Ushuhuda: Nilichokiona kwenye kikao cha ukoo/familia, bila pesa huthaminiwi


Kuna jamaa mmoja aliwahi kunisimulia kuwa katika familia za Kikurya, kama huna wake wengi, hakuna anayekusikiliza kwenye vikao vya ukoo. Kwa hiyo kwenye vikao hivyo vya ukoo, wewe ukiwa na mke mmoja ukashauri kuwa tujenge nyumba mpya ya ukoo, utasikia wote wanasema kuwa "haya sawa", halafu wanaendelea na mjadala uliopo kama vile wewe hujasema kitu. Sasa akisimama ndugu mwenye wake sita katika kikao hicho hiyo akarudia kusema kuwa itabidi tujenge nyumba mpya ya ukoo, basi utawasikia wote wanasema "hilo kweli hilo ni wazo zuri sana inabidi litekelezwe;" wanasahau kuwa wewe mwenye mke mmoja ndiye uliyekuwa wa kwanza kulitoa.
 
Inategemea na familia Tu na mnaheshimiana vipi na uaminifu wako
Binafsi Mimi palitokea msiba wa moja ya wazazi na kiukweli kiuchumi sikuwa vizuri na Mimi ndo kija mkubwa wa familia walichofanya ndugu zangu ni kunipa kusimamia kila Jambo kiasi kwamba hata fedha za kuendesha mazishi walinikabidhi

Kwenye familia chamsingi ni kuheshimiana na uaminifu ndo Jambo la msingi wakati mwingne watu wenye malengo Sawa huwa wanajaribu kuwatoa watu wasio na malengo yanayo fanana

Wakati wao wanajadiliana jinsi gani watauboresha mji wewe unakuja na mada ya kuuza lazima wakuepuke
 
Mi siku hizi siendaji[emoji23][emoji23][emoji23] na bahati nzuri nashukuru siuliziwi, yaani namshukuru Allah!

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app

Makabila mengine naonaga hata miaka mitano ikipita bila kwenda kwao ni kawaida sana, kwa makabila mengine ni lazima kuudi kila mwaka
 
Kikao cha ukoo (sio cha kifamilia) kuna watu nadhani hata kikao cha ukoo hawakijui humu maana inaweza kupita miaka mitatu hawajarudi makwao wapo mijini tu 😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…