Ushauri: Waziri Mwigulu Nchemba ni liability kwa Uchumi wetu!

Ushauri: Waziri Mwigulu Nchemba ni liability kwa Uchumi wetu!

Salaam,Shalom!!

Nimesikia Mh Mwigulu, waziri wa Fedha akilalama kuwa, Wafanyabiashara waliopewa nafasi ya kukusanya Kodi Kwa niaba ya Serikali ni chanzo Cha kukosekana mapato ya Serikali.

Ukisikiliza Kwa ufahamu kauli hiyo, analenga kuwaelekeza TRA warudi tena Kwa wafanyabiashara na kuwabana tena wakipigiwa Kodi kandamizi za miaka ya nyuma. Nia hii inapingana na Nia ya Rais ya kukusanya Kodi Kwa akili.

Nia hiyo ya kuminya wafanyabiashara Si njema, na kamwe haiwezi kuinua Uchumi wa Nchi yetu, kupata Kodi, ni LAZIMA kuwatengenezea wadau mazingira mazuri ya biashara.

Mazingira mazuri ya biashara nchini, ni pamoja na kupunguza gharama ya umeme, BWAWA limejengwa Kwa mkopo, na pesa Inatakiwa ilipwe, kupunguza Bei ya unit ya umeme kutusaidia kuongezeka Kwa domestic industries za chini, kati na juu. Kujua Kwa viwanda vya ndani kutaongeza mauzo ya nje ya Nchi, kutaongeza ajira na kuongeza mzunguko wa pesa nchini. Haya Mawazo ya kuuza umeme nje ya Nchi yanatoka wapi!!

Kuinua Uchumi wa Nchi ni kubadili mtizamo wa kukopa Kila kukicha. Jambo Hilo ,Mwigulu limemshinda, hivyo mtu sahihi ni kukaa nafasi hiyo ni Mh Kimei.

Waziri Mwigulu ameshindwa kuhakikisha nchi inapata pesa za kigeni za kutosha Kwa kuimarisha Exportation ya bidhaa za ndani, Badala yake nchi yetu inageuka gulio la bidhaa Toka china ambalo linachangia pakubwa kukosekana Kwa pesa za kigeni.

Ni Imani yangu Waziri Mwigulu hajaota mizizi, hivyo naamini ni Rahisi tu kuondolewa na kuwekwa mwingine.

Ni mengi ya kusema, lakini itoshe kusema, Mwigulu Nchemba imetosha sasa!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Uko sawa mkuu
Ccm na vibaraka untouchable wamemiliki uchumi, tulete sera za liberalize uchumi

Umeme wamehodi
Mafuta wamehodhi
Usafarishaji wamehodhi
Madini wamehodi
Naliasili wamehodi

Serikari imekuwa kama kibaraka wa hao matycoon, mipango ya serikali inalenga kuwakingia kifua hao matycoon wasiathirike hivyo
Nchi inakosa mapato mengi tu

Mfano Nini kinazuia kuwekeza ili tuwe na umeme wa uhakika wa bei nafuu ili tuvutjie viwanda na uwekezaji?
Jibu ni matycoon Wachache wanafaidika na hii Hali. Ya umeme

Waziri analalamika lawama anawasukimia wafanyabiasharawadogo wasio na hatia, anawaogopa matycoon

Nyerere aliwahi sema ukiona serikari inakimbizana na wachuuzi ujue ni corrupt

Serikali unawalinda walarushwa inakimbizana na machinga
 
Hiyo ni kazi ya Waziri wa fedha ya kuongeza exports za bidhaa tunazozalisha?
Huoni Kuna mahusiano ya Moja Kwa moja kuhusu kutengeneza mazingira mazuri ya biashara nchini na kupunguza Kodi kunahusiana na kusaidia exports?

Hujui kuwa hizo wizara zinatefemeana? BILA exports kujua, Kodi utatoka wapi?

