USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Hivi viti maalumu vikiondolewa kutakuwa na wanawake wangapi bungeni? Kuuondoa mfumo dume na kupata uwiano mzuri kati ya wanawake na wanaume katika vyombo vya utawala na maamuzi ni process ndefu....na nimekuwa naamini viti maalumu ni sehemu ya mchakato huo. Kusema tu tuondoe viti maalumu bila kusema tufanye nini ili kuleta uwiano bora wa kijinsia katika bunge nadhani ni irresponsible. Labda kama tunajadiliana katika premise kwamba gender imbalance is not a problem!
 
Naona wengi mmeshangaa kusikia Regia Mtema nae anatoa kauli kama hii, mkumbuke nae ni MWANASIASA na wanasiasa wote ni waongo
 
Inawezekana hoja yangu ni dhaifu kwa mtazamo wako, to me is very strong u know. Kwani unafikiri mfumo dume upo kwa wanaume tu? Ukweli utabaki kuwa ukweli tuna mfumo dume.

Remmy unanichekesha kwanza wapiga kura wengi ni wanawake halafu wewe unaamini kabisa mfumo dume upo sasa kama upo mbona kuna wanawake wanashinda? Kuanzia Halima Mdee, Dr Batilda, Anne Kilango, Anna Makinda wanashindaje? Basi wanaowaangusha sio wanaume bali wanawake wenyewe! Mfumo dume remains a myth and just an excuse for your guys to have your way to parliament. Why am I saying this:

a. Kuna watu wamekuwa wabunge wa kuteuliwa kila siku wanabakia wa kuteuliwa. Sasa kama mnasaidiwa ili muweze kuwa wabunge wanaoweza kuwatetea wananchi unasemaje hawa wabunge wa kuteuliwa ambao kwa miaka karibu 10 wao ni wabunge wa kuteuliwa wanafanya nini?

b. Kumteua mbunge kuwakilisha jimbo kunategemea mahitaji ya mkoa husika sasa tuwaulize mliwauliza wananchi kama wanahitaji wawakilishi zaidi ili mpate kuteua hao wabunge viti maalum?

c. Tabia za baadhi ya wabunge zinaleta mashaka sana utendaji wao mfano kuna mmoja anaitwa Catherine (no disrespect but bado hajaiva hata kuwa mbunge wa mtaani kwetu), Mwengine huyu Regia vile vile bado anahitaji kujifunza, Kuna mmoja mwengine mweupe wa CCM ana hamaki kama mkizi kijana mdogo mwanamama. Mama Rwakatare naye a controversial figure. Aina hii ya wabunge ndio wanaoenda kutungia sheria za nchi hii kama character zao ni hizi you wonder the relevancy and importance of the special seats.

d. Uteuzi wa wabunge wa viti maalum ni wa kutia shaka vile vile na ndio maana watu wanapelekea kuamini kuna upendeleo fulani unaendelea. Mfano watoto wa wabunge wengine ndio wamepewa viti maalum. Au watu waliokuwa mawaziri waliopita ndio wanapewa viti maalum. etc. Sasa mnapeana viti kwa upendeleo huo msaada kwa akina mama uko wapi? Kwanini viti maalum msitafute watu wanaojitolea kwa jamii wakaenda huko kama msaada ni akina mama.

c. Tukianza na mfumo dume kuna akina albino nao watadai haki vile vile ya kuwakilisha. Kuna wenye ulemavu wa viungo nao watadai viti maalum. Kuna wasioona nao watadai viti maalum. Mwisho wa SIKU HATA MASHOGA NAO WATAOMBA VITI MAALUM.

d. What happened ikiwa wanawake mkiwa wengi KIUONGOZI na wanaume wa chache je na wanaume waanzishe malalamiko? Sasa hivi kuna wapiga kura wengi ni wanawake na je WANAUME NAO WANAATHIRIWA NA MFUMO JIKE???
 
dah! hata kama lugha iliyotumiwa na mleta mada imekukera hususa hilo la "kuashiria" wabunge wa viti maalum/kuteuliwa ni
vimada ilibidi uonyeshe busara zaidi na sio kujishusha kiasi hiki.[

nasita kusema hii komenti yako imekaa kama vile umeitoa baada ya kukurupushwa usingizini. pole sana

QUOTE=Regia Mtema;2829720]Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.[/QUOTE]
 
Hivi tatizo lako ni uwakilishi tu? yaani nani wa kumtetea si ndio? siwezi kujieleza wee hapa kwani siwezi kuiondoa mind set yako iliyokwisha pevuka kwa mawazo kuwa wanamwakilisha nani. Hivi hujaona kazi anayoifanya Regia juu ya watu wa Kilombero? Huyo Mteketa kafanya nini hasa? hebu toa hesabu hapa mbele za Mungu mpaka sasa, maswali mangapi kauliza kuwatetea hao wana Kilombero?au hata speech ngapi kachangia bungeni kutetea wana kilombero? Anyway viti maalumu viondolewe kwani imekuwa kero, chuki, wivu na dharau kwa wanawake.

Hiyo kufanya kazi zaidi ya mwakilishi halali hailalishi kuwepo kwa viti maalumu. Kwani so far tukifanya cost and benefit analysis ya viti maalumu, hasara ni nyingi kuliko faida. Huyo Regia hana legitimacy ya kusema anawawakilisha wananchi ambao hawakumchagua.

Hawa wabunge wa viti maalumu hawana tofauti na wale wanajiita ni wabunge waliopita bila kupingwa; nao hawana legitimacy ya kuwasemea watu ambao hawakuwachagua!
 
Hivi viti maalumu vikiondolewa kutakuwa na wanawake wangapi bungeni? Kuuondoa mfumo dume na kupata uwiano mzuri kati ya wanawake na wanaume katika vyombo vya utawala na maamuzi ni process ndefu....na nimekuwa naamini viti maalumu ni sehemu ya mchakato huo. Kusema tu tuondoe viti maalumu bila kusema tufanye nini ili kuleta uwiano bora wa kijinsia katika bunge nadhani ni irresponsible. Labda kama tunajadiliana katika premise kwamba gender imbalance is not a problem!

Hapo ndipo ninaposimamia mimi, uwiano bungeni utakuwaje? maana tunauhakika hawatachagulkiwa vya kutosha.
 
Hivi viti maalumu vikiondolewa kutakuwa na wanawake wangapi bungeni? Kuuondoa mfumo dume na kupata uwiano mzuri kati ya wanawake na wanaume katika vyombo vya utawala na maamuzi ni process ndefu....na nimekuwa naamini viti maalumu ni sehemu ya mchakato huo. Kusema tu tuondoe viti maalumu bila kusema tufanye nini ili kuleta uwiano bora wa kijinsia katika bunge nadhani ni irresponsible. Labda kama tunajadiliana katika premise kwamba gender imbalance is not a problem!

Mkuu, kuna vitu vingine ukivifanya unakua against nature. Suala la kuwa na gender balance katika vyombo vya utawala na maamuzi halitakuja kufanikiwa kamwe. Hawa viumbe (wanawake) wametoka kwenye ubavu wetu, halafu itawezekanaje kuwa sawa na wanaume kwa asilimia 100?!?

Hawa wanawake wanapaswa wapambane hivyo hivyo, watakaofanikiwa ndio hao wanakuwa wawakilishi wa wenzao. Hata katika nchi zilizoendelea gender balance in democratic political systems is very dubitable.
 
