Ushauri wa namna ya kutatua changamoto ya kidini kabla ya ndoa

Nakazia. Kwa msimamo wake huyo mwanamke hamfai mleta uzi.
 
Ninyi ni watu wazima, chapchap ndoa ya serikali, wazazi wataelewa baadae.
 
Kwenye macho ya Mungu?
 
Kuna mmoja alikubali akaslimu ndoa,Watoto watatu now wanaishi kila mtu na dini yake mwanaume anamwambia mke nilibadili gelesha tu hili nikupate[emoji16],
 
UDINI TATIZO SANA MNGEOANAKISERIKALI ISINGEKUWA SHIDA SHIDA NISHASHUHUDIA FAMILIA ZA IVYO NA WAKAISHI VIZURI WATU WANAPENDANA TU TUSIWEKE UDINI MBELE ZAIDI
 
Hii situation ni Normal sana. Hivi navyoandika miezi miwili nyuma nilitokea kumpata na kumpenda binti wa kiislam huko zenji.

Mimi upande wangu sina shida na Dini. Ni Mkristu niliye safi na kuelewa Ukristu vyema hivyo kuoa binti wa kiislam kwangu isingekuwa shida sababu Uislam umetokea kwa ISHMAIL mtoto wa Abraham kutoka tumbo la kijakazi wake aliyepewa na Sarah mkewe ambaye hakupata mtoto hadi alipofikisha miaka 90+. Hivyo kwa Imani yangu dhabiti ya Ukristo kama Dini Sahihi, kabla ya kurudi kwa Yesu Kristu.


Changamoto ikaa pale manzi hataki mwanaume wa Kikristu sababu ameshakuwa na wanaume wawili wa kikristu na mahusiano hayakwenda vizuri na katika maisha yake ame date mwanaume mmoja tu wa Kiislam.

Hivyo mwanaume baada ya kusoundisha vya kutosha nikaona hapa siwezi kubadili mtazamo wa huyu binti nikaamua kuchapa lapa na kukamata njia mwelekeo kutafuta mwingine wa kutulia nae.

Kijana kama hapo utashindwa kuweka mimba. Nakushauri tembea na beat kutafuta mwingine.
 
Unasimulia ujinga unajiona mjanjaaa
 
Wewe ni moja ya wanaume wajinga duniani na hata hiyo ndoa hutaiweza
 
Umeshaonesha udhaifu.

Unaolewa wewe.

Kama ameshindwa kuiteka Imani yake tafsiri yake hata moyo wake ameshindwa.
Mwanamke akikupenda anaweza fanya lolote Kwa ajili ya Mpenzi wake.

Anachojaribu Kueleza jamaa hapa ni kuwa Huyo Mchumba Ake hampendi.
Ingekuwa ni Mimi napita kushoto.
Wala muda WA kumpiga mimba mtu ambaye hakupendi ni kupoteza muda.
 
Huyu binti ana upendo wa dhati kabisa, ishu ni hapo tu kwa mshua wake.
 
UDINI TATIZO SANA MNGEOANAKISERIKALI ISINGEKUWA SHIDA SHIDA NISHASHUHUDIA FAMILIA ZA IVYO NA WAKAISHI VIZURI WATU WANAPENDANA TU TUSIWEKE UDINI MBELE ZAIDI

Waislamu ndio shida.. wanawake wao hawataki waolewe na wakristo.. huku wao wenyewe hawawezi kuwatunza hao wanawake zao
 
Badili dini,oa,mzalishe halafu rudi kwenye dini yako pamoja naye.

Uzuri uislamu hauna mambo mengi,unasilimishwa na kuoa papo kwa papo bila hata mafundisho.
Hapo ni swala la imani mkuu, siwezi kubadili dini sababu ya ndoa. Solution ni kiwa neutral kwa maana ya kufunga ndoa ya kiserikali then maisha yaendelee. Tutabariki mbele ya safari
 
Ushauri wa humu wengi wanapotosha.

Palipo na upendo Kuna maelewano mkuu. Usikubali kumpoteza huyo mama watoto

Ndoa inaongozwa na mambo makuu mawili
1. Upendo
2. Sheria

Unapounda familia/serikali lazima kuwe na SHERIA ambazo hufuata baada ya Upendo.

Sheria za familia lazima ziwe na kitabu cha Muongozo, ambayo ndio Katiba.
Anayeongoza familia/Baba ndiye hutoa sheria ili kudhibiti Mabadiliko yoyote ya kitabia, kihisia na kiakili yatakayotokea ndani ya familia.

Kama Mwanamke amekataa tafsiri yake hataki kuongozwa na Mshikaji hiyo ndio maana. Yaani huyo Manzi yey ndiye anataka kuongoza hiyo serikali.
 
Unasimulia ujinga unajiona mjanjaaa
Acha ujuaji wew,upi ujinga wangu?au ulitaka niache dini yangu kwa ajil ya mwanamke!?huwa mnapenda sana watu wafuate dini yenu,ndio Tena najisifu nimemuwin mpemba kabadili yeye mwenyewe na kakil ameenda sehem sahihi.
 
Mkuu tulishakubaliana kuwa watoto watakuwa upande wa imani yangu. Hilo halina ubishi, changamoto ni hapo kwa mshua wake tu, tukivuka hapo tumetoboa.

Watoto ni wamama ndugu YANGU.
Malezi yanatoka Kwa Mama.

Sasa utaoaje mwanamke ambaye hatawafundisha watoto wako kile unachotaka awafundishe.
Anyway kila mtu ananamna yake ya kuunda Familia.
Ila weka akilini watoto wadogo hujifunza tabia za Mama Kwa urahisi zaidi kutokana na ukaribu wao na Mama Yao.

Ushauri, Kwanza hukupaswa kujadiliana Naye mambo ya Dini Bali ungemfundisha indirect way mpaka auone Ukristo ni mzuri Kwa matendo zaidi kuliko maneno.
Unachotakiwa kukifanya ni kumbadilisha huyo Shemeji yetu awe vile utakavyo ndipo umuoe.

Vinginevyo unajipa kazi huko mbeleni.
Zingatia, tofauti za Kidini ni moja ya sababu za kisheria za kuvunja Ndoa
 
Wala sio kitu cha kujisifia hiki
 
Mkuu tulishakubaliana kuwa watoto watakuwa upande wa imani yangu. Hilo halina ubishi, changamoto ni hapo kwa mshua wake tu, tukivuka hapo tumetoboa.
Mkuu tafuta mwana mke mwingine huyo amesha kushinda.

Siku zote wazazi wa mchumba wako wakikukataa usilazimishe maana undani wa familia yao huijui ukirazimisha unaweza kufungua mlango wa matatizo makubwa katika maisha yako.

Wanawake wapo wengi sana wanahitaji kuolewa tena wa dini yako.

Na kusisitiza achana na huyo binti ,hao wanao kumshauri sijui umpe mimba sijui umtoroshe wana kupotosha maana hujui huyo mzee ni jinsi gani anampenda binti yake anaweza kukufanyia kitu kibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…