Karibu 🙏
 
Anatakiwa mchumi mwenye uwezo kweli asiye na tamaa na hela, hawa watu ni vyema wakaandaliwa na sio teua teua ya hawa wachumia tumbo.
Nakuunga mkono nitofautia e na mleta mada si lazima awe kimei, raisi anaweza teua mtu mwenye sifa na kumpa ubunge then uwaziri

Ingawa nayo ni soln ya muda mfupi. Yunatakiwa turudi kwenye sera

Mwigulu aende kwenye chama kutekeleza sera zake za kuua wapinzani
 
Uko sawa mkuu
Ccm na vibaraka untouchable wamemiliki uchumi, tulete sera za liberalize uchumi

Umeme wamehodi
Mafuta wamehodhi
Usafarishaji wamehodhi
Madini wamehodi
Naliasili wamehodi

Serikari imekuwa kama kibaraka wa hao matycoon, mipango ya serikali inalenga kuwakingia kifua hao matycoon wasiathirike hivyo
Nchi inakosa mapato mengi tu

Mfano Nini kinazuia kuwekeza ili tuwe na umeme wa uhakika wa bei nafuu ili tuvutjie viwanda na uwekezaji?
Jibu ni matycoon Wachache wanafaidika na hii Hali. Ya umeme

Waziri analalamika lawama anawasukimia wafanyabiasharawadogo wasio na hatia, anawaogopa matycoon

Nyerere aliwahi sema ukiona serikari inakimbizana na wachuuzi ujue ni corrupt

Serikali unawalinda walarushwa inakimbizana na machinga
Watafika mwisho tu,

Walikuwa wanapika data kuwa Mapato yamepaa, saiz wanataka kurudi kuminya tena wafanya BIASHARA wanaotembelea choki🤔
 
NADHANI KUNA KIASI AIDHA FIGURE AU LAMSAM TUNAIKOSA KUPITIA BANDARI,THERE IS A HUGE ECONOMY SHAKE UP!
Namaanisha kwa kifungo ambacho inawezekana tumekiingia, yawezekana yale maswala ya serekali kuna mapungufu hapa tupatieni hiki, yakawa yanashindikana kwa kifungo cha mkataba huo.
 
Huyu kweli hajaota mizizi. Mawaziri ambao wameota mizizi na haitatokea waondolewe hata Rais Samia atawale miaka 30 ni Mchengerwa, Makamba na Ummy Mwalimu. Wengine waliobaki ni suala la muda tu.
 
Nchi Haina umeme halafu eti waziri anatagemea uchumi.na mapato ya nchi yapande?

Hao wafanyabiasha hela za Kodi watazitoa wapi wakati miaka 2 hatuna umeme
Hiyo Inaitwa,

Kuvuna usichopanda,

Unamkamua ngombe ambaye hukumbuki mara ya mwisho lini ulimpa maji na malisho!!

Waziri huyu aondolewe haraka.
 
Kodi haijawahi kuwa rahisi kukusanywa.
Mbona watumishi wa Serikali inakusanywa kirahisi?

Iweje washindwe kujua nini wafanye Ili biashara zianzishwe, zikue Kisha ajira zitengenezwe Kodi ikusanywe Kwa wingi?

Kuyafikia hayo ,unahitaji mchumi Original, Si huyu mgambo mkamua wachuuzi!!
 
Mie kwa ujumla simuamini Mwigulu, Nape pamoja na Makamba.
Magu pamoja na mawenge yake naamini aliwatimua kazi kwasabb walichemka...haiwezi kuwa hivi hivi tuu!.
Sasa huyu malkia ye kasomba tu ili mradi kashauriwa na JK.
Sasa Kwa kuwa ushauri Si amri,

Apime ushauri, mbaya aachane nao, achukue ushauri mzuri Toka Kwa wananchi wanaoshauri katika Kweli na HAKI!
 
