Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Ushauri wangu kwa vijana wa form 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya chuo kikuu.

Tanzania ya sasa haihitaji Degree, zimeshakuwa nyingi sana mtaani mpaka copy za vyeti zinafungiwa vitumbua. Yaani degree ni luxury sio hitaji muhimu.

Tanzania ama dunia ya sasa inahitaji stadi na ujuzi, ambao mfumo wa elimu yetu haujauweka kupatikana chuo kikuu. Yaani huwezi kwenda chuo kikuu ukapata degree ya kupaka rangi kwa mfano. Na kwa kiasi kikubwa ujuzi huu unapatikana VETA. Watu wengi huwa wanadharau kwa kuchukulia kama ni njia ya waliofeli shule.

Hata hivyo kutokana na maisha yanavyoenda, elimu ya chuo kikuu ni kipimo cha daraja la elimu tu kama ilivyo darasa la saba, form 4 na form 6 na unahitajika kuwa na kitu kingine nje ya hivyo ili uweze kufanya kitu. Hasa ikiwa umetoka moja kwa moja Form 6, ndo una hali mbaya zaidi.

Lakini kama utaamua kujitengea miaka miwili au mmoja kabla ya kwenda kujiunga na hiyo elimu ya ndoto yako. Ukaenda VETA na kusomea ujuzi tofautitofauti kama udereva, umeme wa magari, umeme wa majumbani, ujenzi na ufundi wa vitu vya aluminium nk.

Basi utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa kimaisha popote ulipo na hutolala njaa kwa kukosa ajira kwani utakuwa na vyeti zaidi ya vitano vya ujuzi vitakavyokuwezesha kupenya sehemu nyingi sana kuliko namna ambavyo cheti chako kimoja cha degree kinavyoweza. Na kwa ujuzi huo utaweza kujipatia pesa za kujisomesha hiyo degree muda wowote utakaotaka. Ni vigumu kulala njaa ukiwa na elimu ya VETA, ila uwe na uhakika kuwa utalala njaa ukiwa na cheti cha degree kabla hujapata ajira. Kitu ambacho ni kitendawili.

Ukweli ni kwamba, kama una uhakika wa ajira yaani kuna mahala umeandaliwa, au kuna mtu wako yuko ofisi fulani na atakuwepo mpaka muda utakapomaliza kusoma hiyo degree, basi kasome. Kama huna uhakika basi nenda kwanza VETA. Wengi wanaopata ajira huwekwa na watu wao, au kuhonga mishahara yao mmoja au miwili ya awali ili kuajiriwa.

Hata utakapomaliza maisha ya mtaani yatakulazimisha na yatakudai ujuzi au stadi fulani utakaopaswa kuwa nao nje ya hiyo degree yako ili ujiingizie kipato. Na ndicho ninachokisema hapa. Kwa bahati mbaya hutakuwa nao, na hutakuwa na uwezo wa kusoma VETA tena kwani hela ambayo ungeweza kuitumia kama mtaji wako wa kujipatia ujuzi huo utakuwa umeimaliza kwenye degree.

Elimu ya VETA ina uwezo wa kukusomesha degree, ila elimu ya degree ni vigumu mno kukusomesha kama bado hujapata ajira. Ni rahisi kujiajiri ukiwa na elimu ya VETA ila ni ngumu sana ukiwa na degree. Kwani utahitaji mtaji, na huo mtaji ndio utakuwa umeutumia kusomea degree. Kwa hivyo utakuwa mtaji huna na ujuzi huna, na itakuwia vigumu sana kujitafuta. Hapa wadada wengi waliohitimu ndio hudanga kusiko kawaida na wa kiume kupinduka na bodaboda kukimbilia abiria wapate hela nyingi ndani ya muda mfupi ili waache kazi hiyo.

