Ni ukweli usiopingika kuwa CCM sasa wanaiogopa CHADEMA kuliko hata namna wanavyomwogopa Mungu.
Ukweli huu unatokana na ukweli kuwa, ni dhahili kuwa Watanzania wote sasa hivi wameona na wameelewa kuwa Chama cha Kweli cha Siasa ambacho kipo kwa ajili ya kuwapigania kweli ili kuwapatia maisha bora na maendeleo ya kweli ni Chadema.
Support kubwa wanayozidi kuipata Chadema kila siku kutoka kwa Watanzania kwa kutosaini Kanuni za Uchaguzi pamoja na kutaka Mabadiliko ya Katiba na Sheria za Uchaguzi ili kuwe na Uchaguzi Huru na wa Haki kusema kweli inawatesa sana CCM. Inawanyima usingizi hakika.
Sasaivi ukipita mitaani, ukipita kwenye vijiwe vya kahawa, vijiwe cha wacheza pool table, mitandanoni kuanzia twitter, Facebook, Instagram, Tiktok na kwingineko kote unaona namna Watanzania wanavyotoa maoni bila kupepesa macho kuunga mkono misimamo ya Chadema. Hili linawafanya CCM wawehuke sana.
Kinachonisikitisha ni kwamba, CCM baada ya kuogopeshwa na Chadema na kuchanganyikiwa, wanazidi kutumia hela za watanzania kufanya mambo ya ajabu badala ya kuziridisha hizo fedha Serikalini zikaboreshe barabara mbaya zinazowaathiri Watanzania kila siku.
Kinachonisikitisha ni suala kwamba badala ya CCM kujikita kutumia fedha za Watanzania kwa maendeleo yao ikowemo kuboresha madarasa yaliyochakaa wanayosoma watoto wa kitanzania masikini pamoja na mfumo wa elimu wanatumia fedha hizo kuwahonga mapandikizi waliyonayo huko Chadema kujaribu kuleta mtafaruko Chadema ili kuwakatisha tamaa Watanzania.
Makundi ya G55, Covid 19, Vyombo vya habari kuandika propaganda mfu dhidi ya Chadema na hawa wajinga waliofungua Kesi Mahakama Kuu eti kudai shughuli za Chadema zisitishwe kwa sababu chama kimeitenga Zanzibar ni ushahidi wa uhakika namna CCM wamechanganyikiwa na wanatumia fedha za Watanzania kwa shughuli za kipumbavu za kutengeneza mapandikizi Chadema ili yawanusuru Chama chao kutokana na kukataliwa na Watanzania kwa kiwango cha kutisha.
Nawashauri tu CCM. Watanzania wameona Chama Pekee cha Siasa kinachowapigania kweli ili wawe na maendeleo ya Uhakika ni Chadema, hivyo lolote mtakalofanya dhidi ya CHADEMA hamtafanikiwa.
Poleni sana CCM.