Sa 7 mchana
JF-Expert Member
- Dec 30, 2018
- 5,214
- 10,276
Waliosoma VETA ndio kusema wametoboa haya maisha au vipi bhana.Bora mzazi ukamsomesha Binti yako ufundi cherehani, kisha ukampa mtaji wa milioni 3, kuliko kupoteza miaka 3chuoni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waliosoma VETA ndio kusema wametoboa haya maisha au vipi bhana.Bora mzazi ukamsomesha Binti yako ufundi cherehani, kisha ukampa mtaji wa milioni 3, kuliko kupoteza miaka 3chuoni
Wewe unasoma kwa mihemko ila husomi kuelewa intention ya mwandishi. Rudia kusoma uelewe ututolee ujinga wako. Wewe ni miongoni mwa walengwa mnaopaswa elewa hii mada ila kushupaza tu shingo, ptuuuh.Kuna seheku vyeti.vinahitajika acha uongo
Mfano unaweza panda ndege ambayo rubani hana vyeti? Au waweza kubali.kutibiwa na daktari asiye.na vyeti?
Wazee wa kukariri hamkosekani hata siku1.Big No.. elimu haijawah kushuka value yakeee.. atasoma degree na akimaliza anaweza kuwa hata fundi cherehani... First apate elimu kwanza
Kwani watu mnasomaga mkiwa mnawaza nini, umeelewa intention/goal ya mwandishi au mnasoma kumaliza? Hulala!Huna kingine cha kufanya zaidi ya kupotosha vijana wa watu? We ni mchawi siyo bure maana malengo ya uchawi ni kuharibu, kutesa na kuua. Marekani na Ulaya yote bado watoto wao wanasoma, nchi changa kabisa km Tanzania unasema elimu ya chuo kikuu haina maana? Acha kujifanya mjuaji wakati hakuna unalojua.
Comment ya kizembe, changamsha ubongo huo siyo unacomment kama unakmblia kula.Ni kweli hutolala njaa ila mafanikio utayasikia tu
Kuna watu wanasoma combination ya Physics, mathematics na Computer science form 6 pale, mi nawashauri Hawa waliosoma hii kombi, miezi hii mitatu minne wajibrush YouTube kwa content za Computer science kiundani then, afanye kazi Upwork na freelancer.Ushauri wangu kwa vijana wa form 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya chuo kikuu.
Tanzania ya sasa haihitaji Degree, zimeshakuwa nyingi sana mtaani mpaka copy za vyeti zinafungiwa vitumbua. Yaani degree ni luxury sio hitaji muhimu.
Tanzania ama dunia ya sasa inahitaji stadi na ujuzi, ambao mfumo wa elimu yetu haujauweka kupatikana chuo kikuu. Yaani huwezi kwenda chuo kikuu ukapata degree ya kupaka rangi kwa mfano. Na kwa kiasi kikubwa ujuzi huu unapatikana VETA. Watu wengi huwa wanadharau kwa kuchukulia kama ni njia ya waliofeli shule.
Hata hivyo kutokana na maisha yanavyoenda, elimu ya chuo kikuu ni kipimo cha daraja la elimu tu kama ilivyo darasa la saba, form 4 na form 6 na unahitajika kuwa na kitu kingine nje ya hivyo ili uweze kufanya kitu. Hasa ikiwa umetoka moja kwa moja Form 6, ndo una hali mbaya zaidi.
Lakini kama utaamua kujitengea miaka miwili au mmoja kabla ya kwenda kujiunga na hiyo elimu ya ndoto yako. Ukaenda VETA na kusomea ujuzi tofautitofauti kama udereva, umeme wa magari, umeme wa majumbani, ujenzi na ufundi wa vitu vya aluminium nk.
