Ushauri wa bure kwa TBWAY 360 wa EATV

Ushauri wa bure kwa TBWAY 360 wa EATV

Mi najiambiaga kila mafanikio yanaendana na umri,ukiyapata umri usiostahili lazma yakuyumbishe.
Hapa umeandika jambo muhimu sana ndio maana Mungu huwapa pesa vijana umri ukiwa umesogea kidogo kuwaepusha na mambo kama haya...yani huyu kagari ka kubandika sticker na kubandua mbwembwe nyingi hadi anataka kujiua.....
 
Hapa umeandika jambo muhimu sana ndio maana Mungu huwapa pesa vijana umri ukiwa umesogea kidogo kuwaepusha na mambo kama haya...yani huyu kagari ka kubandika sticker na kubandua mbwembwe nyingi hadi anataka kujiua.....
Tunayaona haya mkuu hata huku mitaani kwetu.
 
View attachment 710678
Umofia Kwenu wana JF,

Imeniladhimu nimuandikie waraka mfupi ndugu yetu Tonny Aka Tbway360 ili watu walio karibu nae au yeye akipitia humu JF aweze kuusoma.Nimeshawahi kukutana na Huyu jamaa mara kadhaa,mara ya kwanza nilimuona maeneo ya Mlimani city akiwa anatoka NSSF kufatilia nadhani mafao yake,nilimuona mtu wa vurugu sana kwenye gari lakini nikaona bado kijana labda bado ana ushamba wa gari.

Mara ya Pili niliona Clip mtandaoni akikimbiza gari kwa speed ya ajabu kisha akakamata Hand-Brake gari ikarotate ikarudi ilipotoka na ilikuwa eneo la wazi kabisa barabarani maeneo ya ununio,nikaona huyu jamaa kumbe ndi0 hulka yake kukimbiza magari kwa speed za hatari >160km/hr tena maeneo ya mjini.

Mara ya tatu tena nilimuona live akiwa quality plaza katoka kwenye ATM kutoa pesa,alitoka na speed kubwa sana hadi nikashangaa inakuwaje anatoka na speed kubwa namna ile wakati mbele tu kama mita 20 kuna foleni? Nikagundua jamaa bado haijui gari vizuri,yes ni dereva lakini haijui gari vizuri,mtu anayeijua gari lazima ataiheshimu.

Kilichonituma niandike huu waraka ni kwamba Jana Tbway360 alikula mzinga wa hatari na gari kubilingika mara mbili,kwa mujibu wa maelezo yake eti anasema alikuwa speed ndogo tu akapushiwa na Suzuki aliyekuwa anaendesha mfanyakazi wa tigo ikamgusa ubavuni na kupelekea gari kubilingika mara mbili.Tbway anatufanya sisi watoto wadogo,gari kwenye speed ndogo uguswe tena na suzuki swift ubilingike mara mbili?

Dogo Tbway360 hiyo umegewa kama funzo,hiyo ni rasharasha tu,punguza sifa barabarani,kwa mtu anayefahamu gari hawezi kufanya ujinga wa kukimbiza gari kwa mispeed ya hovyo hovyo tu,next time hutopata hata muda wa kwenda TIGO HQ kuwatukana SGA....Haya sasa kama ulikuwa na bima kubwa fuatilia michoro ya ajali uende bima kama ulikuwa na 3rd party ugulia maumivu ya Legacy.

Ndinga Baada ya Kula Mzinga.
View attachment 710688
Gari yake kabla ya ajali.
View attachment 710689

VIDEO CLIP TBWAY360 ALIPOVAMIA TIGO HQ NA KUANZA KUWATUKANA SGA SECURITIES KWA TUHUMA ZA KUMFICHA MFANYAKAZI WA TIGO ALIYEIGONGA GARI YAKE.
Daaah maisha yanabadilika
Nakumbuka dogo nilikuwa namcheka Sana'a coz alikuwa mshamba afu mpenda sifaaa
Nilipoteza naye mawasiliano kumbe now bado anaendelea na mambo yake???
Daaah dogo ana ulimbukeni huyo
 
[emoji3][emoji3] tbway ndio zake..kuna washkaji zangu nlimaliza nao chuo nae ni washkaji zake sana tu..wanajiita TeamTezza..wanafujo vibaya mno..na mmoja kati yao alipataga bonge la ajari kwa sifa hzohzo tulijua atakufa ..ila bado wanaendelea na michezo yao
Umemaliza chuo wapi wewe huwezi hata kuandika ajali = ajari?
 
