Ushuhuda: Leo nimekutana na kipanga jeuri wa darasani. Kweli hakuna uhusiano wa uwezo darasani na wa maisha halisi

Ushuhuda: Leo nimekutana na kipanga jeuri wa darasani. Kweli hakuna uhusiano wa uwezo darasani na wa maisha halisi

Wewe ni mjinga hata kudanganya hujui!
IQ yako ndogo sana! Mtu mliyesoma naye darasa moja obviously atakuwa age mate wako!
Sasa ulivyom-address na huyo rafiki yako alivyom- address kijana wake wa kazi kwako obviously hakuna uhalisia wowote! Hizi ni story za vil.aza kutungia vil.aza wenzao
eti kijana wa kazi[emoji2]
 
Nakuona na wewe ni mshamba fulani, hata kama ulijua huyo kipanga ndie ulitakiwa umchukulie kawaida tu, lakini inaonekana kwa ushamba wako ulimtazama kwa jicho fulani la kiumbea la kutoamini kama ni yeye hali iliyompelekea ajihami kwa kukwamnia hiyo biashara ni yake, laiti ungekuwa na akili ya kiutu uzima hilo lisingetokea.

Hii dunia huwa haieleweki, iko siku huyo kipanga atapanda juu wewe urudi chini ndio utapata akili, haya maisha siku zote unatakiwa umuangalie mwenzio halafu upite zako, sio unaanza kuhukumu wengine.
 
Mimi nilikuwa kipanga pale pugu sekondari combination ya PCB mwisho wa siku nikajikuta mlimani BSc Education. Wenzangu wengine vilaza wenye connection pamoja na kupata division III walienda Algeria na China kusoma medicine, wengine wazazi wao wenye uelewa wakawaambia wakasome wildlife sasa hivi wako TANAPA.

Hawa jamaa hawakuamini kwamba yule mtabe wa organic, cytology na simple harmonic motion kawa ticha.

Nilifundisha miaka miwili nikaenda kupiga degree nyingine tofauti. Haya maisha yana mengi ya kujifunza.
 
Ndio maana huko niliko kwenye group moja ya secondary huwa na mute kimyaaaa kwasababu ya vichuki chuki vya kijinga kama hivi watu kukupiga majungu kisa ulikua unawakimbiza darasani ila maisha hamtofautiani kivilee mtaani wanaona kama ulikua una ringa hata kama walikua washkaji zako .Wivu mbaya sana. 😂😂😂
 
Wewe ni mjinga hata kudanganya hujui!
IQ yako ndogo sana! Mtu mliyesoma naye darasa moja obviously atakuwa age mate wako!
Sasa ulivyom-address na huyo rafiki yako alivyom- address kijana wake wa kazi kwako obviously hakuna uhalisia wowote! Hizi ni story za vil.aza kutungia vil.aza wenzao
Sawa kipanga

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kipanga wa darasa [emoji16]

Elimu n kitu kingine

Maisha Ni kitu kingine.
 
Kipanga wa darasa [emoji16]

Elimu n kitu kingine

Maisha Ni kitu kingine.
Elimu bado haina mbadala maishani.

Hakuna shughuli ya kiuchumi utakayoifanya ambayo haihitaji Elimu.

Hata kwenye KILIMO, UVUVI na UFUGAJI nako kunahitaji Elimu, ndiyo lazma ujifunze (ujielimishe) kuhusu Kilimo, Misimu, Uvunaji, Mbolea, Dawa n.k.

Kufungua BIASHARA yoyote ile lazma pia unahitaji Elimu, ndiyo unahitaji kujifunza (Elimu) kuhusu Je ni Wapi Utapata bidhaa? Ni wapi utaziuza? Faida utapata vipi? Pesa yako utaitunzaje? Biashara utaitangaza vipi? Na Biashara yako utaikuza vipi?

Hata UFUNDI, iwe ni Makenika, Seremala, Umeme, Ujenzi, Ushonaji Nguo, Uchomeleaji na Uungaji Vyuma n.k.

UFUNDI wowote ule lazma pia utulie ujifunze vitu (Elimu) na kisha ndiyo uanze kazi.

Hata MICHEZO, SANAA na BURUDANI, hapa napo hata kama unacho kipaji lakini pia utahitaji kuna vitu ujifunze (Elimu) kisha ndiyo uanze safari yako kutafuta mafanikio.

