Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Namuonagaonaga hivi kama Hisa anazomiliki huyo jamaa zinaweza kuwa na thamani gani kwa pesa, au utajiri wake unaweza kuwaje maana radio naichuliaga poa.

Naomba eleza kama unajua.
labda tukadirie haitashuka 600mln.na anayo gari moja ya kibabe range.

hayo ni ya macho sijajua ya sirini bank huko na kwingineko.
 
labda tukadirie haitashuka 600mln.na anayo gari moja ya kibabe range.

hayo ni ya macho sijajua ya sirini bank huko na kwingineko.
Yaani Hisa kubwa ni 600M kwa tathminj kwa mantiki hii radio nzima haifikishi 1.5B kwa thamani.
 
Nilikaribishwa na binamu zangu me nikaenda, kufika nikakuta wageni ambao ni mama yao mkubwa na mama mdogo, mdogo wao pia mzazi mwenzie yule me mkubwa. Kuna wanaonijua pale na wengine hawanijui Ila wananisikia. Baada ya kutambulishwa hakuna aliyenijali kabisa hadi nikajisikia unyonge yaani ni wale vijana ndio walinihudumia kila kitu hawakuwa na muda na Mimi kabisa hao ke. Ikapita kama mwaka mmoja hivi dogo akataka kuoa wakafanya kikao kwa mama ya mdogo Mimi sikwenda niliwaambia chochote watakachohitaji nitatoa Ila sitofika hapo, baadae muoaji akaniomba harusi iingilie nyumbani kwangu baada ya wiki mbili watakwenda kwenye chumba chao nikawakubalia. Ikawa kila akiulizwa swali bwana harusi mtarajiwa anajibu nitamuuliza dada X. Ikabidi wamwambie huyu X aje hapo atudhirishie kama kwenye yeye atabeba mzigo huo na haya mengine unayoyataja, akanipigia simu palepale nikajibu Jumamosi ijayo nitakuja kweli nikaenda nikaulizwa yote nikakubali. Nikawaelekeza kwangu hivyo wakaja tukafanya harusi wakaondoka [emoji3][emoji3][emoji3]. Kuanzia hapo heshima juu. Maana wote walihudhuria, kubwa na Kali yule aliyekuwa ananipandisha na kunishusha siku iso na jina akanieleza matatizo yake ya ugonjwa nikamugharamikia. Hadi sasa heshima juu. Nashukuru simdharau mtu ila napenda kuwa mkweli na sijutii hilo, hivyo jibu langu mtu anaweza fikiri nimemdharau
mkuu hata cjaelewa hii story yako ase
 
Binafsi nina visa vingi nimewahi kumbana navyo vya kuchukuliwa powa. Hapa nitataja vinne tu.

1.Nakumbuka nilihamia sehemu fulani ofisi flani mahali fulani.
Kwa vile nilikuwa mgeni sikuhama na kitu chochote zaidi ya mi mwenyewe.

Basi nikawa na tabia ya kwenda kula kwa mama ntilie ugali wa buku japo pale jirani kulikuwako na mgahawa mmoja wa kiwango cha juu kwa ajili ya watu wa tabaka la juu .

Wateja wenzangu wengi wao walikuwa bodaboda na machinga. Yule mama ntilie pamoja na wasaidizi wake walikuwa wababe na kauli mbaya kwa wateja wao, kiujumla kwao mteja alikuwa sio mfalme bali lofa.

Jioni moja nikaomba niongezewe mboga kidogo ili nimalizie ugali wangu lakini nilijibiwa kwa jibu la dharau sana mpaka wateja wenzangu wakanicheka.

Tangu siku hiyo nikahamia kwenye mgahawa wa wadosi nikawa nakatiza kwa mamantilie naingia mgahawa wa kishua. Yule dada akawa anapatwa na mshangao kama haamini kama ninauwezo wakula kule.