Na uzuri wa kuya face maisha kwa ujuzi na stadi utakazopata VETA, ni kwamba utakuwa na uzoefu na namna ya kukabiliana na maisha ya mtaani na kikubwa zaidi utatambua wazi ni aina gani ya degree inayohitajika mtaani kwani vijana wengi huchagua degree kwa kutazama uzuri wake wa kutamkwa mdomoni. Ukitoka na cheti chako cha chuo kikuu hapa Tanzania ukaenda nchi za ughaibuni, kuna uwezekano mkubwa ukahitajika kusoma tena au kujiboresha kwa elimu watakayokupa wenyewe.

Yaani kwa kifupi, elimu yetu haiaminiki. Na ndio maana watoto wa viongozi na watu wenye pesa husoma nje ili kuepuka hili. Lakini ukitoka na Vyeti vyako vya VETA hata vikachanwachanwa, ujuzi wako utaongea. Na popote pale utapata nafasi, kisha utajisomesha hiyo degree.

Nimeandika kwa uzoefu wangu, na degree yangu niliyonayo ikiwa ni mwaka wa tatu tangu nihitimu na sijui hata interview inafananaje. 😀. Kabla sijaenda chuo niliambiwa karibia kama hivi nilivyoandika hapa, sikutilia maanani sana, na nikasoma degree kwa cash zaidi ya milioni 11, yaani ada pamoja na gharama za kuendesha maisha ya chuo baada ya kukosa mkopo. Mzazi asingenipa pesa hizi nikajiajiri, na sikuwa na lolote kuhusu kujiajiri. Mimi nimejitahidi hapa kuyanyoosha zaidi kwa vijana wenzangu.

Jitathmini kisha utajijibu. Ukiparamia degree, utakapomaliza hata hela za vocha utagongea kwa washkaji zako walioenda VETA na hao ndio watakusave vimeo vyako vyote. Hutaamini. Sikukatishi tamaa, ndio ukweli.

Kwa kifupi, degree imekuwa sio kitu cha kuanza nacho mtaani yaani ni lazima uwe na kitu kingine kwanza kisha ndio uongezee na elimu ya degree. Wanaonufaika moja kwa moja na elimu hiyo ni wale ambao tayari wako kazini, wanaenda vyuo kuongeza elimu kisha kurudi kazini kupandishwa vyeo. Sio mtoto wa form 6 au diploma.

Lakini kama umebahatika kupata mkopo, nenda kasome ila hakikisha unajinyima sana na hela zako una save ili utakapomaliza upate ada ya kwenda VETA kujiongezea kitu cha ziada au kufungua biashara yako binafsi lakini sio ajira. Na hata kama utatafuta ajira utahitaji nauli za kunguka mjini, hata ukipata sehemu ya kujitolea bado utahitaji kujigharamia kwa karibu miezi 6.

Mzazi hatokupa gharama hizo, kwani wazazi wetu wengi mkataba wao wa kukugharamia huishia siku una graduate. Baada ya hapo huanza kukutazama wewe sasa namna utakavyoweza kurudisha fadhila. Baada ya graduation hakutakiwa na pocket money wala boom la serikali.

Semester 6 au 8 ni muda mchache sana, lakini una mambo mengi na graduation halisi ni kurudi mtaani si ile ya kuvaa joho.

Stadi za maisha na kubobea kwenye kile mtu anachoamua kuchukua. Kama kuna global certification courses go for them. The certificate will isolate you in the crowd, as an expert in the subject matter.
Mitandao, imefanya mambo mengi kuwa rahisi. Sio lazima uwe professor kuwa mbobezi wa aina fulani ya utaalamu
 
Hivi hawawezi ku incorporate hio elimu ya degree iwe na ujuzi ndani yake, mtu wa degree akimaliza aweze kujiajiri?
Hichi ndio kinachofanyika kwa wenzetu... US, UK and the like. Elimu yetu inaonekana haina maana kwasababu mitaala yetu imefeli kwenye hicho ulicho kisema.

Ilitakiwa kinachofanyika veta kifanyike na kwenye elimu ya juu pia kwa ku_incorporate mitaala ya veta kwenye elimu ya juu.
 