Na kila kitu kina Elimu yake. Hivyo hakuna mbadala wa Elimu kwa kweli.

Asikudanganye mtu eti kuwa maisha hayahitaji Elimu, huyo mtu ni muongo na pengine hajui ELIMU ni nini.

Wakati mwingine unakuta kabisa mtu ni Msomi kabisa wa Ngazi ya Stashada au Shahada lakini ajabu naye atakuambia eti Maisha hayahitaji Elimu ili ufanikiwe, Huyo Mtu ni Muongo na Hajui ELIMU ni nini.

ELIMU - ni kujifunza na kupata ujuzi au maarifa chanya yenye mantiki ya kitu chochote kile ambacho hukijui katika jambo lolote lile iwe ni Sanaa, Ufundi, Madawa, Tiba, Habari, Mawasiliano, Utamaduni etc.

Hata kabla ya Ukoloni, Afrika elimu zilikuwepo pia, elimu za Ususi, Uhunzi, Uwindaji, Uvuvi, Ujenzi n.k.

Ndiyo lazma kujifunza (elimu) vitu maishani, Elimu haina mbadala.

Ndiyo maana wanasema ELIMU HAINA MWISHO, sababu Elimu ni kujifunza mambo, na hakuna mtu anayejua kila kitu duniani na maishani. Hivyo KUJIFUNZA HAKUNA MWISHO (ELIMU HAINA MWISHO)

Namna Kuu MBILI za kupata Elimu (kujifunza).

• ELIMU (KUJIFUNZA) KUTOKA KWA WATU WENGINE, mfano:- kusoma, kuelekezwa, kufundishwa etc.

• ELIMU (KUJIFUNZA) KUPITIA MTU MWENYEWE (Self taught, Self Learning).
Mfano:- mtu kujifunza na kujifundisha vitu yeye mwenyewe kupitia kuchunguza watu na vitu, na kisha kujaribu mambo.
 
Usianze kumponda eti tu kisa kawa mfanyakazi wa stationary coz huezi jua mambo gani hapo kati alikutana nayo katika maisha. Na story za aina hii wengi mnaozileta ni wale ambao mlikuwa mnafeli darasani na mwishowe mkawa na chuki dhidi ya wale waliokuwa wanafaulu sana. Wewe kama ulikuwa unafeli au uwezo wako ulikuwa wa kawaida kwa kipindi hicho unasoma then na leo hii una maisha mazuri na kazi hupaswi kumkebehi jamaa maana Mungu humpa kila mtu kwa muda wake.
 
Kwanza umesoma Chuo gani?
Na ulisoma kozi ipi?
Na je ulisoma astahada, stashahada au shahada?
Na huyo kipanga wenu wa chuo alikuwa anapiga marks na ma-GPA ya ngapi ngapi?
Tuanzie hapo kwanza...

Anyway kikubwa maishani cha kwanza ni Afya Njema, halafu inafuata mtu uweze kumudu mahitaji manne ya msingi [ chakula, mavazi, malazi na gharama za usafiri (nauli) ].

Mengineyo ni nyongeza... Anything is possible, the situation of being at upstairs or downstairs in economy-wise depends on many other things and not only scoring the high-grades at school..., Pia tukumbuke its not over until it is finally over.


Leo upo Juu, hujui siku zijazo utapatwa na nini, unaweza rudi chini pia. Na msaada ukaupata kwa mtu ambaye unamdharau sasa.
 
Ni maajabu

Aliefeligi shule,kapata hela by accident,ila alivyo na chuki tangu anapitwa zamani,chuki hazijaisha mpaka leo,kamkuta yule aliekuaga anampita anaanza kumcheka na kumdhihaki kuridhisha moyo wake wenye chuki ya milele ili kujifurahisha?

Ulipitwa,records ziko wazi,huwezi badili,ilishapita,you cant change the hands of time ukafute,huwezi...ilishapita na inajulikana alikupita

Sasa umepata pesa,ooh well,enjoy yourself while it lasts maana hakuna garantii huyu ambae hana kitu leo hawezi kua na kitu kesho....

Wewe kuna na vihel leo sio garantii utakua navyo pia kesho....usichekee sanaaa kuridhisha chuki zako kwa aliekupitaga zamani
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Back
Top Bottom