Remmy unanichekesha kwanza wapiga kura wengi ni wanawake halafu wewe unaamini kabisa mfumo dume upo sasa kama upo mbona kuna wanawake wanashinda? Kuanzia Halima Mdee, Dr Batilda, Anne Kilango, Anna Makinda wanashindaje? Basi wanaowaangusha sio wanaume bali wanawake wenyewe! Mfumo dume remains a myth and just an excuse for your guys to have your way to parliament. Why am I saying this:-
a. Kuna watu wamekuwa wabunge wa kuteuliwa kila siku wanabakia wa kuteuliwa. Sasa kama mnasaidiwa ili muweze kuwa wabunge wanaoweza kuwatetea wananchi unasemaje hawa wabunge wa kuteuliwa ambao kwa miaka karibu 10 wao ni wabunge wa kuteuliwa wanafanya nini?

b. Kumteua mbunge kuwakilisha jimbo kunategemea mahitaji ya mkoa husika sasa tuwaulize mliwauliza wananchi kama wanahitaji wawakilishi zaidi ili mpate kuteua hao wabunge viti maalum?

c. Tabia za baadhi ya wabunge zinaleta mashaka sana utendaji wao mfano kuna mmoja anaitwa Catherine (no disrespect but bado hajaiva hata kuwa mbunge wa mtaani kwetu), Mwengine huyu Regia vile vile bado anahitaji kujifunza, Kuna mmoja mwengine mweupe wa CCM ana hamaki kama mkizi kijana mdogo mwanamama. Mama Rwakatare naye a controversial figure. Aina hii ya wabunge ndio wanaoenda kutungia sheria za nchi hii kama character zao ni hizi you wonder the relevancy and importance of the special seats.

d. Uteuzi wa wabunge wa viti maalum ni wa kutia shaka vile vile na ndio maana watu wanapelekea kuamini kuna upendeleo fulani unaendelea. Mfano watoto wa wabunge wengine ndio wamepewa viti maalum. Au watu waliokuwa mawaziri waliopita ndio wanapewa viti maalum. etc. Sasa mnapeana viti kwa upendeleo huo msaada kwa akina mama uko wapi? Kwanini viti maalum msitafute watu wanaojitolea kwa jamii wakaenda huko kama msaada ni akina mama.

c. Tukianza na mfumo dume kuna akina albino nao watadai haki vile vile ya kuwakilisha. Kuna wenye ulemavu wa viungo nao watadai viti maalum. Kuna wasioona nao watadai viti maalum. Mwisho wa SIKU HATA MASHOGA NAO WATAOMBA VITI MAALUM.

d. What happened ikiwa wanawake mkiwa wengi KIUONGOZI na wanaume wa chache je na wanaume waanzishe malalamiko? Sasa hivi kuna wapiga kura wengi ni wanawake na je WANAUME NAO WANAATHIRIWA NA MFUMO JIKE???

Nakubaliana na wewe kuwa wanawake ndo wapiga kura ingawa sina uhakika na asilimia, na nimesema mfumo dume si kwa wanaume tu wapo wanawake wengi wamewabeza wanawake wenzao kuwaona hawawezi.

Swali lako la b, yawezekana walipoamua kuingiza vitimaalumu walifanya study unluck i was not there na sijui historia yake.

Swali la c, nauliza how pure wabunge wa majimbo they are? au je hakuna wabunge wababa ni vilaza? Mimi naona asilimia ndogo hata haizidi 30 ya wabunge wanaume ni wazuri, je unasemaje katika hili? tuwafanyaje hawa? wako safi kwa kuwa ni wamajimbo? hivi ni kweli in every sekta tunataka watu wote wawe wazuri? mbona kila eneo tuna watu wa aina zote? ni wabunge tu wa viti maalumu? no way? Tujenge hoja nyingine lakini si ya uzuri.

Vipi uteuzi wa kura za maoni kwa wa majimbo? je hatuna watoto wa wakubwa? hatuna walio na uhusiano na wakubwa? kwenye idara nyingine serikalini au kwenye ajira hakuna nepotisim? ni vitimaalumu tu?

Swali lako la e, mi naona yes wakidai kupata wawakilishi wafanyiwe hivyo, suala si uwakilishi? what the problem? money?

Swali la mwisho, tunataka uwiano unaokubalika, wamama wakizidi ni problem wala si upande wa wanawake tu.
 
Hiyo kufanya kazi zaidi ya mwakilishi halali hailalishi kuwepo kwa viti maalumu. Kwani so far tukifanya cost and benefit analysis ya viti maalumu, hasara ni nyingi kuliko faida. Huyo Regia hana legitimacy ya kusema anawawakilisha wananchi ambao hawakumchagua.

