Ila kwakweli first impression inamata sana ndio maana matapeli pale posta mpya wana suti kali unaingia mkenge mwenyewe,kwahiyo huyo mtoa mada sio kwamba muongo ni kweli kabisa,watu wanakuchukulia jinsi wanavyokuona
Nakumbuka wakati mzee amehamishiwa wilaya ya kinondoni tukaenda kuishi oysterbay,sasa pale hatupo mbali sana coco beach,so unaweza tupia yebo yebo tu kisha unajisogeza tu beach
Nimekaa zangu beach,nikamuona mrembo anapita nikamuita,sasa wakati huo miguu yangu ilikuwa imezibwa na kigogo cha mnazi,demu kusogea si ndio akaniona nimevaa yebo yebo huwezi amini demu akasepa,,kimoyo moyo nacheka we hujui mimi ni mtoto wa kishua
Kwahiyo kwa kifupi jinsi gani unajiweka ndio watu wanakupa hadhi yako