#COVID19 Ushuhuda wa Mchungaji Godwin Chilewa kuhusu COVID-19: Je, tunamficha nani, kwanini na kwa Faida gani?

#COVID19 Ushuhuda wa Mchungaji Godwin Chilewa kuhusu COVID-19: Je, tunamficha nani, kwanini na kwa Faida gani?

Asante mleta mada someni ni muhimu.
1. Corona ni gonjwa serious, tumuombe Mungu atunusuru.
2. Kila mmoja achukue wajibu binafsi kujilinda na kuwakinga wengine.
3. Kwa kuwa ni garama kubwa tutumie kila tiba asili iliyothibitika,lishe nk.
4. Serikali itimize wajibu wake wa msingi kuwa na mpango dhabiti na sio kukwepa wajibu.
Hapo #4 pana utata. Ilikuwa rahisi sana kwa waliogundua hiyo dawa kuwapa wagonjwa kadhaa wenye umri tofauti tofauti na maendekeo yakafuatiliwa kwa karibu sana na watalaam, halafu baada ya mafanikio tukatangaza. Badala yake wanasiasa wanatangaza dawa na hawasemi wametafiti vipi. Kama kiti kiko bora kwanini pasiwe na uwazi
 
Habari ya nyungu ni upumbavu mkubwa! Kama unaumwa corona, ukitaka hali iwe mbaya zaidi, au uwahi kuondoka, piga nyungu.

Mbunge yule aliyefia Dodoma mwakajana, alijisikia vibaya, akadanganywa na wenzake, jioni akapiga nyungu - hakuna anayejua alifariki saa ngapi, asubuhi walishuhudia maiti.
Utashangaa nyungu iko promoted na watu wenye phD, nchi hii kwa kweli Ina bahati mbaya sana.
 
Ujumbe mzuri, ila hii picha niliiona mwaka jana humu JF kwenye phase 1 ya COVID-19. Je kaugua tena COVID mwaka huu
 
Utashangaa nyungu iko promoted na watu wenye phD, nchi hii kwa kweli Ina bahati mbaya sana
Kuna watu wengi nchi wametumia muda mwingi kukaa darasani, lakini wakatoka wajinga kuliko aliyeishia darasa la 7.

Degree zao zote zilichowasaidia ni kuongea Kiingereza tu, na wengine hata hicho Kiingereza hawakijui.

Watu kama Rais Magufuli, Kabudi, Mahera, Mutungi, Mganga Mkuu, Waziri Gwajima - sioni kama hizo PhD zao zina faida yoyote kwa Taifa. PhD zao wanazitumia zaidi kusema uwongo kuwalaghai watu. Ni afadhali darasa la 7 la Musukuma, kuna wakati linakuwa na faida, kwa sababu kuna wakati anaeleza ukwel wa hali ilivyo.

Sifa ya kwanza ya msomi wa kweli ni kuwa mkweli na kujiamini. Lakini hawa wasomi uchwara wa kwetu ni waongo, wanafiki, waoga - kazi yao kubwa ni kumsifia Rais Magufuli hata anapostahili kukosolewa.
 
Kujiajiri kugumu pamoja na phD hivyo lazima kujitoa ufahamu maisha yaende.Unajua ni namna gani ilivyo hatari kuwa sahihi wakati boss wako akiwa amechemka, kuna mtu hapa kwetu ana kiburi Cha uzima,hata akikosea Jambo huwa harudi nyuma yeye anasonga tu lolote na liwe na atasema Sana uongo na kuwalazimisha wengine kusema uongo kulinda ujinga wake.
 
Endelea tu kukaa huko huko usije tena Tz. Sisi hatutakia lockdown. Tutajenga immunity zetu hivi hivi.
 
Kuna mambo mengine tunamchosha tu Mungu. Mungu ametupa akili na kutupendelea kuwa mfano wake.
Hapa mchungaji kaeleza hali halisi tu.
Tusimsumbue Mungu kwa yetu. Hebu fikiri Simba wanasali na kufunga ili wamfunge Yanga. Na Yanga wansali na kufunga ili wamshinde Simba. Mungu amtamsikiliza yupi na mambo yenu hayo.
Kama Mungu ametupa akili na maarifa na kwa hayo tunaweza kujiponya. Inakuwaje tunakataa kutumia katu katu na badala yake tunapaaza sauti na kurahisisha mambo
Hoja ya mchungaji pia ni kwamba serikali inabeba jukumu gani kitaalamu na kifedha kuwaokoa waathirika wa covid_19.
Kwa nini inatumia njia rahisi kusisitiza nyungu na maombi ambalo kimsingi sio jukumu lake. Serikali hujikita kwenye mipango na rasilimali kutatua matatizo na sio kuhubiri imani. Kazi hiyo ifanywe na watu wa dini.
Huu ni mtizamo wangu.
 
Endelea tu kukaa huko huko usije tena Tz. Sisi hatutakia lockdown. Tutajenga immunity zetu hivi hivi.
Unajenga immunity kwa gharama ya watu wasio na hatia? Je kujenga immunity ndo kunatufanya tuseme uongo kuhusu Corona? Kujenga immunity ndo kunatufanya tusitunze data sahihi ili kutuwezesha kufanya tadhimini kesho kujua Kama njia tuliyochukua was good or no ukilinganisha na njia walizo chagua wengine?
 
Irresponsible government inayoongozwa na irresponsible individuals na inayoonza wajinga huwa ipo hivyo
 
Si kila mtu ni mshirikina kama ww na jiwe. Hata wamarekani wangekufa wote na sisi watanzania asife hata mmoja, ukweli ni kuwa US wana viwango vya juu vya matibabu.
 
Kabla hata sijaendelea mbele wewe ugonjwa umeupatia marekani na siyo Tanzania

Tarehe sita na tarehe 14 ukapata majibu covid hana incubation period fupi hivyo waweza mulaumu lambda vipimo although navyo vimetoka huko huko unakoishi na still vina error kama kawa
 
Back
Top Bottom