Hawa wabunge wa viti maalumu hawana tofauti na wale wanajiita ni wabunge waliopita bila kupingwa; nao hawana legitimacy ya kuwasemea watu ambao hawakuwachagua!

Legitimacy ni vidole sio? ameingiaje bungeni bila legitimacy? basi tanzania haifai, anyway.....
Demokrasia ni pana ni zaidi ya kupiga kura. Unaweza piga kura kumchagua mtu usiyemtaka vilevile, kwako likaonekana ni demokrasia kisa wamepiga kura. tunahitaji elimu ya uraia tz, walahi tena.
 
Nakubaliana na wewe kuwa wanawake ndo wapiga kura ingawa sina uhakika na asilimia, na nimesema mfumo dume si kwa wanaume tu wapo wanawake wengi wamewabeza wanawake wenzao kuwaona hawawezi.

Swali lako la b, yawezekana walipoamua kuingiza vitimaalumu walifanya study unluck i was not there na sijui historia yake.

Swali la c, nauliza how pure wabunge wa majimbo they are? au je hakuna wabunge wababa ni vilaza? Mimi naona asilimia ndogo hata haizidi 30 ya wabunge wanaume ni wazuri, je unasemaje katika hili? tuwafanyaje hawa? wako safi kwa kuwa ni wamajimbo? hivi ni kweli in every sekta tunataka watu wote wawe wazuri? mbona kila eneo tuna watu wa aina zote? ni wabunge tu wa viti maalumu? no way? Tujenge hoja nyingine lakini si ya uzuri.

Vipi uteuzi wa kura za maoni kwa wa majimbo? je hatuna watoto wa wakubwa? hatuna walio na uhusiano na wakubwa? kwenye idara nyingine serikalini au kwenye ajira hakuna nepotisim? ni vitimaalumu tu?

Swali lako la e, mi naona yes wakidai kupata wawakilishi wafanyiwe hivyo, suala si uwakilishi? what the problem? money?

Swali la mwisho, tunataka uwiano unaokubalika, wamama wakizidi ni problem wala si upande wa wanawake tu.
Kote hukko tutafika maadam vita yetu ni mfumo dume ama asemavyo Mdondoaji...Kama tumeliona hili lete jingine tutalijadili maanake tumeisha sema sana kuonyesha mfumo mbaya wa kiutawala. Na hili la viti maalum ni mojawapo yaani hatukuwa na mwanamke mwenye uwezo wa kuwa spika hadi tumchague mpambe kupitia viti maalum... kweli hii inaingia akilini?
 
...... Hawa viumbe (wanawake) wametoka kwenye ubavu wetu, halafu itawezekanaje kuwa sawa na wanaume kwa asilimia 100?!?...[/I]
Kwamba wao hawatokani na muunganiko wa mbegu na yai kama ilivyo wanaume? Kama lengo lako ni kusema wanawake ni tofauti na wanaume....hilo nakuunga mkono......na ndio mojawapo ya sababu uwiano wa kijinsia unahitajika!
 
Kwamba wao hawatokani na muunganiko wa mbegu na yai kama ilivyo wanaume? Kama lengo lako ni kusema tupo wanawake ni tofauti na wanaume....hilo nakuunga mkono ni mojawapo ya sababu uwiano wa kijinsia unahitajika!

Uwiano wa kijinsia unahitajika wapi na kwa nini?

Hivi kama wanawake hawana interest au uwezo wa kuwa viongozi ni lazima tuwape nafasi ili kuweka uwiano?
 
Gaijin, pengine tukitaka kulitizama suala hili vizuri tunaweza kutumia model ya familia. Nini nafasi ya mwanamke katika familia? Vipi kama katika familia kama mwanamke hashirikishwi katika maamuzi au uendeshaji wa familia kwa ujumla?
Hivi ni kweli wanawake hawapendi kushiriki katika maamuzi....ama ni mfumo mbuvu tu umewaweka kando? Kurekebisha mfumo huu ili uwe friendly kwa jinsia zote ni suala la muda mrefu na ni lazima tuanzie mahali fulani. Ni kweli kuna matatizo ya utekelezaji wa hayo mabadiliko lakini sifikirii kama suluhisho ni kuacha kufanya chochote.
 
