Ushuhuda: Leo nimekutana na kipanga jeuri wa darasani. Kweli hakuna uhusiano wa uwezo darasani na wa maisha halisi


Mbona kuna wanaoitwa vilaza lakini bado wanasota? Asilimia kubwa wanapata kazi but ni huyo tu .......asi conclude kwa wote......jeuri sio nzuri kabisa km kweli basi alizingua.....

All in all ulikuwa utoto ,mbona majeuri wengine wapo mbali tu....


Life halina formula unaweza kuta jamaa akapata kibarua kizito tu akapaaa ndan ya mwaka mmoja .......

Usicheke nyani kabla haujavuka mto
 
"nikamkuta njiani kipanga nikamwambia apande kama anajitaji lifti yeye akasema anasubiri mtu".......Hapa ndio umeandika pumba kabisa
 
Nadhani tulikuwa wote tupo Ubungo-mataa tunataka kufika Posta mpya;
Wewe ukapitia mwenge mimi nikapitia Buguruni (tulikuwa tunapishana njia tu na pengine tusingepishana sana kufika safari yetu)

Shida hapa mwishoni umevurunda hadi sielewi umeingiwa na kitu gani au sijui nio usomi wenu wenzetu??

Tusizalishe mada nyingine ila kifupi hapo nilipokoleza kuna jambo;
Una Elimu kisha unashindwa kuwasomesha wanao hiyo ni akili au matope?????
Sikia ,
Yupo mzee namjua SINZA mfano hai kabisa ni
Std 7. ana mawe balaa, watoto watatu mmoja ndio kamaliza Chuo juzi tu,
Anasimamia vituo vya mafuta viwili Dar achilia mbali mirai mingine na majumba anayoyafuatilia mzee mwenyewe Dar na mikoani.

Sasa wewe endelea kuongeleza 'Digilii'.
 

Huyo mzee wako hata wanae wafikie hadi kuwa na PHD ila yeye atabakia kuwa darasa la saba TU. Hilo halibadiliki mkuu

Kingine usikariri maisha, si kila mtu anatamani kuwa kama Marehemu Mengi au Bakhresa. Kuna waalimu wamezalisha matajiri na viongozi wakubwa nchi hii lakini maisha yao hadi wanastaafu ni ya kawaida na wameridhika...

Pia usiangalie matajiri wachache wasio na elimu ukadhani walioshindwa elimu wamefanikiwa maisha kuliko wale wenye elimu utakuwa unajidanganya. Kaa na watu wasio na elimu kabisaaa uone wanahangaika kiasi gani labda utapata wazo ni kwa kiasi gani wanajuta kwa kupishana na fursa kibao sababu hata form four haipo kichwani
 
Maisha ni milima na mabonde, kuna kupanda na kushuka. Usishangae baada ya miaka kadhaa ukapata ajira kwa huyo kipanga unaemcheka
 
Wakati nasoma seco Kuna mmoja alikuwa ndiye mshika mkia darasani,lakini chakushangaza jamaa alikuwa na pesa za matumizi kuliko mwanafunzi yoyote darasani,ikifika mapumziko msururu wa marafiki anawanunulia chai na mazagazaga yakula,siku moja nilipita mtaani kwao nikamkuta anauza Chipsi tukasalimiana akaniambia hili ni goli langu la Chipsi,ndio nikajua kumbe zile pesa za matanuzi school anapataje,so Mafanikio ya maisha na akili za darasani ni vitu viwili tofauti.
 
Sijawahi kuponda wala kumdharau mtu kwalolote isipokuwa nikichokozwa tu.

Kwakuwa naona tumetoka kwenye mauhui ya hoja kuu pengine tuishie hapahapa,
ibaki tu, mwenye mavyeti akae nayo na mwenye mali bila vyeti atumbue maisha yake, itapendeza.
 
Umesoma chuo gani mkuu ambacho darasa zima mlikuwa agemate? Nimesoma vyuo 3 na hakuna nilichokuta wanafunzi wrote no agement au siku hizi Sera ya vyuo imebadirika.Au agemate sawa na classmate? Unapomkosoa mtu jaribu kufikiri kidogo sio kukurupuka tu.
 
Asante Lupweko ... wewe ni mtu mbadi.. jibu murua sana.. mtoa mada naona anahaha kukujibu..
 
Huyu kipanga alisoma Chuo gani.
Shule gani advance,
Shule gani O level
Shule gani ya msingi.
Naomba tuanzie hapo kwanza.

Maana kuna vipanga wengine ni butu kama huyo uliyetwambia.
 
Huu uzi unanikumbusha mambo ya ule uzi wangu mhitimu mambo nayopitia katika kipindi hiki
 
umeandika pumba, Vipanga ndio viongozi wako, vipanga ndio wako TRA, Vipanga ndio wapo TBS, Vipanga ndio wapo EWURA, Vipanga ndio wanaokutoza kodi, vipanga ndio wako ofisi ya Rais, vipanga ndio walimu vyuoni, vipanga ndio wanaokutibu ukiumwa. Futeni hizo pumba zenu.
 
Maisha yako hivi! ZIG -ZAG... usicheke na kudharau kwa sababu ya moto wa kisuri suri! unaompitia mwenzio!! huu nao ni ukilaza na kweli ulikuwa kilaza! Mimi nilikuwa kipanga hasa!! kaupepo kaka nipitia nikarudi zero haswa. huko mkoa!
,
from no where ukanipitia upepo mzuri! nikatumia CV Zangu zile zile! niliponyoka kama Mshale Mzoefu ziakani! Pyaaaa! yule mbwiga alinipa somo! na alibaki vilevile! alivo zaidi eti bila aibu wala kumbukumbu ananitafuta nimpe line za maisha! ndo km wewe! mtu alie nicheka nimpe line???

Siri ya Maisha heshimu, saidia kila mtu aliye chini yako hujui kesho yako! wala mtoto wako ataishia wapi!! tena km alikuwa mtu mzuri shirikiana nae! lkn kumbe wewe ulikuwa unaumia!! ulivo muona anavo peta sasa nakupa miaka 3 km utamuona akisua sua kimaisha!!! some times tenda wema uende zako,

huenda alikuwa haringi mtu wa watu, unaonekana wewe mzushi flani hivi mwenye kinyongoooo! kile cha kichawi!! ningekuwa mimi huyo jamaa kwa mtu km wewe haloooo! ntajifanya sikujui kabisaaaaaaaaaaa! hata tukiwa kijijni kwetu utakuwa wa kawaida sana tena siyo mara moja kil siku, kamwe sitaki ushirika na mtu km weye! utajitambulisha kila siku!! bora ujipitie tuuu!

Nitusue!! nisi tusue!! kimaisha naku dellete mazimaaaaaaa!! lkn km ulikuwa mtu wa neno! mtu wa msaada sijui upendo aaah! kwangu asee!! ntakupendaje? ntakupa ushirika mpaka napo kuwa Rais wa jamhuri, km Boyz 2Men! na hukosi ka uwaziri MKuu!

hata iweje wanao sijui mkeo watapeta kwa mgongo wangu. ili mradi tu mimi Rais. na watu wema wa hivi wamo humu Duniani humu wengi tu Mbona!!! km Dr Evelyn Zagwi yaani yule Dr labda nisiwe Rais! Lazima ale bure vya Ikulu! hata iweje!!
 
Kilaza katika ubora wake.
Haya maisha yana siri kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…