Kama issues ni ajira tu na kupata hela ya kula wambie waingie kwenye bodaboda maana unajifunza siku mbili ya tatu unakula vichwa road ila kama ni elimu waende chuo kikuu wakapate maarifa na wafikilie mafanikio makubwa zaidi sio kuwa fundi michudu
 
Tatizo fikra Zako zinawaza kuajiriwa tu.. focus ya elimu ya chuo ni kukujenga kifikra. Ndo maana utakuta wahindi au waarabu wanasomesha watoto wao hadi university Kwa lengo la kurudi kusimamia biashar Zao..
Tatizo Hawa wanawaza kupata hela ya kula na sio maarifa hata vijana wa kinigeria wangekuwa wanafikiri kama Hawa jamaa wasingeingia kwenye nchi za watu Sasa sijui Kila mtu akiwa fundi mchundo itakuaje
 
GARAB mwenyewe hana degree yeyote.

Kasoma zake kigurunyembe teachers college diploma ya education.

U Mc ni mdomo wako tu. DR CHENI nae MC mkubwa na hana degree yoyote
Nasikia kuna Chuo cha uMC kimefunguliwa Mwanza wanafunzi wa awamu ya kwanza yaani first intake watasoma bure na wanagharamiwa kila kitu bure, fursa kwa vijana
✍️
 
Ushauri wangu kwa vijana wa form 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya chuo kikuu.

Tanzania ya sasa haihitaji Degree, zimeshakuwa nyingi sana mtaani mpaka copy za vyeti zinafungiwa vitumbua. Yaani degree ni luxury sio hitaji muhimu.

Tanzania ama dunia ya sasa inahitaji stadi na ujuzi, ambao mfumo wa elimu yetu haujauweka kupatikana chuo kikuu. Yaani huwezi kwenda chuo kikuu ukapata degree ya kupaka rangi kwa mfano. Na kwa kiasi kikubwa ujuzi huu unapatikana VETA. Watu wengi huwa wanadharau kwa kuchukulia kama ni njia ya waliofeli shule.

Hata hivyo kutokana na maisha yanavyoenda, elimu ya chuo kikuu ni kipimo cha daraja la elimu tu kama ilivyo darasa la saba, form 4 na form 6 na unahitajika kuwa na kitu kingine nje ya hivyo ili uweze kufanya kitu. Hasa ikiwa umetoka moja kwa moja Form 6, ndo una hali mbaya zaidi.

Lakini kama utaamua kujitengea miaka miwili au mmoja kabla ya kwenda kujiunga na hiyo elimu ya ndoto yako. Ukaenda VETA na kusomea ujuzi tofautitofauti kama udereva, umeme wa magari, umeme wa majumbani, ujenzi na ufundi wa vitu vya aluminium nk.

Basi utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa kimaisha popote ulipo na hutolala njaa kwa kukosa ajira kwani utakuwa na vyeti zaidi ya vitano vya ujuzi vitakavyokuwezesha kupenya sehemu nyingi sana kuliko namna ambavyo cheti chako kimoja cha degree kinavyoweza. Na kwa ujuzi huo utaweza kujipatia pesa za kujisomesha hiyo degree muda wowote utakaotaka. Ni vigumu kulala njaa ukiwa na elimu ya VETA, ila uwe na uhakika kuwa utalala njaa ukiwa na cheti cha degree kabla hujapata ajira. Kitu ambacho ni kitendawili.

Ukweli ni kwamba, kama una uhakika wa ajira yaani kuna mahala umeandaliwa, au kuna mtu wako yuko ofisi fulani na atakuwepo mpaka muda utakapomaliza kusoma hiyo degree, basi kasome. Kama huna uhakika basi nenda kwanza VETA. Wengi wanaopata ajira huwekwa na watu wao, au kuhonga mishahara yao mmoja au miwili ya awali ili kuajiriwa.

Hata utakapomaliza maisha ya mtaani yatakulazimisha na yatakudai ujuzi au stadi fulani utakaopaswa kuwa nao nje ya hiyo degree yako ili ujiingizie kipato. Na ndicho ninachokisema hapa. Kwa bahati mbaya hutakuwa nao, na hutakuwa na uwezo wa kusoma VETA tena kwani hela ambayo ungeweza kuitumia kama mtaji wako wa kujipatia ujuzi huo utakuwa umeimaliza kwenye degree.

Elimu ya VETA ina uwezo wa kukusomesha degree, ila elimu ya degree ni vigumu mno kukusomesha kama bado hujapata ajira. Ni rahisi kujiajiri ukiwa na elimu ya VETA ila ni ngumu sana ukiwa na degree. Kwani utahitaji mtaji, na huo mtaji ndio utakuwa umeutumia kusomea degree. Kwa hivyo utakuwa mtaji huna na ujuzi huna, na itakuwia vigumu sana kujitafuta. Hapa wadada wengi waliohitimu ndio hudanga kusiko kawaida na wa kiume kupinduka na bodaboda kukimbilia abiria wapate hela nyingi ndani ya muda mfupi ili waache kazi hiyo.

Na uzuri wa kuya face maisha kwa ujuzi na stadi utakazopata VETA, ni kwamba utakuwa na uzoefu na namna ya kukabiliana na maisha ya mtaani na kikubwa zaidi utatambua wazi ni aina gani ya degree inayohitajika mtaani kwani vijana wengi huchagua degree kwa kutazama uzuri wake wa kutamkwa mdomoni. Ukitoka na cheti chako cha chuo kikuu hapa Tanzania ukaenda nchi za ughaibuni, kuna uwezekano mkubwa ukahitajika kusoma tena au kujiboresha kwa elimu watakayokupa wenyewe.

Yaani kwa kifupi, elimu yetu haiaminiki. Na ndio maana watoto wa viongozi na watu wenye pesa husoma nje ili kuepuka hili. Lakini ukitoka na Vyeti vyako vya VETA hata vikachanwachanwa, ujuzi wako utaongea. Na popote pale utapata nafasi, kisha utajisomesha hiyo degree.

Nimeandika kwa uzoefu wangu, na degree yangu niliyonayo ikiwa ni mwaka wa tatu tangu nihitimu na sijui hata interview inafananaje. 😀. Kabla sijaenda chuo niliambiwa karibia kama hivi nilivyoandika hapa, sikutilia maanani sana, na nikasoma degree kwa cash zaidi ya milioni 11, yaani ada pamoja na gharama za kuendesha maisha ya chuo baada ya kukosa mkopo. Mzazi asingenipa pesa hizi nikajiajiri, na sikuwa na lolote kuhusu kujiajiri. Mimi nimejitahidi hapa kuyanyoosha zaidi kwa vijana wenzangu.

Jitathmini kisha utajijibu. Ukiparamia degree, utakapomaliza hata hela za vocha utagongea kwa washkaji zako walioenda VETA na hao ndio watakusave vimeo vyako vyote. Hutaamini. Sikukatishi tamaa, ndio ukweli.

Kwa kifupi, degree imekuwa sio kitu cha kuanza nacho mtaani yaani ni lazima uwe na kitu kingine kwanza kisha ndio uongezee na elimu ya degree. Wanaonufaika moja kwa moja na elimu hiyo ni wale ambao tayari wako kazini, wanaenda vyuo kuongeza elimu kisha kurudi kazini kupandishwa vyeo. Sio mtoto wa form 6 au diploma.

Lakini kama umebahatika kupata mkopo, nenda kasome ila hakikisha unajinyima sana na hela zako una save ili utakapomaliza upate ada ya kwenda VETA kujiongezea kitu cha ziada au kufungua biashara yako binafsi lakini sio ajira. Na hata kama utatafuta ajira utahitaji nauli za kunguka mjini, hata ukipata sehemu ya kujitolea bado utahitaji kujigharamia kwa karibu miezi 6.

