Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Huyu inaonekana alikua ameshakua Murtard adhabu yao ni kifo, naona mateso yali muanza mapema tu kwa hicho kitendo......baba mzazi alikua sahihi kama kweli ulikua Murtadi na mimi siwezi kukutafuta tena.
Dini ni jambo binafsi...kila mtu ana haki ya kuchagua jambo sahihi kwake

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu

Kwa faida, hizi hukmu za kisheria zote tunazozifahamu ambazo zimetajwa kwenye Quran na sunna. Utekelezaji wake unakuwa chini ya kadhi katika dola husika, na wala sio eti kwa kuwa tunafahamu hukmu ya mwizi ni kukatwa mkono basi mtu yeyote akimkamata mwizi amkate mkono, hapana.

Bali kuna mambo ya kuyatazama kabla ya kutekeleza hukmu hiyo, kama vile ushahidi na thamani ya kilichoibwa je kinalingana na kukatwa mkono, na haya yote anayeyatazama ni kadhi.

Na hivyohivyo hukmu nyinginezo, na kunyume na hivyo ni fujo na kujichukulia sheria mkononi, na Uislamu sio dini ya fujo.
Naelewa sheikh wangu kuwa na amani hawa wajinga hawawez kuelewa naamua kufurahishana nao tu hapa maana sina kazi leo nipo nipo tu

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
upitapo ktk moto hutateketea,wala miali ya moto haitakuunguza,utakuwa na dhiki siku kumi,uwe mwaminifu hata kufa...
Hello habari za asubuhi!
Hii story nimewahi kuwasimulia wachache sana.
Ni rahisi kumtia moyo mtu kuwa magumu yatapita, Mungu atakusaidia kipindi uko vizuri na umeshiba. Ila ukipitia kipindi kigumu hata ushauri na courage utasikia kama kelele tu unapigiwa.
Nilihitilafiana na wazazi pamoja na ukoo nzima 2009 kwasababu ya kuingia katika Imani tofauti.
Kwakweli yule baba yangu ana roho mbaya sana, hata sasa hajawahi kunitafuta. Nami natamani kwenda kumsalimia na kumpa msaada lakini msimamo wake ni kwamba niende kwake nikairudie dini yangu ya zamani kitu ambacho Mimi sikiafiki, sitakiafiki na hakitatokea hata kwa kuchinjwa.
Sasa katika maisha ya kuhangahikia ugali pasi na sapoti ya mtu (mzazi, mlezi, ndugu n.k) nikajiendea mgodini. Nikaenda kupiga kibarua kwa siku elfu 7, nilienda Mgodini November , December mgodini pakawa na mapumziko ya sikukuu hivyo watu wote tulipaswa kuondoka mgodini mpaka January.
Nikiwa na pesa kidogo sijui nifanye nini au niende wapi nikaamua niende Mkoa wa Ruvuma Tunduru.
Safari ya kwenda Tunduru nikitokea Nachingwea (Lindi) ikaanza.
Kwakuwa nilitumia Lori Tunduru tulifika siku ya pili . Nimefika Tunduru mchongo niliouendea ukagoma hivyo nikaunga mpaka Songea. Nafika Tunduru mfukoni nina pesa ndogo sana hata elfu 2 haifiki.
Safari ikaendelea barabara chafu maana ni masika. Njaa inauma Lori likisimama naangalia huku na kule kama kuna mwembe nikaangalie maembe.
Njaa ikaongezeka Songea tulifika kwa kuchelewa, Lori lilibeba nazi hivyo sometimes nilipata nazi zilizovunjika zenyewe na kuanza kula.
Tumefika Songea usiku wa saa 4, sina ndugu, Sina hata mia na ni mgeni huko
Am back.
Basi ile sijui niende wapi, nikaanza kuelekea mahali kwenye kelele nikafika stand kuu sasa pale nina njaa plus usingizi.
Nikajichanganya kwa machokoraa wa stand, Mungu awainue huko waliko, wakanipa andazi moja na chai kikombe kimoja.
Niliwashuru sana, pale stand hapakuwa na lounge ya abiria kipindi hicho. Sijui sasa kukoje.
Nikapita mitaani kuzurura kutafuta mahali nilale nikapata mahali pembezoni mwa mji nikalala kwenye shamba la mahindi.
Asubuhi nikashikwa na polisi nikiwa stand na kupewa kesi ya uzururaji, jumla ya watuhumiwa tulikuwa kama 15-20.
Tukiwa korokoroni gari ya super Feo iliyokuwa ikitoka Songea kwenda Dar es salaam ikapata ajali. Sasa mkuu wa kituo akaamuru tubebwe tupelekwe Central halafu wale maaskari wakaatend ajali.
Ile tunapandishwa kwenye gari tukitokea ndani kituoni kuingia kwenye karandinga mmoja mmoja Mimi nikafichwa na wingu la Mungu hawakuniona wakawasha gari wakaondoka . Polisi si chini ya watano wote hawakuniona ilhali nilisimama mbele yao na wengine niliwagusa.
Next day tena nikarudi stand, nikachujua nguo zangu nzuri nikaziweka mkononi na kujigeuza mmachinga. Nilizunguka manispaa yote, Aisee katika kipindi kigumu kila solution hugeuka kuwa ngumu. Nguo nilianza kutangaza nauza kwa elfu 5 , nikashushe bei ikawa elfu 3 na mwishowe nikawa nauza buku buku lakini hata moja sijaiuza.
Siku ikaisha njaa Kali, nikalala nje.
Kila nikijaribu kuomba kazi yoyote hata kulima au kulishia ng'ombe nilikosa. Watu wanasema hawanijui hivyo hawawezi kuniamini.
Hapo nilikuwa nimeibiwa vitu muhimu ikiwemo daftari la namba za simu, I'd ya kupigia kura na I'd ya skuli maana nilikuwa ndo nimetoka kumaliza form four.
Siku moja nikiwa taabani fundi viatu akanisaidia 500 ila suala la kunisaidia makazi ya kulala hakuweza sijui kwanini . Nikifurahi sana nikaanza kuzungukia migahawa nikaupata mmoja nikapewa ubwabwa wa 500 mwingi sana nikala huku nahemea maana nilikuwa nikikuta chocote kitu barabarani changu iwe muhindi, karanga au hata dagaa namla.
Kwa ufupi sasa niko Da es salaam, nimeajiriwa na Kaisari, nina familia yenye furaha na amani, niko kwenye uchumi wa kati.

