Ushauri wangu kwa ACT Wazalendo na Maalim Seif

Mwisho wa siku dunia haiwezi kusimama kisa maamuzi ya Seif.

Alisusa 2015,nini kimebadilika?

Hizo nafasi mbili tayari zina wateule kasubiriwa ajichetue tu watu waapishwe.
Ccm haiwezi kutowa makamunwa kwanza wa Rais, hizo nafasi za uwaziri wampe Hamad Rashid ndio thamani yake.
 
Maalim Seif yupo kwenye position nzuri zaidi ya kujua faida na hasara za kujoin/kutojoin SUK. Alikuwa ndani 2010 - 2015 then akakaa nje yeye na wanaCUF wenzake wote kipindi cha 2015 -2020.

Huyu Mzee bila shaka atafanya uamuzi sahihi kwake na chama chake kuingia hii ngwe ya 2020 - 2025 kwa sababu anajua pro/cons za maamuzi ya aina yoyote.
 
We jamaa wewe si ukisema Lissu asiposhinda Urais utakuwa tayari kufunuliwa malinda.
 
Hizi jumuia a kimataifa tangu ziumbwe zimefanya nini kuisaidia dunia ?
Halaiki ya watu wanauliwa leo katika nchi nyingi duniani na jumuia za kimataifa zipo zinaona,watu wanaishi maisha ya kimasikini na jumuia za kimataifa zinaona.
Jumuia za kimataifa ni uchafu gani unaousema unauwezo wa kuja kukusaidia wewe na watu wako,wangekuwa wanaweza hayo ambayo wewe unayaona yanafanaa leo dunia ingekuwa sehemu bora kabisa,leo dunia umechafuliwa na jumuia hizo unazoziona za kimataifa zimebweteka,
Kwanza jiulize jumuia za kimataifa ni kina nani,wanafanya nini,kwa faida ya nani,wameundwa lini na wamefanikiwa vipi kama jumuia ?
Ukiweza hapo njoo tujadili hili kwa mara nyingine.
 
Tafsiri ya kusamehe kwa muktadha huu inakuwa ni ipi?
 
Umakamu wa rais huko Zanzibar umewekwa kimtego ili kuleta divide and rule katika kambi ya Upinzani ili wasiwe wamoja kwenye kuiconfront CCM na serikali yake kwenye ishu za msingi kama haki za binadamu na tume huru ya uchaguzi.
Hivi vitu tricky sana. Wapinzani huko Zanzibar wakigoma kujoin SUK sasa watatumia platform ipi stahiki na effective kuwaconfront CCM na Serikali yao kwenye issue za msingi?

Wamejifunza nini kipindi cha 2015-2020 walipokuwa nje ya ulingo?
 
Sikiliza wewe.

Maalimu alijaribu kuitisha maandamano, ila mkakimbia.

Sasa mnataka afanye nini? Inabidi akubali cheo.

Huwezi kumuachia Nyani shamba la mahindi

2015 - 2020 "NYIE NYANI" mliachiwa shamba la mahindi, mkala na mkamaliza lakini hamkushiba...

Leo unadhani hata mkiachiwa ( na ofcoz hamtaachiwa kwa mtindo ule wa kwanza) unadhani mtashibia wapi wakati hamkumwagilia shamba kukuza na kukomaza hayo mahindi ili nyani nyie mle Leo...??

There's no way. Safari hii nyani nyie, mtaachiwa shamba tupu lililokwisha kuvunwa mahindi ili mle mabua tu...!!
 
Seif siyo mjinga!

Kajitabidi kuwaamusha watu muandamane mkaishia kuandamania twitter na jf,

Kama mleta mada alijifungia chumbani huku akimtegemea kigogo kwamba eti ana kituo chake cha kujumlishia matokeo.
 
Una umri gani?

Unachokijua ni next to nothing!

Post-election violence za 2010 zilichinja watu 3000+ Ivory Coast kisa Gbagbo kung'ang'ania madaraka.

Na kwa taarifa yako mpaka sasa Gbagbo keshafutiwa mashitaka yote toka November 2019 anakula bata akisubiri rufaa yao,sasa sijui Gbagbo yupi kafungwa ICC.

Kama mambo yangekuwa rahisi hivyo basi ICC ingeshajaa wafungwa.

Mnapoteza muda wenu tu.
 
Hahaha watanishangaza kweli, walikataa hili wakiwa CUF sitaelewa wakikubali wakiwa ACT.

Kwanini walikataa hilo miaka mitano iliyopita, kwanini wakubali leo?!
 
Hivi vitu tricky sana. Wapinzani huko Zanzibar wakigoma kujoin SUK sasa watatumia platform ipi stahiki na effective kuwaconfront CCM na Serikali yao kwenye issue za msingi?

Wamejifunza nini kipindi cha 2015-2020 walipokuwa nje ya ulingo?

Ni kuiwacha nchi iende hivyo hivyo, hakuna mshahara hakuna kazi hakuna kula hapo sote tutaisoma namba pamoja na hao mapolisi na majeshi yao. Ndio jeshi na pisi watapopata akili ya kutokutumiwa au kuipindua nchi
 

Hata wakati wa ukoloni, kulikuwa na Waafrika wanasema Wazungu wasisumbuliwe maana wamewapa Waafrika wenzetu vyeo. Ni hivi, huyo maalim Seif akikubali kuingia kwa hiyo serikali ya wamwaga damu na wezi wa kura ajue ndio mwisho wetu wananchi kuwaamini.
 
Sefu alimsaliti jumbe
Sisi tuliokuwepo wakati wa Jumbe tunajua nini Jumbe alitufanyia. Kama Maalim alimsaliti Jumbe basi Jumbe alitusaliti kwa kutangazia mavamizi 1964 na kutusaliti wazanzibari wote kwa kumpelekea Nyerere chama cha ASP
 
Mnachoweza ni kushauri wengine cha kufanya ila nyinyi mkipewa majukumu kwenye hizi harakati mnatia mkia mapajani.😁.

Yale maandamano yangeiamsha zaidi hiyo jumuiya kuliko hata ilivyo sasa!

Wasiowajibika,wasifundishe wengine uwajibikaji.

Huku kwenyewe kupata hizo kura ni kwasababu wamepewa na hao hao wananchi. Kuandamana hata hao viongozi wangeandamana hakuna aliyewakataza.
 
Huku kwenyewe kupata hizo kura ni kwasababu wamepewa na hao hao wananchi. Kuandamana hata hao viongozi wangeandamana hakuna aliyewakataza.
Msiwafundishe cha kufanya sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…