Hivi hao wanawake waloweza majimboni wananini kilichowawezesha kuweza na hao wengine ikabidi lazima wapewe kwenye sahani?

Suali unalikosea kuliuliza.....sio "jee wanwake hawapendi kushiriki katika maamuzi" bali "jee wanawake hawapendi heka heka za kutafuta ubunge?". ....Ni sawa na suala la kuwa wanawake wangependa kuwa wahandisi lakini hawapendi heka heka zihusianazo.

Naamini mwanamke akiwa anataka kuwa mbunge hakuna mfumo unaomzuwia, sawa na akiwa anataka kuwa mhandisi
 
So far ni wachache mno 'walioweza/wanaoweza' hekaheka hizo ukilinganisha na wanaume. Sasa labda tujiulize...trend hiyo ni suala la mwanamke tu au ni suala la kimfumo. Kama unaona ni suala la mwanamke tu then i rest my case......lakini kama ni suala la kimfumo(kama ninavyoamini mimi), then kunahitajika kufanyika kitu kurekebisha hali hiyo.

Hata kwenye hilo la uhandisi bado kumekuwepo na jitihada kama hizi za kujaribu 'kuwapa' nafasi wasichana wengi zaidi. Pre entry hapo udsm wakati inaanza iliwalenga zaidi wasichana na kwa maoni yangu so far imefanikiwa sana....nimeona sasa vyuo vingi zaidi vimeiga na kuongeza wigo kutoka ule wa uhandisi/sayansi na kuhusisha taaluma nyingine.
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.

Suala la wabunge KUOANA kwakweli halihitaji kifungu kwenye katiba Mpya hata kidogo. I say NO. Why?
Kwasababu suala la mahusiano ni individual affairs, mwananchi ana uhuru wa kuoa au kuolewa na yeyote haijalishi status, suala la KATIBA ni "Tanzania Nation Affair" and this is what we care about, not individual affairs. Kama katiba itazuia wao kuoana but haijawazuia kugongana then whats the point? i say its bull shit, where did you get this idea from madam, khe?
Ndo yale yaleeee, tunapeleka bungeni vilaza, ona sasa pendekezo la mzaha hiloo...........

Kweli Tz tumeishiwa mawazo sasa, duh!!
 
SMU,

Kuna mawili hapa. Inawezekana kuwa ni suala la mfumo pia lakini zaidi ni suala la wanawake au uanamke na jinsi jamii inavyolichukulia. Hata katika hali ya mazingira sawa bila ya kuwepo mfumo dume wa aina yoyote, basi wanwake wengi zaidi wana-opt kusoma social science kuliko natural science kwa mfano (hilo hata nchi zilizoendelea lipo hivyo). Naamini ni hivyo hivyo kwenye siasa. Sio kama hawana uwezo, hawataki. Na hilo huwezi kulilazimisha kamwe.

Kwa hiyo huwezi kumchukua wanawake 100 kati ya wanawake milioni kumi Tanzania ukawapa ubunge bila ya kuuhangaikia kwa chochote ukatarajia kuwa umeondoa mfumo dume. Sana sana ni kuwa umeuongeza. Kwa sababu wanawake wataanza kuwakilishwa na watu wasiokuwa na uwezo na hivyo kuonekana hawawezi kuwa viongozi.

Iwapo tunahitaji kulazimisha wanwake wawe kwenye nafasi ya uongozi basi walau tufanye hivyo kwa kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanapata elimu, hivyo kuweza kuchukua uongozi kuanzia majumbani mwao, makazini na ultimately kwenye bunge.

Naamini bilioni 90 zingeweza kujenga mabweni bora zaidi kwa shule za wasichana, na walimu wa kuaminika, ili kuhakikisha wanawake wanaweza kusoma kwa amani
 
Back
Top Bottom