Basi utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa kimaisha popote ulipo na hutolala njaa kwa kukosa ajira kwani utakuwa na vyeti zaidi ya vitano vya ujuzi vitakavyokuwezesha kupenya sehemu nyingi sana kuliko namna ambavyo cheti chako kimoja cha degree kinavyoweza. Na kwa ujuzi huo utaweza kujipatia pesa za kujisomesha hiyo degree muda wowote utakaotaka. Ni vigumu kulala njaa ukiwa na elimu ya VETA, ila uwe na uhakika kuwa utalala njaa ukiwa na cheti cha degree kabla hujapata ajira. Kitu ambacho ni kitendawili.
Ukweli ni kwamba, kama una uhakika wa ajira yaani kuna mahala umeandaliwa, au kuna mtu wako yuko ofisi fulani na atakuwepo mpaka muda utakapomaliza kusoma hiyo degree, basi kasome. Kama huna uhakika basi nenda kwanza VETA. Wengi wanaopata ajira huwekwa na watu wao, au kuhonga mishahara yao mmoja au miwili ya awali ili kuajiriwa.
Hata utakapomaliza maisha ya mtaani yatakulazimisha na yatakudai ujuzi au stadi fulani utakaopaswa kuwa nao nje ya hiyo degree yako ili ujiingizie kipato. Na ndicho ninachokisema hapa. Kwa bahati mbaya hutakuwa nao, na hutakuwa na uwezo wa kusoma VETA tena kwani hela ambayo ungeweza kuitumia kama mtaji wako wa kujipatia ujuzi huo utakuwa umeimaliza kwenye degree.
Elimu ya VETA ina uwezo wa kukusomesha degree, ila elimu ya degree ni vigumu mno kukusomesha kama bado hujapata ajira. Ni rahisi kujiajiri ukiwa na elimu ya VETA ila ni ngumu sana ukiwa na degree. Kwani utahitaji mtaji, na huo mtaji ndio utakuwa umeutumia kusomea degree. Kwa hivyo utakuwa mtaji huna na ujuzi huna, na itakuwia vigumu sana kujitafuta. Hapa wadada wengi waliohitimu ndio hudanga kusiko kawaida na wa kiume kupinduka na bodaboda kukimbilia abiria wapate hela nyingi ndani ya muda mfupi ili waache kazi hiyo.
Na uzuri wa kuya face maisha kwa ujuzi na stadi utakazopata VETA, ni kwamba utakuwa na uzoefu na namna ya kukabiliana na maisha ya mtaani na kikubwa zaidi utatambua wazi ni aina gani ya degree inayohitajika mtaani kwani vijana wengi huchagua degree kwa kutazama uzuri wake wa kutamkwa mdomoni. Ukitoka na cheti chako cha chuo kikuu hapa Tanzania ukaenda nchi za ughaibuni, kuna uwezekano mkubwa ukahitajika kusoma tena au kujiboresha kwa elimu watakayokupa wenyewe.
Yaani kwa kifupi, elimu yetu haiaminiki. Na ndio maana watoto wa viongozi na watu wenye pesa husoma nje ili kuepuka hili. Lakini ukitoka na Vyeti vyako vya VETA hata vikachanwachanwa, ujuzi wako utaongea. Na popote pale utapata nafasi, kisha utajisomesha hiyo degree.
Nimeandika kwa uzoefu wangu, na degree yangu niliyonayo ikiwa ni mwaka wa tatu tangu nihitimu na sijui hata interview inafananaje. 😀. Kabla sijaenda chuo niliambiwa karibia kama hivi nilivyoandika hapa, sikutilia maanani sana, na nikasoma degree kwa cash zaidi ya milioni 11, yaani ada pamoja na gharama za kuendesha maisha ya chuo baada ya kukosa mkopo. Mzazi asingenipa pesa hizi nikajiajiri, na sikuwa na lolote kuhusu kujiajiri. Mimi nimejitahidi hapa kuyanyoosha zaidi kwa vijana wenzangu.
Jitathmini kisha utajijibu. Ukiparamia degree, utakapomaliza hata hela za vocha utagongea kwa washkaji zako walioenda VETA na hao ndio watakusave vimeo vyako vyote. Hutaamini. Sikukatishi tamaa, ndio ukweli.