Soln
1. Punguza au ondoa baadhi ya Kodi tozo kwenye biashara na manufacturing industry

2. ondoa burecracy na unnecessary compliance procedures,

ili uanzishr biashmhara bongo Kuna compliance zaidi ya 20 kupata vibali, tozo kuwe na approval fees Chache na zote zilipiwe sehemu Moja one stop centres taasisi zikagawane

3. Leta umeme wa uhakika karibu na bure unit 1 iuzwe angalau sh 50

4. Selikaliv ipunguze matumizi ya hovyo, serikali ije na mpango angalau wa kupunguza matumizi kwa 50%
5.
6.
 
Salaam,Shalom!!

Nimesikia Mh Mwigulu, waziri wa Fedha akilalama kuwa, Wafanyabiashara waliopewa nafasi ya kukusanya Kodi Kwa niaba ya Serikali ni chanzo Cha kukosekana mapato ya Serikali.

Ukisikiliza Kwa ufahamu kauli hiyo, analenga kuwaelekeza TRA warudi tena Kwa wafanyabiashara na kuwabana tena wakipigiwa Kodi kandamizi za miaka ya nyuma. Nia hii inapingana na Nia ya Rais ya kukusanya Kodi Kwa akili.

Nia hiyo ya kuminya wafanyabiashara Si njema, na kamwe haiwezi kuinua Uchumi wa Nchi yetu, kupata Kodi, ni LAZIMA kuwatengenezea wadau mazingira mazuri ya biashara.

Mazingira mazuri ya biashara nchini, ni pamoja na kupunguza gharama ya umeme, BWAWA limejengwa Kwa mkopo, na pesa Inatakiwa ilipwe, kupunguza Bei ya unit ya umeme kutasaidia kuongezeka Kwa domestic industries za chini, kati na juu. Kukua Kwa viwanda vya ndani kutaongeza mauzo ya nje ya Nchi, kutaongeza ajira na kuongeza mzunguko wa pesa nchini. Yote hayo, yana connection na wizara ya Fedha, Haya Mawazo ya kuuza umeme nje ya Nchi yanatoka wapi!!

Kuinua Uchumi wa Nchi ni kubadili mtizamo wa kukopa Kila kukicha. Jambo Hilo ,Mwigulu limemshinda, hivyo mtu sahihi ni kukaa nafasi hiyo ni Mh Kimei.

Waziri Mwigulu ameshindwa kuhakikisha nchi inapata pesa za kigeni za kutosha Kwa kuimarisha Exportation ya bidhaa za ndani Kwa kushindwa kuweka mazingira mazuri ya biashara, Badala yake nchi yetu inageuka gulio la bidhaa Toka china ambalo linachangia pakubwa kukosekana Kwa pesa za kigeni.

Ni Imani yangu Waziri Mwigulu hajaota mizizi, hivyo naamini ni Rahisi tu kuondolewa na kuwekwa mwingine.

Ni mengi ya kusema, lakini itoshe kusema, Mwigulu Nchemba imetosha sasa!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Mkuu mleta mada tatizo kubwa la hoja yako ni kwamba hujajiuliza au (kiusahihi zaidi) hujaona umuhimu wa kujiuliza kuwa mteuzi wa Mwigulu anataka nini hasa katika nafasi hiyo. Ana malengo gani hapo? Ni kama umekisia (assume) tu kuwa anahitaji mtu mwenye sifa ulizozibainisha. Haiko hivyo katika nchi hii.

Je, unaamini Kimei ana sifa muhimu anazozihitaji mteuzi katika nafasi hiyo? Kwamba mzani wa mteuzi ukiwekwa Kimei atamshinda Mwigulu kwa sifa za mteuzi kuhusu nafasi hiyo?

Unaweza kuwa na “ndoto” njema sana kuhusu nchi yako. Lakini, be realistic. Tatizo haliko hapo unapofikiri.
 
Back
Top Bottom