Binafsi nina visa vingi nimewahi kumbana navyo vya kuchukuliwa powa. Hapa nitataja vinne tu.
1.Nakumbuka nilihamia sehemu fulani ofisi flani mahali fulani.
Kwa vile nilikuwa mgeni sikuhama na kitu chochote zaidi ya mi mwenyewe.
Basi nikawa na tabia ya kwenda kula kwa mama ntilie ugali wa buku japo pale jirani kulikuwako na mgahawa mmoja wa kiwango cha juu kwa ajili ya watu wa tabaka la juu .
Wateja wenzangu wengi wao walikuwa bodaboda na machinga. Yule mama ntilie pamoja na wasaidizi wake walikuwa wababe na kauli mbaya kwa wateja wao, kiujumla kwao mteja alikuwa sio mfalme bali lofa.
Jioni moja nikaomba niongezewe mboga kidogo ili nimalizie ugali wangu lakini nilijibiwa kwa jibu la dharau sana mpaka wateja wenzangu wakanicheka.
Tangu siku hiyo nikahamia kwenye mgahawa wa wadosi nikawa nakatiza kwa mamantilie naingia mgahawa wa kishua. Yule dada akawa anapatwa na mshangao kama haamini kama ninauwezo wakula kule.
Lakini pia akaanza kuniona na kampani za watu fulani ambao wanafahamika na ni maarufu eneo lile. Tangu kipindi hicho akawa anajichekesha chekesha kwangu maana alisha fahamu nafasi yangu ndani ya jamii yao ila nashukuru sikuwahi kumshobokea hata kwa salamu.
2 Nikiwa ofisini, kwa vile nilikuwa mgeni, siku moja aliingia mteja ofisini akanikuta nimekaa kwenye meza yenye ya wageni, nilifanya hivyo ili kujipatia mazingira ya urelax kwa assigment niliyokuwa nafanya kwa muda ule. Ili kufanikisha hilo kiti changu na meza yake ninavyotumia kufanyia kazi vilibaki wazi hivyo ikawa kana kwamba mi ni mgeni na boss hayupo maana kiti hakina mtu.
Mara nikaona jamaa amefungua mlango ghafla nakuanza kuuliza bila hata kusalimia. Jamaa akawa ananiuliza huku akinyosha kudole kwenye kiti cha boss " jamaa yuko wapi" nikamjibu "katoka kidogo" Mara nikaona PS anaingia ofisini na kuniuliza "huyu mgeni hajakuona kwani mbona kasema hakuna mtu"? Nikamjibu mwambie aingie.
Basi yule jamaa akaingia ila hakuwa na confudence tena maana alishavurugika kisaikolojia japo nilijitahidi kumjenga kisaikolojia na kumuhuumia vizuri.
3.Siku ingine nafika ofisini nakuta wamama wawili wamekaa kwenye benchi wanamsubiri mwenye ofisi, nikasimama na kawasalima vizuri kwa utulivu, mmoja kajibu kwa kujilazimisha kwa kubetua mdomo yaani ni kama wananishit wanaona nawapotezea muda maana wanamsubiri boss wamweleze kilio chao. Basi nikaingia ofisini kidogo kama dk 3 kisha nikatoka nnje mara nikasikia PS anawambie " nyie mbona hamwingii?, anaondoka huyo! Mara nasikia kwa nyuma watu wananikimbilia huku wanaita kwa sauti za unyonge" baba samahani tunashida na wee! Nikasimama na kuwaomba twende ofisini tuongee. Niliwahudumia vizuri japo walisha potewa na confidence maana nafsi ziliwasuta maana waliuchukulia poa mwonekano na umri wangu nadhani.
3. Juzi kati nilipanda basi kuelekea mkoa fulani. Kwa vile nilipandia njiani nikapata siti jirani na dada wa makamo bonge. Nikamsalimia vizuri ila hakuitikia kwa kutoa sauti bali akatikisa kichwa tu . Baada ya mwendo wa safari ndefu, nadhani mdada alinisoma na kugundua alini underate kwa makosa. Basi akaanza kujitahidi kuniongelesha mara ooooh, "samahani kaka eti hapa ndo wapi," ooooh, "kaka hivi we ni mwenyeji ............"(anataja jina la mji tunaoelekea) Sikumshobokea , nami nikawa namjibu kwa kutikisa kichwa tu huku niko bize na simu yangu.
4.Juzi nimehudhuria harusi ya jamaa yangu. Nilikuwa peke yangu kwa vile wife alikuwa na udhuru.
Basi nikaelekezwa kwenye meza moja ambayo tayari ilikuwa na wenza wawili (umri kati ya 30 na 35) Basi nikawasalimia kwa sauti huku nikivuta kiti na mie nikae. Yule mdada aliitikia lakini mwanaume hakuitikia.
Ukaja muda wa kugobganisha glasi kila mtu na jirani yake , kwa vile nilikuwa sina mtu mingine zaidi yao nikagonganisha nao glasi lakini naona yule mkaka kama hataki . Ok, shughuli ikaendelea naona jamaa yuko bize na kushikana shikana na mpenzi wake nami niko bize na simu yangu.
Tumekula chakula tumemaliza mi sikuwa na haraka ya kuondoka ukumbini maana nilikuwa bado namalizia kinywaji changu. Basi baada ya kumaliza kula naona msela ananyanyuka anamvuta demu anamwambia "twende zetu acha hiyo" demu akaiacha redbull ambayo ndio kwanza ameifungua. Kwa vile tulikuwa mimi na wao pale mezani nilitarajia angalau " broh sie ngoja tutangulie"!
Bada ya kama dk 15 namimi nikatoka ukumbini ili nirudi home maana ilikuwa yapata saa 7 za usiku. Nafika karibu na parking, nawakuta wale mtu na demu wake bado wapo kumbe wanasubiri bodaboda huku wakipata adhabu ya kipupwe cha usiku . Nikawapita kwa karibu, nikaingia kwenye usafiri wangu nikawasogelea nikashusha kioo kidogo na kuwaaga "jamani mi natangulia, naona nyie bado mpo". Sijui kama walijibu ama la ila nilichogundua niliona msela amekosa confidence na amekuwa mnyonge saana.
Yawezekana kuwa na madhaifu ya kibinadamu ila kujisocialize na watu bila kujali hadhi zao ni faida kwako kuliko hasara.