Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Ndio maana nimemjibu mdau hapo. Nenda Kisiju Pwani.....huko njiani ni vichaka mpaka unashangaa kama upo misitu ya Congo.
Vile ni vijiji na vitongoji na kila unachoita kichaka ni mashokora ya watu[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hii nchi ina shida katika utawala, hasa decision makers. Wanagawa mikoa tu daily, kuna tija gani? Labda tujiulize, wangapi leo hii wanaenda ofisi ya mkoa? Kufata nini?
Je, hicho wanachokifata hawawezi kukipata hapo walipo?
Eti mwalimu anaenda mkoani anatoka Rufiji au Mafia mpaka Kibaha maili 1 kupeleka barua ya kuomba uhamisho kwa afisa elimu mkoa. Wakati tunaishi dunia yenye email na simu.

Hatuhitaji mikoa mingi. Tunahitaji utoaji huduma ulio bora katika mikoa michache tu. Hilo lingepangiliwa pamoja na mipango miji, serikali ingeweza kuhudumia population yote ijayo.
Hakika umeongea vema sana
 
Vile ni vijiji na vitongoji na kila unachoita kichaka ni mashokora ya watu[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Mashokora hayalimwi, yana minazi iliyozeeka mirefuuuu na mikorosho iliyozingirwa na vichaka. Hongereni lakini.
 
Hata Mm natamani Morogoro imegwe! Ipungue
[emoji23][emoji23][emoji23] Ukubwa ulionao Morogoro kwa sasa hujatosheka nao unataka uiongezee na pwani pamoja na Dar boss[emoji28] fikiria kwanza
 
Pwani ni ndogo kwa Ruvuma, Tabora na Morogoro!
Hilo Jambo nilikuwa naliwaza Leo mchana wakati nakuja Moshi...nkasema hivi kwanini mkoa wa pwani usigawanywe ...maana ukitoka bagamoyo Hadi mpakani mkoa wa Tanga Ni kipande..halafu ndio useme Hadi rufiji Ni mkoa mmoja..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
chalinze, Kibaha, Bagamoyo, Ruvu na Wami hao wote wawe Dar es salaam..

Mbagala,Mkuranga, Kisarawe, rufiji, Kibiti, Kilwa Iwe Pwani makao makuu Mkuranga..
 
Kipindi nakua mji ulikuwa mwisho ubungo, pale lilipo jengo la Tanesco ndio ulikuwa mzani wa kupima malori ambao sasa uko mkoa wa Pwani, Dar inakuwa kuelekea kaskazini,npaka wa Dar na kibaha unafutika, mpaka wa Dar, Bagamoyo unafutika kwa kasi sababu ya ujenzi unaokuwa kwa kasi ya ajabu.

Jiografia ya mkoa wa Pwani inashangaza sana, mtu wa Bagamoyo akitaka kwenda Rufijii au mafia lazima apitie Dar au apande chombo cha baharini. Ushauri wangu
Hizi wilaya mbili Kibaha na Bagamoyo zije Dar, ili kubalance mapato na uchumi wa mkoa wa Pwani Kigamboni na Mbagala yote iende Pwani,waungane na Mkuranga,Kisarawe, Mafia Kibiti na Rufiji.

Faida zake:

Jiji la Dar eS Salaam litapumua kwa kupata ardhi ya kutosha na kukua kwa kasi ya ajabu kibaha itakuwa kama urusi kwa technology na viwanda na Bagamoyo zitakuwa kama ukraine kwa utalii, pata picha chalinze iwe ni sehemu ya Dar es Salaam.

Tuje Pwani sasa.

Pwani kwa kupewa Kigamboni na Mbagala itachangamka sana, tatizo la Pwani ni kukosa amsha amsha. Mbagala itakuwa Dubai mpya kwa biashara mpaka sasa Mbagala inazidi baadhi ya mikoa kwa idadi ya watu na amsha amsha ya kibiashara njoo Mbagala kuanzia saa kumi jioni mpaka saa nne usiku hutaamini macho yako pata picha Mbagala iko Pwani na na sehemu ya Kigamboni itakuwa Paris au Spain sehemu za kula bata kwenye fukwe.

Mto mzinga utenganishe dar na Pwani.Bandari ibaki Dar
Wakazi wengi wa Mbagala wana asili ya Pwani au Kusini mwa Tanzania, watafurahi kurudi nyumbani kwa style nyingine.
Chawa wa mama mfikishieni hii
Nakubali..mbagala, Mbande,Mvuti,Msongola, chanika, Pugu ,kisemvule,vikindu zote ziende mkoa wa Pwani
 
Dar es salaam imezungukwa na mkoa wa Pwani katika pembe tatu..upande wa kaskazini , kusini na magharibi yote imezungukwa na mkoa wa pwani , upande wa mashariki tu ndio unepakana na bahari
 
MAPINGA, KEREGE, ZINGA ukizihamishia DAR na Majirani zao nao watakuwa karibu na DAR utasema tena hivo hivo
Kama mapinga na kerege na zinga uwezi kuzitofautisha na dar mfano Bunju na Tegeta.
Naunga mkono baadhi ya maeneo yasogezwe dar kama sio wilaya nzima.
 
