Ushauri wa bure kwa mchezaji Feisal Salum baada ya mchezo wa marudio kati ya Taifa Stars na Uganda The Cranes

Dogo anazingua. Mbaya zaidi mama yake naye siyo msaada kwake. Maana hata yale mahojiano yake alijikita zaidi kwenye kuongelea mabaya, kana kwamba mtoto wake hakuwahi kutendewa wema wa aina yoyote ile na Yanga; jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
 
Amekaririwa akisema huko unguja..kwamba akirudi yanga na afe..yanga kuna kitu wamemkwaza huyu kijana
Kama kingekuwepo, Yanga wangemkubalia kwa urahisi hilo ombi lake la kutaka kuondoka. Inawezekana hasira zake zote zimetokana na kukoda hilo dau alilo ahidiwa na hiyo timu iliyokuwa ikimtaka.

Na kwa bahati mbaya, alishindwa kutafsiri mkataba wake, na sasa ameamua kuchagua maisha ya popo! Anatambulika kama mchezaji wa Yanga, na wakati ukweli hauko hivyo.

Wakati mwingine nitashangaa sana kama ataitwa tena kwenye timu ya Taifa, na kutambulika kama mchezaji wa Yanga, asiyo ichezea kwa sababu zake binafsi.
 
Muda si mrefu ataikumbuka hata ile M4 aliyokuwa analipwa! Kwa kiwango kile cha jana hata Namungo hapati namba!
 
Kwani kafanya kosa gani?
Kwa mtazamo wangu, na kwa umri na akili zake; naona kosa lake kubwa ni utoto.

Hivyo kuomba radhi hadharani, ni uungwana kwa mchezaji wa kiwango chake. Na uzuri akifanya hivyo, hatapungukiwa na chochote.
 
Dogo anazingua. Mbaya zaidi mama yake naye siyo msaada kwake. Maana hata yale mahojiano yake alijikita zaidi kwenye kuongelea mabaya, kana kwamba mtoto wake hakuwahi kutendewa wema wa aina yoyote ile na Yanga; jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
Sisi waswahili professionalism huwa tunaweka pembeni katika masuala mengi tu ya Msingi. Michezo inahitaji sana nidhamu pengine kushinda nyanja nyingine kwasababu jambo dogo linalo onekana la kawaida linaweza kumpotezea mwekekeo mchezaji. Kwa hiyo ukisha tanguliza mambo ya kiswahili huwezi fika popote. Angalia Samata ambaye ndiye icon ya mpira wetu kwa sasa, ana nidhamu ya hali ya juu nje na ndani ya uwanjani toka yupo Simba. Asingekuwa na nidhamu angeishia tu TP Mazembe.
 
Muda si mrefu ataikumbuka hata ile M4 aliyokuwa analipwa! Kwa kiwango kile cha jana hata Namungo hapati namba!
Uko sahihi kabisa. Jana alikuwa ni yule Fei Toto wa JKU! Athari za kutokuwepo klabuni na wenzake, zimeshaanza kumuathiri. Bila shaka itamchukua muda kurejea kwenye kiwango chake cha awali.
 
Na thamani yake inapotea slowly..!!! Jana kwanza utadhani hakuwepo uwanjani.
Nina uhakika angekuwa ametokea kwenye klabu yake, angeanza kwenye kikosi cha kwanza. Ila ndiyo hivyo tena, hata alipopewa nafasi, hakuwa Fei yule tuliyemzoea.
 
Nakumbuka Samatta kuondoka Mazembe haikua rahisi Katumbi alikataa kumuachia ikabidi avumilie mkataba uishe aondoke bure baadae waka zungumza biashara ikafanyika
 
Ulichosema ni kweli kuna mda inabidi ujishushe ila mambo yaende,umemaliza kila kitu
 
Uko sahihi kabisa. Jana alikuwa ni yule Fei Toto wa JKU! Athari za kutokuwepo klabuni na wenzake, zimeshaanza kumuathiri. Bila shaka itamchukua muda kurejea kwenye kiwango chake cha awali.
Kwanza hapo ashukuru kuitwa. Ningekuwa mimi kocha🤣 angeangalia wenzie kwenye TV
 
Kuomba radhi ni kitendo tu cha uungwana, ili wakati fulani kupisha mambo mengine yaendelee. Na wala hakuna uhusiano na kuabudiwa.
Kwa nini mnakesha mkiomba aje kuwaomba radhi kwani amekiri kuwakosea? Acheni mambo zenu.
 
Ungekuwa umeajiriwa, ungeielewa kwa haraka sana mantiki yangu.
Kwani kawaambia anaishi kwa shida? Mnatumia geresha ya kumuonea huruma wakati yeye hana hata habari na nyie. Kama mnamuonea huruma, ongezeni mshahara wake maana ameshawaambia ana majukumu mengi ya kifamilia na mshahara mnaomlipa hautoshi. Kama hamuwezi, kaeni kimya.
 
kukubali kuichezea taifa stars jana kwa kutambulika kama mchezaji wa yanga amedhihirisha kwamba dogo hajitambui,ni dhahiri kabisa vishawishi vyenye nguvu ya pesa ndivyo vilivyomfanya awasingizie yanga mambo ya kipuuzi ili jamii imuone anaonewa aondoke kirahisi ni kama vile alivyofanya demu wa greenwood...SHAME ON HIM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…