Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe nanyi
Leo Rais wa JMT amemtumbua Mkurugenzi wa Bandari Ndug Erick Hamis.
Pamoja na kumtumbua Rais Samia amelalamika juu ya efficiency ya Mamlaka yetu ya Bandari na kusema kuwa Mamlaka hii ingekuwa inafanya kazi vizuri ingeweza kuchangia hata nusu ya mapato ya Bajeti yetu. Ni kweli kabisa naungana na Rais Samia kwenye hili!
Mfupa wa Bandari ni mfupa uliowashinda Marais karibu wote waliowai kutawala Tanzania! Hii imekuwa kawaida kila Rais mpya akiingia au Waziri Mkuu mpya akiteuliwa sehemu ya kwanzq kwenda kulalamika na kutumbua imekuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Kwa kumbukumbu zangu kuanzia kwa Mkapa, Kikwete, Magufuli hadi sasa Samia, Bandari hapajawai kupoa.
Hoja yangu kuu kwenye hili ni kwamba inawezekana sana bado hatujajua shida ni nini hasa pale Bandarini na kwa uelewa wangu mdogo napenda leo nimshauri Mhe Rais mambo ya kufanya na naamini kama nilivyoshauri kuhusu Ngorongoro na ikafanyika na sasa imefanikiwa basi nashauri juu ya hili la Bandari na naamini ikifanyika itafanikiwa
1. Lazima tukubali kuwa Bandari ya DSM haiwezi kuwa efficient kwa sababu imekuwa finyu kuhimili idadi ya mizigo, Meli na Magari kiushindani
2. Lazima tukubali kuwa Serikali haiwezi kuendesha bandari kwa ufanisi tunaoutaka katika dunia hii ya ushindani. Bandari kubwa zote duniani na zinazofanya vizuri kwenye soko la ushindani kuanzia Dubai, Hong Kong, Singapore, New York na nyinginezo, zinaendeshwa either kwa sehemu kubwa na private sector au kwa ubia baina ya Serikali na Private Sector
Hivyo ili kufanikiwa kupata ufanisi hapa Tanzania kwenye sekta ya Bandari , Lazima tutake tusitake, tufanye yafuatayo
a. Kwa haraka sana, Ijengwe Bandari ya Bagamoyo ambayo iwe na Gati zisizopungua 40. Bandari hii iendeshwe na Private sector with exception kwenye masuala ya Ulinzi, Usalama na Kodi
b. Sekta binafsi wapewe pia fursa ya kujenga Miundombinu ya Reli na barabara kuunganisha Bandari ya Bagamoyo na Jiji la Dar es Salaam ikiwemo reli ya kati SGR na TAZARA
c. Bandari za DSM, Tanga, Mwanza na Kigoma na Mtwara ziendeshwe kwa ubia na Private sector. Serikali isimamie masuala ya kodi , ulinzi na usalama tu!
d. Barabara ya Mandela Road( dsm) itanuliwe kuwekwa njia 8 kutokea Bandarini hadi Ubungo na utanuzi wa njia 6 uendelee kutoka Kimara hadi Ubungo. Hii ni ili kuleta ufanisi wa usafirishaji mizigo katika Jiji la Dsm. Ikiwezekana Private sector washirikishwe kwenye hili.
e. Kulikuwa na Mpango wa Kujenga Barabara ya Malori kutokea Bandarini hadi Chalinze. Mpango huu ufufuliwe na barabara hii ijengwe hata kwa kutumia Private sector! Fedha zitarudi haraka sana hata kwa toll tax!
Nchi kubwa duniani ziliona hili na wakaamua kufanya! Hata kwa Tanzania Serikali iking'ang'ania kuendesha bandari kila siku mtaishia kushikana uchawi na kutumbuana!
Ni suala la kuamua tu na wakati ni sasa