Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Nimejifunza kutoka kwa ndugu yangu aliepita VETA baada ya kumaliza akafungua duka la vifaa vya ujenzi (workshop) sana sana akawa anauza mabomba na makolokolo mengine ya kuhusu mabomba pamoja na kufanya ufundi majumbani akawa kila akipata kazi nakua msaidizi wake
na ananipa maelekezo hapa fanya hivi pale fanya hivi pima hivi funga hivi hiki funga hivi hapo ndipo nilipopata ujuzi, kingine wadau wangu wa dawasco nao walikua wananipa ABC za hiki fanya hivi hiki fanya hivi vifaa hivi ndio vizuri vifaa hivi usitumie na mengine mengi, sasa mpaka hapo Mimi sio technician ambae sina cheti cha VETA

Ongeza kingine unaonaje?
Naomba niruhusu nikuulize kitu kuhusu plumbing nione kama kweli unaijua
 
Uliza chochote unachojisikia kwa lugha ya kiutendaji maana ile ni kazi ya mikono sio kazi ya mdomo
✍️
Kipimo kati ya hizo elbow 2 hapo inatakiwa iwe ngapi? Kwenye hizo bomba za ppr

Na kipimo kutoka chini hadi kwenye hizo elbow inatakiwa kuwa ngapi ikiwa tayari kuna tiles?
Screenshot_20230713-194202_Gallery.jpg
 
Distance kati ya hizo elbow 2 hapo inatakiwa iwe ngapi? Kwenye hizo bomba za ppr

Na distance kutoka chini hadi kwenye hizo elbow inatakiwa kuwa ngapi?
View attachment 2686943
Yaan Mzee hadi umeenda kudesa ndio umekuja na swali ? Wewe kwa kukadiria hapo unaona distance ipoje ? Maana ili nipime hapo inabidi niwe hapo napima vipi kwa picha ya simu ? Ndio maana nimekwambia uliza swali la kiutendaji sio theory uliza practical questions mfano nikifunga bomba nafunga likiwa kavu au natumia tape je rubber iliyopo kwenye connector naiondoa au naifanyia nini naiweka au naiondoa ? Naunganisha vipi bomba lililopasuka n so forth, uliza maswali km hayo ya kiutendaji sasa unaniambia hapo nipime kwa makadirio si ntaonekana fundi kilaza
✍️
 
Hakuna ambacho hakina umuhimu Mimi nawachora tu hapa usiseme eti degree haina umuhimu inategemea umesoma degree ya nini, kasomee degree ya uMC upige Pesa km Gara B finish
✍️

GARAB mwenyewe hana degree yeyote.

Kasoma zake kigurunyembe teachers college diploma ya education.

U Mc ni mdomo wako tu. DR CHENI nae MC mkubwa na hana degree yoyote
 
Yaan Mzee hadi umeenda kudesa ndio umekuja na swali ? Wewe kwa kukadiria hapo unaona distance ipoje ? Maana ili nipime hapo inabidi niwe hapo napima vipi kwa picha ya simu ? Ndio maana nimekwambia uliza swali la kiutendaji sio theory uliza practical questions mfano nikifunga bomba nafunga likiwa kavu au natumia tape je rubber iliyopo kwenye connector naiondoa au naifanyia nini naiweka au naiondoa ? Naunganisha vipi bomba lililopasuka n so forth, uliza maswali km hayo ya kiutendaji sasa unaniambia hapo nipime kwa makadirio si ntaonekana fundi kilaza
✍️
Vipimo kati ya elbow moja na nyingine hapo ni universal havibadiliki.

Hiyo ni shower hapo kuna elbow ya maji moto naya maji baridi. Kikawaida kutoka centre ya elbow moja hadi nyingine ni 15 cm kokote uendapo duniani haibadiliki
 
Kiongozi umenena ILA bado Elimu ya CHUO KIKUU ina UMUHIMU tena mkubwa kwa kuwa itampa maarifa na upeo mkubwa zaidi,hivyo acha vijana waende vyuo vikuu ILA wakimaliza waende vyuo mbali mbali kuongeza uzito zaidi..wale watakao weza kwenda VETA sawa,wale wa Law school sawa,wale wa NBAA/ACCA sawa wale wa CISCO sawa..ili mradi waongeze ujuzi zaidi..
 
