kukiwa na uchache wa mizigo inayokuja na kupitishwa nchini matokeo yake ma agents wengi siku hizi ni kama vishoka tu,watu wanalizwa sana na hao hao ma agent ndio wamekuwa kama ndio wanasaidia kukwepa sana kodi wakishirikiana na watumishi wa mamlaka za ukusanyaji mapato(TRA)
Bandari haina ufanisi na hata mamlaka zingine kama TRA,TMDA,TBS,GCA wamekuwa na ufanisi mdogo sana.
Napendekeza hizi Clearing agents ziwe chache zenye sifa ya kimtaji na kiuweledi na hizo ndio zitoe ajira kwa agents wengi ufanisi utapatikana tu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
dawa yao hao wote ni management nzimq isimamiwe na strong private sector!

Muwekezaji makini akiwa anamanage bandari hawezi kuacha upuuzi kama huo kuendelea maana utaharibu biashara yake na reputation yake
 
Inasemekana chama Cha kijani kinaweka makada wake huko bandarini kwa maslahi ya kichama wakitaka mpunga wanaupata kirahisi can
Hiki chama uwepo wake Ni hatari kwa maendeleo ya Tanzania.
Tupe ushahidi kwenye hili
 
... ndio maana nikasema kuna mahali tunakosea! Bila kurekebisha, kufikia level za Singapore ni ndoto za alinacha! Tutaendelea kuota ndoto za maendeleo miaka nenda miaka rudi.
Tuanze kufanya hili sasa
 
... mnakumbuka stori za NetGroup Solutions? Mnakumbuka jinsi ilivyosifiwa? Kwamba siangalii rangi ya paka, muhimu akamate panya? Mnakumbuka jinsi ilivyoiacha taasisi ile mahututi hadi kesho? Private sector is one thing ila kuna tatizo la msingi zaidi! Bila kutatua kiini cha tatizo mtaleta kila aina ya private sector ila nchi itaendelea kubaki mahututi!
Chama Cha kijani kikiendelea kuishi Basi tujue kabisa haya yataendelea kutokea Hadi Kiama....
 
Na suala la utitiri wa Clearing and forwarding agents uangaliziwe.
Siku hizi kumekuwa na utitiri wa Clearing and forwarding agency companies na zingine ni za mifukoni kabisa kwa sababu ya urahisi wa kuzìanzisha na huku kukiwa na uchache wa mizigo inayokuja na kupitishwa nchini matokeo yake ma agents wengi siku hizi ni kama vishoka tu,watu wanalizwa sana na hao hao ma agent ndio wamekuwa kama ndio wanasaidia kukwepa sana kodi wakishirikiana na watumishi wa mamlaka za ukusanyaji mapato(TRA)
Bandari haina ufanisi na hata mamlaka zingine kama TRA,TMDA,TBS,GCA wamekuwa na ufanisi mdogo sana.
Napendekeza hizi Clearing agents ziwe chache zenye sifa ya kimtaji na kiuweledi na hizo ndio zitoe ajira kwa agents wengi ufanisi utapatikana tu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Tasac kaporwa mizigo karibia yote wacha wagombanie ndo kufungua uchumi huko
 
Attachments

  • IMG-20220703-WA0003.jpg
    IMG-20220703-WA0003.jpg
    51.8 KB · Views: 13
Hizi ndio akili za kawaida alizokua anasema Samia.
 
Naomba kuuliza, tulifanya PPP na TICS, tukabinafsisha baadhi ya Mageti, Je ufaninisi uliongezeka?je mapato yaliongezeka? Je tumejifunza nn kutokana na mkataba huo?
Solution niionayo mimi.

1. Tukamilishe upanuzi wa bandari ya Tanga - Uganda, Rwanda na Burudi ile ndo iwe destionation port yao.- hii sio tu itapunguza msongamao Dar bali pia itafufua uchumi wa Tanga.

2. Tukamilishe upanuzi wa Bandari ya Mtwara - Mizigo ya Zambia na Malawi ipitie huko. Hii nayo itapunguza msogamano Dar na kukuza mji wa Mtwara.

3. Dar ibaki na mizigo ya Congo na Mizigo ya Ndani tu.

4. Tujenge highway kwenda mikoa yote inayopakana na inchi jirani.

5. Tuwajengee uwezo watanzania waweze kuziendesha bandari zao..kuwalaumu na kuwatumbua kwakua tu hawaperfom km bandari za nje ni km kuwatumbua viongozi Simba na Yanga kwakua tu hawaendeshi vilabu vyao km na team za ulaya, uarabuni or asia...by theway kwann serikali haijalaumu kwa kutojiendesha km serikali za ng'ambo?
These people need exposure, resouces, support and political will.