Lakini pia akaanza kuniona na kampani za watu fulani ambao wanafahamika na ni maarufu eneo lile. Tangu kipindi hicho akawa anajichekesha chekesha kwangu maana alisha fahamu nafasi yangu ndani ya jamii yao ila nashukuru sikuwahi kumshobokea hata kwa salamu.


2 Nikiwa ofisini, kwa vile nilikuwa mgeni, siku moja aliingia mteja ofisini akanikuta nimekaa kwenye meza yenye ya wageni, nilifanya hivyo ili kujipatia mazingira ya urelax kwa assigment niliyokuwa nafanya kwa muda ule. Ili kufanikisha hilo kiti changu na meza yake ninavyotumia kufanyia kazi vilibaki wazi hivyo ikawa kana kwamba mi ni mgeni na boss hayupo maana kiti hakina mtu.
Mara nikaona jamaa amefungua mlango ghafla nakuanza kuuliza bila hata kusalimia. Jamaa akawa ananiuliza huku akinyosha kudole kwenye kiti cha boss " jamaa yuko wapi" nikamjibu "katoka kidogo" Mara nikaona PS anaingia ofisini na kuniuliza "huyu mgeni hajakuona kwani mbona kasema hakuna mtu"? Nikamjibu mwambie aingie.

Basi yule jamaa akaingia ila hakuwa na confudence tena maana alishavurugika kisaikolojia japo nilijitahidi kumjenga kisaikolojia na kumuhuumia vizuri.

3.Siku ingine nafika ofisini nakuta wamama wawili wamekaa kwenye benchi wanamsubiri mwenye ofisi, nikasimama na kawasalima vizuri kwa utulivu, mmoja kajibu kwa kujilazimisha kwa kubetua mdomo yaani ni kama wananishit wanaona nawapotezea muda maana wanamsubiri boss wamweleze kilio chao. Basi nikaingia ofisini kidogo kama dk 3 kisha nikatoka nnje mara nikasikia PS anawambie " nyie mbona hamwingii?, anaondoka huyo! Mara nasikia kwa nyuma watu wananikimbilia huku wanaita kwa sauti za unyonge" baba samahani tunashida na wee! Nikasimama na kuwaomba twende ofisini tuongee. Niliwahudumia vizuri japo walisha potewa na confidence maana nafsi ziliwasuta maana waliuchukulia poa mwonekano na umri wangu nadhani.


3. Juzi kati nilipanda basi kuelekea mkoa fulani. Kwa vile nilipandia njiani nikapata siti jirani na dada wa makamo bonge. Nikamsalimia vizuri ila hakuitikia kwa kutoa sauti bali akatikisa kichwa tu . Baada ya mwendo wa safari ndefu, nadhani mdada alinisoma na kugundua alini underate kwa makosa. Basi akaanza kujitahidi kuniongelesha mara ooooh, "samahani kaka eti hapa ndo wapi," ooooh, "kaka hivi we ni mwenyeji ............"(anataja jina la mji tunaoelekea) Sikumshobokea , nami nikawa namjibu kwa kutikisa kichwa tu huku niko bize na simu yangu.

4.Juzi nimehudhuria harusi ya jamaa yangu. Nilikuwa peke yangu kwa vile wife alikuwa na udhuru.
Basi nikaelekezwa kwenye meza moja ambayo tayari ilikuwa na wenza wawili (umri kati ya 30 na 35) Basi nikawasalimia kwa sauti huku nikivuta kiti na mie nikae. Yule mdada aliitikia lakini mwanaume hakuitikia.

Ukaja muda wa kugobganisha glasi kila mtu na jirani yake , kwa vile nilikuwa sina mtu mingine zaidi yao nikagonganisha nao glasi lakini naona yule mkaka kama hataki . Ok, shughuli ikaendelea naona jamaa yuko bize na kushikana shikana na mpenzi wake nami niko bize na simu yangu.

