USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

nimekugongea senks hata kabla sijamaliza kusoma...jitu ziiima limekaa kusubiria kuwa maalum hapo hapo linajidai talila nyingi oooohh usawa usawa...!!!!!!
 
Nafikiri ifike mahali sasa viti maalum vitengwe tu kwa ajili ya watu maalum kama Walemavu, Wazee na makundi mengine ambayo hayawezi kustahimili kampeni katika majimbo.

Nadhani Vifutwe tu hata wale wanaoenda Kuwakilisha Makundi Maalumu kama Walemavu n. nao wakifika Mjengoni wanamezwa na System na Midomo yao inajifunga baada ya Miamala yao kusoma Mamilioni kila mwezi..Hivi viti maalumu havina Tija... vifutiliwe Mbali
 
Na wakinyanyaswa kijinsia na hao waliowapa viti wanaaza kulalama!!
 
Unajua wanawake wenyewe kwa wenyewe hawapendani!

Maana % kubwa ya wapiga kura ni akina mama! sasa wenyewe huwa huchagua wanaume ktk majimbo...halafu eti kukaa kusubiria usawa wa viti vya upendeleo! Yaani viti 95!!

Yaani Haiingii akilini!

Mama lao mko hapo?
 
Kweli aiseee viti maalum havina maana kabisaaa!
 
Viongozi wanafuata maagizo kutoka nchi za magharibi. Na wao pia wanajipati rushwa ya ngono mambo kwisha. Viti maalum ni upuuzi mtupu.
 
Kwa kweli mkuu hivi viti maalumu havina tija kwa watanzania, hizi ni gharama za kupuuzi embu angalia hapa chini mishahara pamoja na marupurupu yao;
12,000,000 x 95 kwa mwezi = 1,140,000,000 kwa mwaka 1,140,000,000 x 12=13,680,000,000 kwa miaka mitano 13,680,000,000 x 5=68,400,000,000/= ukichanganya na kiinua mgogngo itakuwa 40,000,000 x 95 =3,800,000,000+68,400,000,000= 72,200,000,000/=

Kwa hiyo taifa linapoteza bilioni 72 kwa wabunge wa viti maalumu

My take: serikali inatakiwa ituambie ni kazi gani hawa watu wanafanya ambayo inaweza kuzalisha zaidi ya Bilioni 72 kwa miaka mitano ili waweze kupata mishara yao na taifa lipate faida pia.
 
mhhhhhhhhhhhhhhhhhhh nimewaelewa ila sasa kwa Kura za maoni tutaweza kupita tena jamani maana pale napo mijicho ya kina baba walewale waandaa vitu maalumu wanatumbua ....
 
na ule wizi wa kura kwenda kubadilisha matokeo saa nane usiku nao .....
na kugawa rushwa saa 10 usiku nako...................
Bora tu tujisubirie viti maalum Mpaka Katiba itakapobadilishwa
 
viti maalum ni kuongezea mzigo kwa mwananchi wa kawaida.

Kiti maalum ilitakiwa iwe ni kwa ajili kumchagua waziri mtu ambaye yupo nje ya bunge ,amteue kiti maalum then ampe uwaziri kama rais anamtaka.
 

Red and Bold: Imenifanya nizimie dakika 3
 
Hivi Kenya na Katiba yao ya zamani na mpya walikuwa na viti maalum? Wanawake wa Kenya wanaeleweka duniani kwa kazi zao jasiri na sio kwenda bungeni kulala na kufitiana

Mfano Mzuri Prof. Waangari
 
Hivi Kenya na Katiba yao ya zamani na mpya walikuwa na viti maalum? Wanawake wa Kenya wanaeleweka duniani kwa kazi zao jasiri na sio kwenda bungeni kulala na kufitiana

Mfano Mzuri Prof. Waangari

is there difference btn kenyan and tz women?
 
Naunga mkono hoja. Tena kama Anna yuko bungeni tangu awamu ya kwanza, ameshajenga uzoefu mpaka akapata uzeefu baado anazuia watu wengine kuleta mawazo mapya bungeni. kuna haja ya kutunga sheria kuwa mtu anapendelewa kipindi kimoja, vingine aingie Jimboni kama alivyo fanya Halima Mdee.
 
Mungu wanguuuuuuuuuuuuuuu........................ Hivi hii hesabu shangingi limo humooooooooooooo................. Mshahara wa dereva......... Mafuta ya shangingi................... YAAANIIIIII HIVI VITI VIFUTWE..............

Jamani hivi umaalumu wake upo vipi..................... ???? Ulemavu, umaarufu................mi thijui...........
 

hapo kwenye red&bold ndipo mafisadi wasipotaka kusikia mtu, ama anaota au anasema laivu
 
Ingekuwa vipindi viwili tuu sasa kuna watu kama akina Lediana munq'onq'o utafikiri huko Iringa hakuna watu wengine anaenda kipindi cha nne hii ni too much
 
Ndo maana tunasema katiba lazima ibadilishwe.
Mbona Mdee,Nkya na Tibaijuka wamegombea na wamepita,hao wengine nini kinawashinda?
Hebu angalia akina Anna Abdalah & co kila msimu ubunge wa viti maalum,hawaoni aibu?
Tubadilike!!!
 

Uko sahihi sana mwanaJF,licha ya mzigo pamoja na matatizo mengi ambayo yanatuzunguka ukijaribu kuchunguza hayo majina wengi ni mabibi zao mfano uliowataja hapo juu na hata wengine ukiwaangalia wanaweza kuchangia nini unaona wengi wao hakuna wanachofanya.Inatia uchungu sana wanapogeuza sera za kumkomboa mwanamke kuwa ni nafasi yao ya kusindikizana na mahawara bungeni.Upendeleo wao hauna tija,nafikiri itakuwa vizuri wakiondolewa.manake walemavu,wasiojiweza,vijana,wanawake nk vyote hivi viko sehemu ambazo kuna wabunge wa kupigiwa kura na ndio hao hao wawakilishe na kuwasaidia kutatua matatizo sidhani kama hao wabunge wako busy hivyo,sana sana tunawapa wabunge muda wa kutuibia na kustarehe badala ya kushughulikia matatizo yetu.
 

si suala la wanawake kupendana na kutopendana unless uwe unataka wanawake wapigie kura wanawake wenzao kwa sababu tu ni wanawake.

vitu maalum ni upuuzi, hasa ukizingatia kuwa vinaruhusu waingie wanawake ambao tayari tulikwisha wakataa majimboni.

vitu maalum ni upuuzi, kwa sababu wanaochaguliwa hawana wanaemuwakilisha kutoka jimboni kwa hiyo hakuna anaeweza kuwawajibisha.

vitu maalum ni upuuzi, kwa sababu hakuna vigezi wakati wa kuwachagua.

kama mwanamke hawezi tusilazimishie kuwa anaweza. mwache akae chonjo. Tumefanya kazi ya kutoa maamuzi mazito ya nchi kuwa nyepesi kiasi cha kuwa yoyote yule anaweza kuifanya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…