Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Kuna siku moja Shahrukhan (mwigizaji wa Bollywood)alikuwa ndani ya ndege anasafiri kiti alichokuwa amekaa alikuwa na mzee mmoja anasoma kitabu kwenye ile sehemu kulikuwa na Abili wengine baada ya kugundua kuwa wapo na Shahrukhan wakaanza kumshobokea mara picha mara wanaomba kusainiwa kama kumbukumbu baada ya watu wote kwenye lile daraja lao kulidhika wakarudi kwenye viti vyao mjomba Shahrukhan kuna kitu kikamshangaza baada ya kujiuliza akashindwa kuvumilia ikabidi amuulize yule Abilia aliyekaa nae vipi mzee we hutaki picha na mimi kama kumbukumbu yako yule mzee akamjibu kwani unajua umekaa na nani Shahrukhan akamjibu hapana sifahamu yule mzee akamtajia jina lake kumbe bwana yule mzee ni Mmiliki wa kampuni ya Tata Nchini India ikabidi Shahrukhan awe mpole kimoyomoyo nadhani alisema kumbe mi ndo natakiwa kuomba picha.NB:Acha Dharau kwa Mtu usiyemfahamu.
 

Kanisani kwetu walikuwa wananichukulia poa,siku amekuja pastor mzungu mimi ndio nikawa natafsiri English to swahili
Baada ya hapo kanisani hadi watoto wadogo waliniheshimu
NB English ya kwenye biblia msiichukulie poa ni noma
Balaaa
 
Kuna kisa kimoja nimekikumbuka hapa,hii ni kuhusu fundisho kwamba ubishi mbaya,tujifunze kusikiliza

Nilikuwa nimepanga afrikana,nilikuwa na kinisani march kidogodogo,kinakula mafuta kidogo sana,so nikajua haya mafuta natoboa mpaka magomeni

Lahaula nafika makumbusho pale kituoni kikakata moto,sasa nikasahau kuwasha hazard zile indicator na kuweka triangle,sasa enzi hizo miaka 2014 kuna operation kamata kamata magari yanayo paki hovyo,jamaa wa tamesa pale magomeni wakanirukia,wewe bwana umepaki kituoni hujawasha hazard na kuweka triangle

Mimi kwa kawaida ni mnyenyekevu sana nikawaomba msamaha sana,jamaa wakakaza lazima twende yadi,na faini si chini ya 250,000 kama sijakosea,wakataka hela kubwa niwapoze nikawaambia wazee chukueni hiki kidogo tu tusameheane,jamaa wakakaza

NIkawambia jaman mimi nikienda huko natoka bure kabisa bora mchukue hiki kidogo tu ilikuwa 20,000,jamaa wanaona wananikomoa kwakuwa walitaka 100,000

Nikawaambia sawa huku nasisitiza jamani mtaikumbuka hata hii 20,000,wakaona labda nawapiga mikwala,nikaenda sheli na kidumu tia wese wengine wapo ndani ya kigar changu na wengine katika land lover yao,kimoyo moyo nasema hawa leo wataumbuka

Paap mpaka yadi pale maeneo ya magomeni,gari nikaingiza ndani,inaandikwa faini,nikaenda pembeni nikamvutia waya mshua ingawa alisha staafu lkn jina lake bado lina uzito,mshua chap akampigia boss wa kamata kamata,boss kaja tena kwa heshima akanisalimia

Mara chap boss wao anasema haya mpeni huyu kijana funguo yake aondoke,jamaa wananipa fungua huku wanaona haya aibu,wakakumbuka sasa maneno yangu

Nikapata faida nyingine nikapewa namba ya boss wa kamata kamata kwamba wakinisumbua ni simu moja tu chap shughuli imeisha

Tujifunze kusikiliza wakati mwingine
 
Hii kitu sijui ni nini asee,mfano jana tu hapa nikakutana na jamaa flani huwa tunaonana kwenye bar flani kila mmoja na hamsin zake,jana ananifuata ananiambia eti kuna shamba linauzwa hapo kibaha milioni 300 kama niko fresh aniunganishe na muuzaji,nikajisemea huyu mtu kanionaje wkt hata milioni 50 tu sina kwenye account?
 
Tea
 
Mkuu unavyodhania ni tofauti na uhalisia nilioukuta pale, ni vibinti vya kiswahili halafu nilikuwa navijibu kavu sana ndio maana vikaropoka sio chai ni uhalisia niliokutana nao, we vitoto vinatembea na vioo kwenye vikoba vyao Unategemea vikuogope?
Kama na wewe ulivijibu mbovu basi huna haja ya kusema vinadharau.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duuh😂😂 Red black pita huku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…