Watu kukosa ajira sio kigezo cha elimu kutokuwa na manufaa.Elimu ya Tanzania kutokuwa na manufaa kwa kutoa ajira kunatokana na Sera mbovu za Serikali na CCM yake.

Everything start with theories,intuitions bila hizo hata hiyo elimu ya VETA haina maana,kwa kuwa VETA ni application ya hizo theories na mawazo.
 
Ushauri wangu kwa vijana wa form 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya chuo kikuu.

Tanzania ya sasa haihitaji Degree, zimeshakuwa nyingi sana mtaani mpaka copy za vyeti zinafungiwa vitumbua. Yaani degree ni luxury sio hitaji muhimu.

Tanzania ama dunia ya sasa inahitaji stadi na ujuzi, ambao mfumo wa elimu yetu haujauweka kupatikana chuo kikuu. Yaani huwezi kwenda chuo kikuu ukapata degree ya kupaka rangi kwa mfano. Na kwa kiasi kikubwa ujuzi huu unapatikana VETA. Watu wengi huwa wanadharau kwa kuchukulia kama ni njia ya waliofeli shule.

Hata hivyo kutokana na maisha yanavyoenda, elimu ya chuo kikuu ni kipimo cha daraja la elimu tu kama ilivyo darasa la saba, form 4 na form 6 na unahitajika kuwa na kitu kingine nje ya hivyo ili uweze kufanya kitu. Hasa ikiwa umetoka moja kwa moja Form 6, ndo una hali mbaya zaidi.

Lakini kama utaamua kujitengea miaka miwili au mmoja kabla ya kwenda kujiunga na hiyo elimu ya ndoto yako. Ukaenda VETA na kusomea ujuzi tofautitofauti kama udereva, umeme wa magari, umeme wa majumbani, ujenzi na ufundi wa vitu vya aluminium nk.

Basi utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa kimaisha popote ulipo na hutolala njaa kwa kukosa ajira kwani utakuwa na vyeti zaidi ya vitano vya ujuzi vitakavyokuwezesha kupenya sehemu nyingi sana kuliko namna ambavyo cheti chako kimoja cha degree kinavyoweza. Na kwa ujuzi huo utaweza kujipatia pesa za kujisomesha hiyo degree muda wowote utakaotaka. Ni vigumu kulala njaa ukiwa na elimu ya VETA, ila uwe na uhakika kuwa utalala njaa ukiwa na cheti cha degree kabla hujapata ajira. Kitu ambacho ni kitendawili.

Ukweli ni kwamba, kama una uhakika wa ajira yaani kuna mahala umeandaliwa, au kuna mtu wako yuko ofisi fulani na atakuwepo mpaka muda utakapomaliza kusoma hiyo degree, basi kasome. Kama huna uhakika basi nenda kwanza VETA. Wengi wanaopata ajira huwekwa na watu wao, au kuhonga mishahara yao mmoja au miwili ya awali ili kuajiriwa.

Hata utakapomaliza maisha ya mtaani yatakulazimisha na yatakudai ujuzi au stadi fulani utakaopaswa kuwa nao nje ya hiyo degree yako ili ujiingizie kipato. Na ndicho ninachokisema hapa. Kwa bahati mbaya hutakuwa nao, na hutakuwa na uwezo wa kusoma VETA tena kwani hela ambayo ungeweza kuitumia kama mtaji wako wa kujipatia ujuzi huo utakuwa umeimaliza kwenye degree.

