Ushauri wa namna ya kutatua changamoto ya kidini kabla ya ndoa

Ushauri wa namna ya kutatua changamoto ya kidini kabla ya ndoa

Majighu2015

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
2,937
Reaction score
3,959
Wakuu nina mchumba wa kiislamu ambae tumeshibana sana na nataka nimuoe lakini imetokea changamoto kwa baba yake anataka nibadili dini na amekomaa kweli kweli.

Baba yake ni mtu wa dini na ni kiongozi kwenye BAKWATA. Binti hana maamuzi sana kwenye swala hilo anamsikiliza mshua wake.

Binti tulishakubaliana tufunge ndoa ya kiserikali (bomani) ili kuondoa huo mkanganyilo wa dini lakini mzee wake hataki.

Nahitaji ushauri wenu wa namna yakutatua hii changamoto.
 
Hicho kitu Ni kidogo sana,Mm enz zangu way back 2013 , nilimpata bint wa kipemba,It was same story like you.mzee wake alikomaa nibadili dini tena nilipoenda kumchumbia alimtaarisha na shekh wa wilaya kabisa ili anislimishe,nlikataa ila bahati mbaya mchumba alikuwa na ujauzito, baada ya kushindwa kunislimisha sikurud Tena Hadi leo lakin Hadi sasa bint nipo nae na mtoto yupo class 2, hivo Kama utaweza piga mimba ukishindwa tafuta mwanamke mwingine, OVER.
 
Huyo mwanamke/binti/mchumba/pisi/mama la mama hakupendi... Haoni future na wewe pita hivi kamanda
 
Yes ni mapenzi ila inapendeza sana ukimuoa mtu wa imani yako.
 
Huu ni mtihani ambao huwezi kuushinda......dawa pekee ni kuachana na huyo binti.......vipengele vya kidini vina nguvu sana kwenye jamii zetu.......ndoa ya kiserekali ni ya kiserekali lakini kwenye macho ya kidini nyinyi ni wazinifu..........

Achana na huyo binti angali mapema ili uweze kuutibu moyo wako na upate wa kufanana nae......
 
Dini ni imani ya mtu binafsi na Mungu wake. Tandika mimba huyo mwanamke maisha yaendelee.

Labda nikuulize swali, watoto mtakaobarikiwa kwa mtazamo wako watakuwa dini gani ukiwa baba wa familia?

Mmeshikilia dini ya uislamu / ukristo ova ni ya kwenu kumbe ni mapokeo tu toka kwa waarabu na wazungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nina mchumba wa kiislamu ambae tumeshibana sana na nataka nimuoe lakini imetokea changamoto kwa baba yake anataka nibadili dini na amekomaa kweli kweli.

Baba yake ni mtu wa dini na ni kiongozi kwenye BAKWATA. Binti hana maamuzi sana kwenye swala hilo anamsikiliza mshua wake.

Binti tulishakubaliana tufunge ndoa ya kiserikali (bomani) ili kuondoa huo mkanganyilo wa dini lakini mzee wake hataki.

Nahitaji ushauri wenu wa namna yakutatua hii changamoto.
Uongo mtupu.
 
Katika mahusiano imara mwanamke akiwa na mwanaume anayejitambua hatakiwi kusikiliza sauti nyingine yoyote nje ya mwanaume wake. Kinyume chake ina maananisha mwanamke hajajicommit.

Ni sawa na mwanaume awe na mpenzi wake halafu anasikiliza maelekezo toka kwa mama yake hapo hakutakuwa na mahusiano serious.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom