Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Huu ndio ukweli.
 
Huu ndio ukweli,waliosoma veta,hasa udereva,fundi umeme,fundi bomba,seremala,kushona,wengi wapo kujiajiri.Hata madereva wengi,hawakosi kazi za ziada.Huwa wanakodishwa kuendesha magari kwenye harusi,safari za utalii,kutoa magari bandarini,na kuyasafirisha mikoani na nje ya nchi.
 


Andiko la hovyo, Vijana mkishapata degree, tafuteni extra, ila degree Maliza, kaa na karatasi lako hata kama haujapata kazi.
 
Kuna course nimesoma aisee nmekuja kufunguka baada ya kumalizia chuo, yan hauoni matangazo ya nafasi za kazi na ukiona ukisema uapply kwenye ajira portal wanakukataa aisee natamani siku zingerudi nyuma nilipomaliza form four
 
Sawa mkuu, na huko Veta wanaenda ngazi gani? Wote wana background ya science? Au unamaanisha kama umesoma science kusoma masomo ya Veta ni rahisi?
 
Watunga mitaala wangekuwa wanaelewa kama wewe tungekuwa mbali sana.
 
Kuna sehemu vyeti.vinahitajika acha uongo
Mfano unaweza panda ndege ambayo rubani hana vyeti? Au waweza kubali.kutibiwa na daktari asiye.na vyeti?
Mkuu hebu jaribu kusoma upya utaelewa zaidi. Hata veta wanatoa vyeti.
 
Kwani watu mnasomaga mkiwa mnawaza nini, umeelewa intention/goal ya mwandishi au mnasoma kumaliza? Hulala!
Ninawasiwasi Hawa ni walewale hawaelewi kabisa. Maana mwandishi ameleza Kwa lugha nyepesi lakini bado wanashindwa kuelewa.

Hapa ndipo unapoona kwanini watu wanatetea DPWorld, bila hata kelewa kilichoandikwa ndani mle kina maana Gani.
 
Mifugo pia ni science tupuu tena pure
 
Tulipaswa tuwe nazo nyingi za mfumo huo. Kuwaandaa vijana na maisha ya uhalisia siyo vitu visivyoeleweka. Public procurement. Unawezaje kumfundisha mtu asomee kununua miaka mitatu. Unasomeka kununua kweli.?
 
Juzi kati niliona UDSM wanataka technician plumber aliyesomea VETA akiwa na cheti cha form 4 ni sawa tu. Mshahara 550,000

Madogo wana magamba ya degree hawana ujuzi kazi ikawapita
Haya ndiyo maeneo ya kufocus, plumbing. Machenical, electronics, watu wawe technicians siyo vinginevyo. Maisha mtaani yanaeleweka yanahitaji watu wa aina Gani.
 
Sasa hio plumber hata Mimi saidia fundi si naifanya mboni kazi simple tu tatizo vyeti

Kesho ataitwa electrical engineer hapo hapo UDSM huyo wa VETA atakaa kushoto sababu hana degree ya EE
[emoji3578]
Ungeenda VETA ungekuwa na vyeti na ugundi. Context ya mtoa mada ielewe vizuri Mkuu.
 
Sawa mkuu, na huko Veta wanaenda ngazi gani? Wote wana background ya science? Au unamaanisha kama umesoma science kusoma masomo ya Veta ni rahisi?
Kikubwa nikujituma sana wanao enda Veta kuanzia level 1 mpaka level 2 ni kuanzia la saba na kuendelea lakini level 3 ni kuanzia form 4 na kuendelea lakini hili usome level 3 lazima ufahuru masomo yote ya level 2 na walio soma scince masomo sio changamoto sana
 
Hizo ngazi level 1 na 2 zinachukua muda gani kumaliza mkuu??? Mimi siamini kama kijana wa darasa la 7 aweze halafu mtu wa chuo kikuu asiweze, kama level 1 na 2 zinachukua mwaka mmoja kwa kila level, then ni rahisi kujumuishwa University, level 3 itakua complicated Ila mimi sijui Haya mambo kiundani….
 
umenigusa direct mimi nilivyomaliza level tu nilienda veta coz nilikuwa napenda ufundi umeme japo mzee alitaka niendelee na advance mimi nikakataa nilikomaa 2yrs namaliza tu grade 2 mtaani kila mtu alikuwa ananiita kufix ishu za umeme nikawa fundi wa mtaa nikazoeleka nikawa napiga wiring hadi majumba makubwa mwaka wa nne nikajiunga advance nikasoma nikamaliza nikapata nafasi nafasi chuo nikiwa nasoma huku napiga ishu za umeme hadi wana wanajua mimi wakshua kumbe mtaalamu yani nilikuwa na wateja kibao kwa simu sikai chuoni kizembe muda wote ni tester,prize,cutter,avometer,na makorokoro mengine ya umeme kwa bag ,cha ajabu mwaka wa 7 sasa ni mwajiriwa Gavo ila sijasahau umeme nyumba zangu nafanya wiring mwenyewe na kutengeneza vifaa vyangu vya umeme
 
Kila level ni mwaka mmoja na kwa kukazia tu mtu aliye toka veta kwenda diploma ni kama anarudia masomo tu na masomo ya kule sio mchezo kwa mtu aliye soma arts ni lazima akaze buti kweli kweli kumbuka masomo ni nane

Fani husika
Entrepreneurship
Computer
English
Technical drawing
Math
Life skills
Engineering scince

Masomo ni mengi uwezi kujumlisha kwenye kozi za chuo kikuu labda kama ita fundishwa fani tu hapo sawa
 
Ningependa kujua hio Engineering science inahusu nini mbona wameiweka kwa kila fani na hio technical drawing mkuu?

kinachohitajika kama graduate anaweza akitoka hapo kufanya fani husika, ndicho kinachohitajika,mengine mbwembwe...lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…