Elimu ya VETA ina uwezo wa kukusomesha degree, ila elimu ya degree ni vigumu mno kukusomesha kama bado hujapata ajira. Ni rahisi kujiajiri ukiwa na elimu ya VETA ila ni ngumu sana ukiwa na degree. Kwani utahitaji mtaji, na huo mtaji ndio utakuwa umeutumia kusomea degree. Kwa hivyo utakuwa mtaji huna na ujuzi huna, na itakuwia vigumu sana kujitafuta. Hapa wadada wengi waliohitimu ndio hudanga kusiko kawaida na wa kiume kupinduka na bodaboda kukimbilia abiria wapate hela nyingi ndani ya muda mfupi ili waache kazi hiyo.

Na uzuri wa kuya face maisha kwa ujuzi na stadi utakazopata VETA, ni kwamba utakuwa na uzoefu na namna ya kukabiliana na maisha ya mtaani na kikubwa zaidi utatambua wazi ni aina gani ya degree inayohitajika mtaani kwani vijana wengi huchagua degree kwa kutazama uzuri wake wa kutamkwa mdomoni. Ukitoka na cheti chako cha chuo kikuu hapa Tanzania ukaenda nchi za ughaibuni, kuna uwezekano mkubwa ukahitajika kusoma tena au kujiboresha kwa elimu watakayokupa wenyewe.

Yaani kwa kifupi, elimu yetu haiaminiki. Na ndio maana watoto wa viongozi na watu wenye pesa husoma nje ili kuepuka hili. Lakini ukitoka na Vyeti vyako vya VETA hata vikachanwachanwa, ujuzi wako utaongea. Na popote pale utapata nafasi, kisha utajisomesha hiyo degree.

Nimeandika kwa uzoefu wangu, na degree yangu niliyonayo ikiwa ni mwaka wa tatu tangu nihitimu na sijui hata interview inafananaje. 😀. Kabla sijaenda chuo niliambiwa karibia kama hivi nilivyoandika hapa, sikutilia maanani sana, na nikasoma degree kwa cash zaidi ya milioni 11, yaani ada pamoja na gharama za kuendesha maisha ya chuo baada ya kukosa mkopo. Mzazi asingenipa pesa hizi nikajiajiri, na sikuwa na lolote kuhusu kujiajiri. Mimi nimejitahidi hapa kuyanyoosha zaidi kwa vijana wenzangu.

Jitathmini kisha utajijibu. Ukiparamia degree, utakapomaliza hata hela za vocha utagongea kwa washkaji zako walioenda VETA na hao ndio watakusave vimeo vyako vyote. Hutaamini. Sikukatishi tamaa, ndio ukweli.

Kwa kifupi, degree imekuwa sio kitu cha kuanza nacho mtaani yaani ni lazima uwe na kitu kingine kwanza kisha ndio uongezee na elimu ya degree. Wanaonufaika moja kwa moja na elimu hiyo ni wale ambao tayari wako kazini, wanaenda vyuo kuongeza elimu kisha kurudi kazini kupandishwa vyeo. Sio mtoto wa form 6 au diploma.

Lakini kama umebahatika kupata mkopo, nenda kasome ila hakikisha unajinyima sana na hela zako una save ili utakapomaliza upate ada ya kwenda VETA kujiongezea kitu cha ziada au kufungua biashara yako binafsi lakini sio ajira. Na hata kama utatafuta ajira utahitaji nauli za kunguka mjini, hata ukipata sehemu ya kujitolea bado utahitaji kujigharamia kwa karibu miezi 6.

Mzazi hatokupa gharama hizo, kwani wazazi wetu wengi mkataba wao wa kukugharamia huishia siku una graduate. Baada ya hapo huanza kukutazama wewe sasa namna utakavyoweza kurudisha fadhila. Baada ya graduation hakutakiwa na pocket money wala boom la serikali.

Semester 6 au 8 ni muda mchache sana, lakini una mambo mengi na graduation halisi ni kurudi mtaani si ile ya kuvaa joho.
Walimu was diploma wapewe maua yao
 
Back
Top Bottom