Nilipewa na mzee hilux double cabin [HASHTAG]#ACE[/HASHTAG] kwenye vioo bado kuna # TZJ. Nilipewa tu maana yeye alinunua gari mpya... Kwanza Kabisa Gia number moja imekufa inaondoka na mbili. Kutoka gia number 4 kwenda 5 kuna wakati haikubali. Nikiipack huwa naiweka kwenye kamlima kidogo ili nikitoka niserereke kidogo niweke gia ndio niwashe ndinga.

Nimeliongezea mbwembwe fulani saivi nikama lamborgin mlio wake. Nikipita lazima wanikubali maana nina sifa balaa .aibu inanipataga ninapotaka kuondoka na mbili gari inakuwa kama inataka kupaa hiv.. Wahuni utaskiaaaaa weweeeeeee.... Miluzi kwa wingi.....

Pole tbway tuko pamoja mdau
 
Kweli wanapenda kamera too much yaani nahisi alijipiga mpaka selfie kwenye hiyo ajali [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hayo maelezo na hiyo clip ambayo anatukana watu maeneo yao ya kazi inaonesha fika ni mtu wa aina gani. Asipojifunza Mungu ampende zaidi tu next time badala ya kuwaondoa wapendwa wa wengine na kuwapa vilema vya maisha kwa ujinga wake
 
Kwan ww anakuhusu nin kila mtu na starehe zake....mtu akulishi, akusomeshi, akusaidii Kwa chochote bado unamashauri achana na upuuzi km hao...cha muhimu fata yako
Tuweke Kumbukumbu Sawa ,Usije Kuedit hapo baadae.
 
Na mmm nanunua Subaru ***** [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji16] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Wabongo walivyo na roho mbaya ukiwapiga overtake wapo kwenye daladala ya mbagala wamebanana wewe upo na ka subari kanapiga kelele mixer mziki mnene unakita huwa wanatamani hata ulipuke ***** [emoji23] [emoji23] Acheni Roho kubwa kuna watu wanatoa ushauri mzuri tu unaona hawana roho kubwa, ila wengi wenu umu mnamchukia Dogo , najua asilimia 90% humu hata starlet ya 1990 hamnaaa mnacomment kwa vitecno vya laki vya promotion [emoji23] [emoji23] [emoji23] mnahisi sijui ndo dogo atajisikia vibaya? Unaweza kuta dogo hata Jf hana time nayo yuko busy na mitandao ya vijana (insta, snapchat,Fb
 
Mnatoa mapovu yenu JF humu mnadhani anawasikia? Mfateni insta mzamieni dm mtoe mapovu yenu [emoji23] [emoji23] huu mnaoleta humu ni umbea! Na hii tabia wabongo tunaipenda saana yani ukipita mbele ya kikundi cha watu lazima wakudiscuss tena kwa mabaya yako hawatakusifia tena unakuta washkaji zako [emoji23] [emoji23] [emoji23] Kukimbiza gari hovyo hiyo sawa sio poa ila kusema Dogo anamiliki kigari cha 2000, dogo hana mafanikio yoyote cjui, kapanga sinza meeda, [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hv bongo hii wangapi wanamiliki vyombo vya moto atleast piki piki? Hata 10% ya wananchi wote haifiki! Sasa dogo anamiliki 15M worth Car unasema sio mafanikio? Dogo kapanga sinza unasema sio mafanikio? Dogo ana ajira EATV na hajafikisha 27 yrs unasema sio mafanikio? [emoji23] [emoji23] labda mm sijui aisee mafanikio ni yapoje by the way? Kumiliki private jet au ? Hizo chuki hazijengi mshaurini ila msimponde dogo
 
Back
Top Bottom