Am happy.
YESU ni BWANA
 
Ulimwengu wa kiroho wewe mweupe sana.
huna nguvu yoyote
Unataka adi nianze kuwauzia watu maji ya upako, mafuta, chumvi na udongo, au niwe navaa kibaraghashia ndio unione mweusi kiroho.... Endelea kuwa misukule kwenye hizo imani zetu, jikite kwenye meditation na kutumia uwezo wako wa subconscious mind ili unijue vizuri, nakutakia usiku mwema.
 
😂😂😂🤣🤣 haya bhana mimi acha ninyamaze ukweli unao wewe kwenye jicho la tatu unaona mambo gani, is demonic spirit or Angelic spirit utajaza mwenyewe
 
Huyo mungu wao huwa ni kilaza sana yaani sana. Mungu gani hadi atetewe tena kwa mapanga!
Ah samahani mkuu, nilisoma vibaya nikajua unaniambia mungu wangu kilaza mpka apiganiwe na mapanga kumbe ulimaniisha wale wa upande wa pili
 
Ila nilichojifunza hapa ni kuwa Allah ni Rahiim sana(Mwenye huruma) kwa viumbe wake.

Tazama mleta mada pamoja na kuikataa dini pekee, ya haki mbele ya Allah, lakini bado anamruzuku mpaka ameweza kuanzisha uzi hapa akijiona shujaa/ mshindi.
Pamoja na hayo huju jamaa bado haja ridhia anatukana sana uislamu hapa JF katika mada mbalimbali.
 
Samahani mkuu Murtadi ndio nini?? Ni imani ya aina gani??

Ndugu yangu

Kwa faida, hizi hukmu za kisheria zote tunazozifahamu ambazo zimetajwa kwenye Quran na sunna. Utekelezaji wake unakuwa chini ya kadhi katika dola husika, na wala sio eti kwa kuwa tunafahamu hukmu ya mwizi ni kukatwa mkono basi mtu yeyote akimkamata mwizi amkate mkono, hapana.

Bali kuna mambo ya kuyatazama kabla ya kutekeleza hukmu hiyo, kama vile ushahidi na thamani ya kilichoibwa je kinalingana na kukatwa mkono, na haya yote anayeyatazama ni kadhi.

Na hivyohivyo hukmu nyinginezo, na kunyume na hivyo ni fujo na kujichukulia sheria mkononi, na Uislamu sio dini ya fujo.
Kwanini umkate mkono? Wewe hauna dhambi?
 
Ila nilichojifunza hapa ni kuwa Allah ni Rahiim sana(Mwenye huruma) kwa viumbe wake.

Tazama mleta mada pamoja na kuikataa dini pekee, ya haki mbele ya Allah, lakini bado anamruzuku mpaka ameweza kuanzisha uzi hapa akijiona shujaa/ mshindi.
😁😁😁😁😁
Kama ana huruma, unajua angekuwa nchi za waislamu 98% adhabu yake ingekuwa ni kifo?
Kama Allah ana huruma halafu wafuasi wake hawana huruma mpk mnaweka mahakama ya kadhi basi mafundisho ya uislamu hayaendani na mafundisho ya Allah?
Watu waliofanikiwa wakiwa kwenye imani zingine km wachina ni huruma ya Allah?
 
Back
Top Bottom