Huwa sipendi kuchangia mada za aina hii kabisa kwa sababu huwa naona hazina tija ila nimevutwa kusema kitu kwa sababu ya michango ya wadau. Naona kila mmoja anajitahidi kurusha makombora upande mwingine uonekane una kasoro. Upande wa wanaoshabikia bikra wamekazana kutuaminisha kuwa mwanamke bikra ndio waifu matirio haswa kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kwa mtazamo wangu jambo hili si la kweli hata kidogo...ndoa/ mapenzi ni zaidi ya ngono, kuna maisha mengine nje ya kitanda....hakuna guarantee kuwa ukioa mwanamke bikra ndio hatachepuka milele, unaweza kuoa bikra na bado ukachapiwa na ukamtoa mwanamke kimboka akatulia ndani kama sio yeye.
Kama nilivyosema awali kuna maisha nje ya tendo la ndoa...unaweza kuoa bikra ila akawa mshirikina, mchonganishi, mchafu, hapendi ndugu zako n.k sasa hiyo furaha ya ndoa na tabia kama hizo sijui furaha ya ndoa itatoka wapi? Mwanamke ni mwanamke tu bikra haina uhusiano wa moja kwa moja na furaha ya ndoa. Wengine ndio wanakuja na generalization za kipuuzi eti mwanamke hawezi kumnyima aliyemtoa bikra hata kama ameolewa....this is totally nonsense.
Tukiangalia upande wa wanaotetea ngono kabla ya ndoa pia wanajaribu kutuaminisha kuwa mwanamke kuwa bikra lazima ana kasoro, mara eti uchuro jambo ambalo naona si la kweli, kuna watu wanaolewa wakiwa na miaka 20,25,30,35 na kuendelea. Kwa mwanamke mcha Mungu na anayeamini katika kujitunza inamaana katika kipindi chote hicho atabaki bikra, sio kwamba hatongozwi ila ameamua kusimamia kile anachokiamini hata kama kuna msururu wa watu wanaotaka kumla kimasihara. Mnataka kusema watu wote wanaopoteza bikra zao kabla ya ndoa ni visu? Hapana wengine wana sura mbovu tu kama mimi hapa ila wanawapanga wanaume asubuhi mchana na jioni.
Kama nilivyosema awali kila mtu ana sababu zake za kujitunza, kuna wale walioshika dini na Mungu akawawezesha kushinda pepo la uzinzi, wapo wale wanaoamini kuwa akiolewa wakiwa bikra wataheshimiwa na waume zao kama mtoa mada ( hii nayo sio guaranteed maana unaweza ukaolewa na mtu ambae yeye virginity sio ishu hata, labda uoelewe na
Jokajeusi).
Wapo wale wanaojitunza kwaajili yao wenyewe, sio kwaajili ya mtu mwingine, wanaona ni jambo la aibu kutembea barabarani watu wanaambiana pale nimepita na mwingine anaunga na mimi pia. Wanatamani mwanaume wa kumuona uchi wake awe mmoja maana wakiwa na ma- ex kila kona wanaona kama wanatembea uchi, na wengine hawataki kuwa emotionally attached na watu tofauti na wale walioamua kuwa nao maisha yao yote.
Nimeandika mengi kiasi wengine mnajiuliza niko upande upi maana sieleweki[emoji16][emoji16][emoji16]. Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa tuheshimiane, kila mtu aheshimu maamuzi ya mwenzie maana kila mmoja wetu ana sababu za kuchagua alichochagua...haina haja ya kupopoana....kama wewe umeamua kugawa kabla ya ndoa gawa tu kwa raha zako, K si mali yako bwana na wewe kama umeamua kujitunza ni uamuzi wako binafsi, ni jambo jema ila ni kwa faida yako wewe na kizazi chako.
Sent using
Jamii Forums mobile app