Kwa kifupi, degree imekuwa sio kitu cha kuanza nacho mtaani yaani ni lazima uwe na kitu kingine kwanza kisha ndio uongezee na elimu ya degree. Wanaonufaika moja kwa moja na elimu hiyo ni wale ambao tayari wako kazini, wanaenda vyuo kuongeza elimu kisha kurudi kazini kupandishwa vyeo. Sio mtoto wa form 6 au diploma.
Lakini kama umebahatika kupata mkopo, nenda kasome ila hakikisha unajinyima sana na hela zako una save ili utakapomaliza upate ada ya kwenda VETA kujiongezea kitu cha ziada au kufungua biashara yako binafsi lakini sio ajira. Na hata kama utatafuta ajira utahitaji nauli za kunguka mjini, hata ukipata sehemu ya kujitolea bado utahitaji kujigharamia kwa karibu miezi 6.
Mzazi hatokupa gharama hizo, kwani wazazi wetu wengi mkataba wao wa kukugharamia huishia siku una graduate. Baada ya hapo huanza kukutazama wewe sasa namna utakavyoweza kurudisha fadhila. Baada ya graduation hakutakiwa na pocket money wala boom la serikali.
Semester 6 au 8 ni muda mchache sana, lakini una mambo mengi na graduation halisi ni kurudi mtaani si ile ya kuvaa joho.
Mkuu mtaa wapo washua wengi walioanza shughuli za ufundi tangia hata bado hatujazaliwa. Ila mpaka anagonga 60 bado awajajipata.Comment ya kizembe, changamsha ubongo huo siyo unacomment kama unakmblia kula.
Hakuna ambacho hakina umuhimu Mimi nawachora tu hapa usiseme eti degree haina umuhimu inategemea umesoma degree ya nini, kasomee degree ya uMC upige Pesa km Gara B finishCha msingi ni kusoma kwa malengo. Veta, vyuo vya kati na degree vyote vina umuhimu wake. Tunachokosa ni ushauri unaotokana na uchambuzi wa soko la ajira.
Nadhani hapa umezingatia zaidi upande wa familia zinazojiweza.waachwe vijana waende vyuo vijuu.... then wakitoka huko... waJoin VETA...
Hatari sanaWenzenu wana retain wasomi wa degree katika nchi zao nyie mnasema haina umuhimu...
Sasa hio plumber hata Mimi saidia fundi si naifanya mboni kazi simple tu tatizo vyetiJuzi kati niliona UDSM wanataka technician plumber aliyesomea VETA akiwa na cheti cha form 4 ni sawa tu. Mshahara 550,000
Madogo wana magamba ya degree hawana ujuzi kazi ikawapita
Kuna taaluma (Professional) hii imekaa kibosi zaidi na kwa sasa kumejaa (wanahitajika watu wachace sana) na nafasi kubwa inachukuliwa na teknolojia!!!!!!!! ujuzi (Skills)hii imekaa kimikono na viungo zaidi huku mpaka unakufa hakutakuja kujaa mpaka kiama!!!!!!!!!!Ushauri wangu kwa vijana wa form 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya chuo kikuu.
Tanzania ya sasa haihitaji Degree, zimeshakuwa nyingi sana mtaani mpaka copy za vyeti zinafungiwa vitumbua. Yaani degree ni luxury sio hitaji muhimu.
Tanzania ama dunia ya sasa inahitaji stadi na ujuzi, ambao mfumo wa elimu yetu haujauweka kupatikana chuo kikuu. Yaani huwezi kwenda chuo kikuu ukapata degree ya kupaka rangi kwa mfano. Na kwa kiasi kikubwa ujuzi huu unapatikana VETA. Watu wengi huwa wanadharau kwa kuchukulia kama ni njia ya waliofeli shule.