Mimi ningekua na uwezo ningehamisha mkoa mzima wa pwani na morogoro na kuuleta Dar ili kutengeneza mkoa mmoja, service delivery ingekua ndio msingi sio utitiri wa hii kitu,nchi nzima mikoa 12 tu.
Mkoa wa morogoro unaujua wewe,?

Kwa taarifa tu huu mkoa ukiumega zinatoka dar 3.
 
Mkoa wa morogoro unaujua wewe,?

Kwa taarifa tu huu mkoa ukiumega zinatoka dar 3.
Huijui morogoro kumbe wala huijui dar,kwa morogoro zinatoka dar si chini ya 40,d ar km za mraba 1500,morgoro km za mraba 70000
 
Mkoa wa morogoro unaujua wewe,?

Kwa taarifa tu huu mkoa ukiumega zinatoka dar 3.
Soma unielewe pumbavu wewe, ukubwa au udogo wa eneo sio issue hapa, common man on the ground need services delivery.
 
Kipindi nakua mji ulikuwa mwisho ubungo, pale lilipo jengo la Tanesco ndio ulikuwa mzani wa kupima malori ambao sasa uko mkoa wa Pwani, Dar inakuwa kuelekea kaskazini,npaka wa Dar na kibaha unafutika, mpaka wa Dar, Bagamoyo unafutika kwa kasi sababu ya ujenzi unaokuwa kwa kasi ya ajabu.

Jiografia ya mkoa wa Pwani inashangaza sana, mtu wa Bagamoyo akitaka kwenda Rufijii au mafia lazima apitie Dar au apande chombo cha baharini. Ushauri wangu
Hizi wilaya mbili Kibaha na Bagamoyo zije Dar, ili kubalance mapato na uchumi wa mkoa wa Pwani Kigamboni na Mbagala yote iende Pwani,waungane na Mkuranga,Kisarawe, Mafia Kibiti na Rufiji.

Faida zake:

Jiji la Dar eS Salaam litapumua kwa kupata ardhi ya kutosha na kukua kwa kasi ya ajabu kibaha itakuwa kama urusi kwa technology na viwanda na Bagamoyo zitakuwa kama ukraine kwa utalii, pata picha chalinze iwe ni sehemu ya Dar es Salaam.

Tuje Pwani sasa.

Pwani kwa kupewa Kigamboni na Mbagala itachangamka sana, tatizo la Pwani ni kukosa amsha amsha. Mbagala itakuwa Dubai mpya kwa biashara mpaka sasa Mbagala inazidi baadhi ya mikoa kwa idadi ya watu na amsha amsha ya kibiashara njoo Mbagala kuanzia saa kumi jioni mpaka saa nne usiku hutaamini macho yako kila aina ya biashara utaikuta .pata picha Mbagala iko Pwani na na sehemu ya Kigamboni itakuwa Paris au Spain sehemu za kula bata kwenye fukwe.

Bandari ibaki Dar.Wakazi wengi wa Mbagala wana asili ya Pwani au Kusini mwa Tanzania, watafurahi kurudi nyumbani kwa style nyingine.
Chawa wa mama mfikishieni hii
Sasa mkuu mpaka wa Dsm na Pwani utakua wapi? kama Mbgl na Kigamboni zikiwa Pwani
 
Kimsingi dsm ibaki kama ilivyo..ila ardh yote irudi serikalini na wakazi wadsm wahamishwe serikali ijenge magorofa appartments za kutosha kisha warususiwe kuja kupangisha tu..hakuna kuruhusu mtu kujenge kama unataka kujenge nenda kajenge pwani huko.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ndio neon strategical..!! ila nawaza kwa serikali ijenge kwa fedha zipi? hizi za kukopa? Je fidia kwa wenye majengo yao?
 
Mimi ningekua na uwezo ningehamisha mkoa mzima wa pwani na morogoro na kuuleta Dar ili kutengeneza mkoa mmoja, service delivery ingekua ndio msingi sio utitiri wa hii kitu,nchi nzima mikoa 12 tu.
Ccm inavunja vunja nchi ili kugawana vyeo na kufanya ufisadi wa pesa za umma ,
 
Back
Top Bottom