pureView Zeiss
Kaka,
Unachosema ni kweli. Binafsi nimekua mtu wa kuendesha usiku mara kwa mara.
Na nimeenda mikoa mingi tu.
Ila changamoto kubwa ya usiku ni hawa watu wa malori na pia mambo ya uharifu zaidi sana iwapo utapata dharura.
Watu wa malory asilimia kubwa wengi wao hua hawazingatii sana sheria nyakati hizo za usiku.
Wamesha sababisha ajali nyingi mno barabarani (baadhi yao)
Kuhusiana na suala la mabus, hizo speed unazosema kaka ni speed zipi?
Mbona jamaa wanatembea vizuri tu, zaidi sana magari yote ya abiria sasa hivi yanaving'amuzi.
Sina hakika kama hakika kweli wanaenda rough hivyo.
Usiku ni raha, lakini ni hatari kubwa sana.