Hata hivyo kutokana na maisha yanavyoenda, elimu ya chuo kikuu ni kipimo cha daraja la elimu tu kama ilivyo darasa la saba, form 4 na form 6 na unahitajika kuwa na kitu kingine nje ya hivyo ili uweze kufanya kitu. Hasa ikiwa umetoka moja kwa moja Form 6, ndo una hali mbaya zaidi.
Lakini kama utaamua kujitengea miaka miwili au mmoja kabla ya kwenda kujiunga na hiyo elimu ya ndoto yako. Ukaenda VETA na kusomea ujuzi tofautitofauti kama udereva, umeme wa magari, umeme wa majumbani, ujenzi na ufundi wa vitu vya aluminium nk.
Basi utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa kimaisha popote ulipo na hutolala njaa kwa kukosa ajira kwani utakuwa na vyeti zaidi ya vitano vya ujuzi vitakavyokuwezesha kupenya sehemu nyingi sana kuliko namna ambavyo cheti chako kimoja cha degree kinavyoweza. Na kwa ujuzi huo utaweza kujipatia pesa za kujisomesha hiyo degree muda wowote utakaotaka. Ni vigumu kulala njaa ukiwa na elimu ya VETA, ila uwe na uhakika kuwa utalala njaa ukiwa na cheti cha degree kabla hujapata ajira. Kitu ambacho ni kitendawili.
Ukweli ni kwamba, kama una uhakika wa ajira yaani kuna mahala umeandaliwa, au kuna mtu wako yuko ofisi fulani na atakuwepo mpaka muda utakapomaliza kusoma hiyo degree, basi kasome. Kama huna uhakika basi nenda kwanza VETA. Wengi wanaopata ajira huwekwa na watu wao, au kuhonga mishahara yao mmoja au miwili ya awali ili kuajiriwa.
Hata utakapomaliza maisha ya mtaani yatakulazimisha na yatakudai ujuzi au stadi fulani utakaopaswa kuwa nao nje ya hiyo degree yako ili ujiingizie kipato. Na ndicho ninachokisema hapa. Kwa bahati mbaya hutakuwa nao, na hutakuwa na uwezo wa kusoma VETA tena kwani hela ambayo ungeweza kuitumia kama mtaji wako wa kujipatia ujuzi huo utakuwa umeimaliza kwenye degree.
Elimu ya VETA ina uwezo wa kukusomesha degree, ila elimu ya degree ni vigumu mno kukusomesha kama bado hujapata ajira. Ni rahisi kujiajiri ukiwa na elimu ya VETA ila ni ngumu sana ukiwa na degree. Kwani utahitaji mtaji, na huo mtaji ndio utakuwa umeutumia kusomea degree. Kwa hivyo utakuwa mtaji huna na ujuzi huna, na itakuwia vigumu sana kujitafuta. Hapa wadada wengi waliohitimu ndio hudanga kusiko kawaida na wa kiume kupinduka na bodaboda kukimbilia abiria wapate hela nyingi ndani ya muda mfupi ili waache kazi hiyo.
Na uzuri wa kuya face maisha kwa ujuzi na stadi utakazopata VETA, ni kwamba utakuwa na uzoefu na namna ya kukabiliana na maisha ya mtaani na kikubwa zaidi utatambua wazi ni aina gani ya degree inayohitajika mtaani kwani vijana wengi huchagua degree kwa kutazama uzuri wake wa kutamkwa mdomoni. Ukitoka na cheti chako cha chuo kikuu hapa Tanzania ukaenda nchi za ughaibuni, kuna uwezekano mkubwa ukahitajika kusoma tena au kujiboresha kwa elimu watakayokupa wenyewe.
Yaani kwa kifupi, elimu yetu haiaminiki. Na ndio maana watoto wa viongozi na watu wenye pesa husoma nje ili kuepuka hili. Lakini ukitoka na Vyeti vyako vya VETA hata vikachanwachanwa, ujuzi wako utaongea. Na popote pale utapata nafasi, kisha utajisomesha hiyo degree.