Mzazi hatokupa gharama hizo, kwani wazazi wetu wengi mkataba wao wa kukugharamia huishia siku una graduate. Baada ya hapo huanza kukutazama wewe sasa namna utakavyoweza kurudisha fadhila. Baada ya graduation hakutakiwa na pocket money wala boom la serikali.

Semester 6 au 8 ni muda mchache sana, lakini una mambo mengi na graduation halisi ni kurudi mtaani si ile ya kuvaa joho.
Asante sana boss kwa kutufumbua macho
 
Kuna watu wanasoma combination ya Physics, mathematics na Computer science form 6 pale, mi nawashauri Hawa waliosoma hii kombi, miezi hii mitatu minne wajibrush YouTube kwa content za Computer science kiundani then, afanye kazi Upwork na freelancer.

Atasahau habari za chuo kabisa.

Yaani aliyeanzisha combination ya Physics, mathematics na Computer science abarikiwe. Hii ndo ya kujiajiri Sasa.
PMC
 
Ndo imetoa 4m 6 ya kwanzaa mwaka huu
Ndio.
Nasikia wanajifunza vitu konki, as if wako chuo sema tatizo tu muda mchache 2 years kuvi-catch vyote inahitaji mtu eidha awe na IQ kubwa au asiwe na mambo mengi.

Ile naiona kama PGM iliochangamka. Ila ni combi nzuri sana hasahasa mtu akimaliza form 6 akiwa konki.
 
Pongezi kwao, wa kwenda IT watakua wana slides na madesa tyuuh
 
Hii thread ni relevant sana Kwa Mazingira tunayopita nchini. White color job kupungua na umasikini wa kipato kuongezeka.

Hivyo lazima kuwa adaptive and strategic. Hii habari ya kusoma bila muongozo maalumu unataka nini maishani umepitwa na wakati.

Mazingira yanataka creative, multitask and skillful minds. Kupata sifa hizo lazima utumie pesa Kwa umakini, hasa vijana wanaotoka familia masikini.

Mfumo wa elimu tulioruthi Kwa mkoloni Kwa Mazingira ya kitanzania haiaksi uliasia wa maisha ya mtaani. Unawaweka vijana busy kusikiliza wakufunzi na kufanya mitihani ila unakosa muda wa kujenga ujuzi tangible. Silly syllabus. Hivyo Kuna ulazima wa kubadirika.

Serikali inajivuta sana kwenye kushughulika na sera ya elimu na namna ya kuboresha ubora . Hivyo wadau na mtu mmoja mmoja lazima kuanza kuchukua hatua.

Mleta mada katuo generic blue print inayotokana na practical life . Na ushauri unaaksi Mazingira tuliyonayo nchini. Inahuzunisha wazazi na walezi masikini kutumia pesa nyingi kuandaa watoto ambao end of the day are useless.

Mbaya zaidi elimu ya chuo inawafanya vijana kupoteza maadili, na hivyo kuchochea upungufu wa thamani ya elimu ya chuo. Ni laana kubwa kuwa na vijana wanaojiita wasomi, ila hawana ujuzi na maadili. vijana wa hivyo hawafai Kwa lolote. Ni huzuni na frustration Kwa wazazi na walezi.
 
Kuna sehemu vyeti.vinahitajika acha uongo
Mfano unaweza panda ndege ambayo rubani hana vyeti? Au waweza kubali.kutibiwa na daktari asiye.na vyeti?
Mkuu hio ni asilimia ndogo Sana labda ukute mzazi au ndugu mlamba asali ya taifa akuunganishe na hio sehemu wanayotaka degree

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Pesa ndiyo elimu.

Huna pesa huna elimu.
Binafsi nashukuru sana Mungu kunipa ujasiri waakuacha chuo semister ya pili mwaka wa tatu.
 
Back
Top Bottom