Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Eeee lazima aende huko maana sasa tutafanyaje kizazi hiki hakitaki huruma .

Vipi lakini wewe uko upande gani ? Ili nijue naongea na ndugu yangu au mmoja wa wanaotakiwa kuuliwa .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Hivi Mungu akitutaka woote kuwa dini moja ili twende Mbinguni nini kinamshinda mpaka atumie vitisho? Kwa nini Mungu ameweka hukumu siku ya mwisho? Mungu wa kweli anatishia watu wasimkimbie, kweli? Ukimkimbia anaamuru uuwawe, kweli?

Ukiona mtu anakulazimisha dili juwa wewe ndo dili lenyewe shtuka.
 
Katika hii story kuna maswali kadhaa labda angetuambia kwa kuwa ni story ambayo yy ameamua kushare na sisi ndugu zake wa JF
1. Alitoka imani gan kwenda imani gan??
2. Sababu zilikuwa nn??
3. Maisha ya mafanikio yake kwa sasa ilikuwaje akatoboa toka kweny hizo changamoto?
4. Anajutia chochote baada ya yy kukorofishana na mzee wake??
 
Ila waislam wengine hua ni wa wapi? Mimi wazazi wangu ni waislam safi. Nilikua muislam ila nilibadilisha dini. Sijawahi kufukuzwa wala kutishiwa kufukuzwa kwetu.

Upendo na ubaguzi hauna dini ni tabia za watu wenye roho nzuri na mbaya respectively. Unambagua mtu utafikiri mbinguni utaenda naye au kama anaenda motoni mtachomwa wote. Kila mtu ataubeba msalaba wa kwake peke yake.
Damu ya Yesu ikufunike na mabalaa yote daima.
 
Mkuu mimi sijawahi kusema hivo nasikia hizo tuhuma tu kwa hao watu ila sijawahi kuhusudia na sina abudi kulitilia maanani kama ni kweli, mimi sina hasira na dini yoyote mimi niko poa kabisa ninacho amini ni utu na ustaarabu wa watu.
Comments zako kwenye huu uzi zimedhihirisha wewe ni dini gani.

Usiogope kujitangaza.
 
Dini ni ya wanadamu tukifika mbele ya hukumu matendo ndo kitu kitakuhukumu....Hilo ni basi tu la kukufikisha safari Yako bhana.....nashangaaa sana anayeshupaza shingo kushindania udini otherwise pole Kwa msoto...huo ndio uanaume....[emoji137][emoji137][emoji137]
 
Kiukweli hata Mimi nimeshawahi kula chakula Cha kwenye dustbin 😭😭😭 maisha yanatufunza mengi sana...wengine tukihangaika hatuna Cha kukila... wengine wanahangaika wapi pa kutupa walivyo vikinai​
 
Muhimu ukikwama ugenini onana na uongozi wa mtaa jieleze wakudhamini kisha nenda nyumba ya mtu au popote muombe mtu akupatie kazi yeyeto hata kwa malipo ya chakula.
Hata hao ni binadam na wana wasiwasi wa kumdhamini mtu wasiyemjua....kwa sasa mambo yameshakuwa mtifuano tunawindana zaidi ya swala na mamba so hakuna wa kukuamini kama huna vielelezo vya kudhibitisha uaminifu wako.
 
Utakufa wewe wa kwanza. Unatishia nani nyau. Mungu gani huyo wa kulazimishana? . Huyo Mungu ingekuta na yeye anafata hizo sheria zake angetuua sisi tulio na imani nyingne kwanza.
Huyo mungu wao huwa ni kilaza sana yaani sana. Mungu gani hadi atetewe tena kwa mapanga!
 
Murtadi adhabu yako ni kifo , hakika utakufa na kifo ni adhabu pekee ninayostahili kukupa tukikutana.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Ndugu yangu

Kwa faida, hizi hukmu za kisheria zote tunazozifahamu ambazo zimetajwa kwenye Quran na sunna. Utekelezaji wake unakuwa chini ya kadhi katika dola husika, na wala sio eti kwa kuwa tunafahamu hukmu ya mwizi ni kukatwa mkono basi mtu yeyote akimkamata mwizi amkate mkono, hapana.

Bali kuna mambo ya kuyatazama kabla ya kutekeleza hukmu hiyo, kama vile ushahidi na thamani ya kilichoibwa je kinalingana na kukatwa mkono, na haya yote anayeyatazama ni kadhi.

Na hivyohivyo hukmu nyinginezo, na kunyume na hivyo ni fujo na kujichukulia sheria mkononi, na Uislamu sio dini ya fujo.
 
Wew Mungu Wangu unamjua ni yupi?? Uliona wapi nimebeba panga namtetea??
Pambana nae boss....muabudu sana tena sana....uzuri ni kuwa kila mtu atajibu mashtaka yake "kama kweli kupo kwa kujibu mashtaka!"
 
Ila nilichojifunza hapa ni kuwa Allah ni Rahiim sana(Mwenye huruma) kwa viumbe wake.

Tazama mleta mada pamoja na kuikataa dini pekee, ya haki mbele ya Allah, lakini bado anamruzuku mpaka ameweza kuanzisha uzi hapa akijiona shujaa/ mshindi.
 
Back
Top Bottom