Tumekula chakula tumemaliza mi sikuwa na haraka ya kuondoka ukumbini maana nilikuwa bado namalizia kinywaji changu. Basi baada ya kumaliza kula naona msela ananyanyuka anamvuta demu anamwambia "twende zetu acha hiyo" demu akaiacha redbull ambayo ndio kwanza ameifungua. Kwa vile tulikuwa mimi na wao pale mezani nilitarajia angalau " broh sie ngoja tutangulie"!

Bada ya kama dk 15 namimi nikatoka ukumbini ili nirudi home maana ilikuwa yapata saa 7 za usiku. Nafika karibu na parking, nawakuta wale mtu na demu wake bado wapo kumbe wanasubiri bodaboda huku wakipata adhabu ya kipupwe cha usiku . Nikawapita kwa karibu, nikaingia kwenye usafiri wangu nikawasogelea nikashusha kioo kidogo na kuwaaga "jamani mi natangulia, naona nyie bado mpo". Sijui kama walijibu ama la ila nilichogundua niliona msela amekosa confidence na amekuwa mnyonge saana.


Yawezekana kuwa na madhaifu ya kibinadamu ila kujisocialize na watu bila kujali hadhi zao ni faida kwako kuliko hasara.
Asante kwa ushauri
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]watu wamefukua uzi wake
Mimi sijafukuzia uzi hata. Ni kwamba nineunganisha vitu kibao nikisema hapa nitakuwa nakosea maana nyingine ni kosa kwa sheria za JF. Na hata si uungwana mambo yake namwachia mwenyewe.
 
Kuna siku niliazima gari nikaenda pale best bite kuchukua zaga.

Sasa nilivyoingia ndani nikakutana na pisi tatu za kwenda zinatoka ndani, nikazipa hi zikachuna full kunipandisha na kunishusha, nikaona POA tu nikafuata kilichonipeleka.

Sasa ile natoka nje nikazikuta ziko bize zinajisnap kwenye gari niliyokua nayo, hiiiiiiiiii bagoshaaa, mbona walikoma kunijua.

Nilianzisha zogo la maana makusudi kabisa, nikaita mpaka uongozi wa pale nikawaambia wawaambie wateja wao wafute picha zote walizopiga gari yangu otherwise niite Askari pale obey waniambie Wana lengo gani na picha za mkwaju wangu?
Hapo kwenye 'mkwaju wangu' tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna kipindi nilikuwa nafanya kazi kampuni flani.Basi siku hiyo ninetoka kufanya mazoezi ya kukimbia kama kawaida yangu asubuhi.Halafu kipindi hicho mvua ilikuwa imenyesha usiku,Sasa ninerudi pale kazini nikawa nipo napiga story na walinzi zile raba na track zimechafuka balaa.Wakaja wadada wawili na boda boda mi nkaanza kuwasalimia kwa bashasha afu ndo nilikuwa naondoka kujipiga maji.Basi wale wadada wote walinipandisha kuanzia juu hadi chini wala hawakuitikia salam wakanipita wakaenda kwa walinzi,Basi mi nkaona noma nkaondoka zangu.Kumbe wale wadada wamekuja kumuulizia meneja wameleta barua za kuomba kazi na meneja mwenyew ni mimi.Nilivorudi walinzi wananambia wale wadada walikuwa wana shida na wewe wameacha barua zao za kuomba kazi.Nikasema mbona hawajanisubiri wakasema wameona aibu,jinsi walivokudharau.Kesho yake wakarudi kuomba nnamba zangu kwa walinzi mi sikuwepo nilienda mkoani walinzi wakanipigia nikawaambia wapeni tu.Kila mmoja akawa ananipigia kwa mda wake,na wote walichezea rungu ila kazi hawakupata walikuwa wangoni mmoja alidata hadi tukabahatika pata mtoto.
Acha roho mbaya mzee baba mzigo umekula na kazi hutoi mpaka umemzalisha unamtesa mwanao kwa kumpa mama jobless
 
Back
Top Bottom