Nimeandika kwa uzoefu wangu, na degree yangu niliyonayo ikiwa ni mwaka wa tatu tangu nihitimu na sijui hata interview inafananaje. 😀. Kabla sijaenda chuo niliambiwa karibia kama hivi nilivyoandika hapa, sikutilia maanani sana, na nikasoma degree kwa cash zaidi ya milioni 11, yaani ada pamoja na gharama za kuendesha maisha ya chuo baada ya kukosa mkopo. Mzazi asingenipa pesa hizi nikajiajiri, na sikuwa na lolote kuhusu kujiajiri. Mimi nimejitahidi hapa kuyanyoosha zaidi kwa vijana wenzangu.
Jitathmini kisha utajijibu. Ukiparamia degree, utakapomaliza hata hela za vocha utagongea kwa washkaji zako walioenda VETA na hao ndio watakusave vimeo vyako vyote. Hutaamini. Sikukatishi tamaa, ndio ukweli.
Kwa kifupi, degree imekuwa sio kitu cha kuanza nacho mtaani yaani ni lazima uwe na kitu kingine kwanza kisha ndio uongezee na elimu ya degree. Wanaonufaika moja kwa moja na elimu hiyo ni wale ambao tayari wako kazini, wanaenda vyuo kuongeza elimu kisha kurudi kazini kupandishwa vyeo. Sio mtoto wa form 6 au diploma.
Lakini kama umebahatika kupata mkopo, nenda kasome ila hakikisha unajinyima sana na hela zako una save ili utakapomaliza upate ada ya kwenda VETA kujiongezea kitu cha ziada au kufungua biashara yako binafsi lakini sio ajira. Na hata kama utatafuta ajira utahitaji nauli za kunguka mjini, hata ukipata sehemu ya kujitolea bado utahitaji kujigharamia kwa karibu miezi 6.
Mzazi hatokupa gharama hizo, kwani wazazi wetu wengi mkataba wao wa kukugharamia huishia siku una graduate. Baada ya hapo huanza kukutazama wewe sasa namna utakavyoweza kurudisha fadhila. Baada ya graduation hakutakiwa na pocket money wala boom la serikali.
Semester 6 au 8 ni muda mchache sana, lakini una mambo mengi na graduation halisi ni kurudi mtaani si ile ya kuvaa joho.
Plumber ni taaaluma rahisi kimtaa lakini aliyesomea sio mwenzako.Sasa hio plumber hata Mimi saidia fundi si naifanya mboni kazi simple tu tatizo vyeti
Kesho ataitwa electrical engineer hapo hapo UDSM huyo wa VETA atakaa kushoto sababu hana degree ya EE
✍️
Tanzania tunayo shida komavu ya kusoma vitu siyo ili tuelewe bali tutoe mawazo yetu kinzani tunayodhani yana point zaidi.Mkuu mtaa wapo washua wengi walioanza shughuli za ufundi tangia hata bado hatujazaliwa. Ila mpaka anagonga 60 bado awajajipata.
Slogan zao ni izo izo fundi alali njaa.
Maisha ni zaidi ya kula.
Sio mbaya ndio kashaingia kwenye system tayariKesho ataitwa electrical engineer hapo hapo UDSM huyo wa VETA
Aisee yani huo mshahara wa mwezi au week?Juzi kati niliona UDSM wanataka technician plumber aliyesomea VETA akiwa na cheti cha form 4 ni sawa tu. Mshahara 550,000
Madogo wana magamba ya degree hawana ujuzi kazi ikawapita
Nimejifunza kutoka kwa ndugu yangu aliepita VETA baada ya kumaliza akafungua duka la vifaa vya ujenzi (workshop) sana sana akawa anauza mabomba na makolokolo mengine ya kuhusu mabomba pamoja na kufanya ufundi majumbani akawa kila akipata kazi nakua msaidizi wakePlumber ni taaaluma rahisi kimtaa lakini aliyesomea sio mwenzako