6. Mimi sio muumini wa Bagamoyo. Sababu kuu ni kua tukiijenga hii bandari za Tanga na Mtwara ndo bai bai..no one will want to go there, 2nd ipo karibu sana na Dar which doesnt make sense...
Umemaliza kiongozi
 
Bandari ya Bagamoyo haiepukiki! Ukipita barabara ya sea view upanga hadi masaki unaona meli nyingi ziko kwenye foleni! Zile meli zinakaa foleni hadi two weeks!

Kwa mendoza ule hatuwezi pata ufanisi kwenye bandari kamwe

Ukiangalia duniani nchi nyingi sana zina bandari nyingi kwa sababu hizi
Kama biashara ipo Kwanini tusiwe na International Ports zaidi?

Kwa mfano tu Philippine wana Major international Ports 10
Hiyo ya 3 ina ukubwa wa 150 hectares inaitwa Batangas
Na wanapokea watalii 10m kwa mwaka

Sasa ni lazima twende na wakati kwani tangu tupate Uhuru mamilioni ya watu wameongezeka

Kwa hiyo tunakuwa masikini zaidi na zaidi kwa kukosa maarifa huku tukijifanya wajuaji
 
Kwel

Kweli kabisa
 
Naunga mkono hoja. Bado kuna changamoto za trafiki njiani mteja anasubiri mzigo lubumbashi njiani unasimamishwa mara 50 na trafiki hizi sekta zingine ziwe zinaenda na kasi ya kufungua uchumi la sivyo tutakuwa tunazunguja palepale.
 
1. Lazima tukubali kuwa Bandari ya DSM haiwezi kuwa efficient kwa sababu imekuwa finyu kuhimili idadi ya mizigo, Meli na Magari kiushindani
Ushauri wako umefeli kuanzia hapa.

Huko chini sijasoma, lakini ulitakiwa ujikite hapa kwenye hii hii yenye ufinyo kabla hujaenda kwingine kokote.

Ukipewa kazi wewe utakuwa hovyo zaidi kwa sabau inaonyesha huna 'focus'. Unaacha tatizo lililopo sasa unaanza kuzunguka kwingine?

Ngoja nikaangalie huko chini umeweka takataka gani.
 
Naomba kuuliza, tulifanya PPP na TICS, tukabinafsisha baadhi ya Mageti, Je ufaninisi uliongezeka?je mapato yaliongezeka? Je tumejifunza nn kutokana na mkataba huo?
Solution niionayo mimi.

1. Tukamilishe upanuzi wa bandari ya Tanga - Uganda, Rwanda na Burudi ile ndo iwe destionation port yao.- hii sio tu itapunguza msongamao Dar bali pia itafufua uchumi wa Tanga.

2. Tukamilishe upanuzi wa Bandari ya Mtwara - Mizigo ya Zambia na Malawi ipitie huko. Hii nayo itapunguza msogamano Dar na kukuza mji wa Mtwara.

3. Dar ibaki na mizigo ya Congo na Mizigo ya Ndani tu.

4. Tujenge highway kwenda mikoa yote inayopakana na inchi jirani.

5. Tuwajengee uwezo watanzania waweze kuziendesha bandari zao..kuwalaumu na kuwatumbua kwakua tu hawaperfom km bandari za nje ni km kuwatumbua viongozi Simba na Yanga kwakua tu hawaendeshi vilabu vyao km na team za ulaya, uarabuni or asia...by theway kwann serikali haijalaumu kwa kutojiendesha km serikali za ng'ambo?
These people need exposure, resouces, support and political will.

6. Mimi sio muumini wa Bagamoyo. Sababu kuu ni kua tukiijenga hii bandari za Tanga na Mtwara ndo bai bai..no one will want to go there, 2nd ipo karibu sana na Dar which doesnt make sense...
Kumbe hakuna kitu!
 
Ushauri wako umefeli kuanzia hapa.

Huko chini sijasoma, lakini ulitakiwa ujikite hapa kwenye hii hii yenye ufinyo kabla hujaenda kwingine kokote.

Ukipewa kazi wewe utakuwa hovyo zaidi kwa sabau inaonyesha huna 'focus'. Unaacha tatizo lililopo sasa unaanza kuzunguka kwingine?

Ngoja nikaangalie huko chini umeweka takataka gani.
Umeshawai hata finally bandarini? Usikute unaongea hata Dar hujawai fika!

Waliopo Dar wanaopita njia ya baharini wakishuhudia foleni ya meli hadi mwezi kila siku hawapingi wewe ulioko kijijini huko unapinga pinga tu hapa
 
Back
Top Bottom