Usianike life style yako mtandaoni, binadamu hana tabia ya kusahau, binadamu hasamehi

Ngoja nikwambia,

Mimi nilianza kuingia kwenye internet for the first time 2003....
Kwahiyo kipindi hicho ni ku google na kuangalia pornographics..

Sasa mitandao ilipanza tukaanza kusave majina yetu na picha zetu ... Karibu kila social networks miaka 6-7 baadae.

Wakati tunaanza kaz na kupata connections za maana, nikaona tunaanza kuwa monitored kwenye social media .

Zaidi sana nikaanza kuona hata medem tuliotongoza wana tu google..

Fast forward ni personal profile kwa public.. na security risk..

Ukipata watu wanaokuchukia au wanaokuwinda kukudaka ni sekunde..

Lakini zaidi ni kukwepa uwajibikaji kwa mambo yanayozuilika, na kuonekana moumbavu mbele ya watoto au watu wanaoku perceive tofaut..

Zipo faida nyingi sana za kuwa na maisha ya siri mbali na social media.

Ushauri wangu kama hupati pesa au kutengeneza kipato kupitia hayo achana huko..

Hata wanasiasa na wanamuziki na wafanyabiashara wajanja wanatumia majina na namba za siri kujua kinachoendelea..

Unakuwa na profile yako yenye official names alafu unakuwa na profile zako za kufanya mambo yanayoendana na wewe kwa ndani, the inner you.

Kwa sasa mimi majina yangu na pich zangu hazionekani popote zaidi ya ile media ya wanafiki ya LinkedIn 😂, na Kidoogo Quora .(Wachache sana wanaijua)

The world is brutal...anything can be used against you.

Ahsante
 
Hapo nimekupata🤝
 
Mara nyingi ushamba wa bahadhi ya watu ndo upelekea hayo yote,kujitia much know nk
 
Sijasema nawahukumu au kuna namna najiskia vibaya kwa sababu siamini katika kupangia watu maisha maana kila mtu yupo unique kimuonekano na hata kimtazamo. Ila kiuhalisia ni mbaya sana kuweka kila detail ya maisha yako mtandaoni kwa sababu huwezi jua ni lini itatumika dhidi yako.

Imagine Zamani watu walificha vitu kama kazi, ujauzito au siri za mahusiano ama familia zao. Hii ni kwa sababu watu wasipokujua ni ngumu kukudhuru au kutumia madhaifu yako dhidi yako. Mbaya zaidi ni kuwaweka watoto au family members ambao pengine mitandao sio mambo yao. Kiuhalisia si sawa
 
Umeongea kitu muhimu mno
 
Mara nyingi ushamba wa bahadhi ya watu ndo upelekea hayo yote,kujitia much know nk
Halafu hawapendi kusahihishwa, kukosolewa au kufundishwa/kuelekezwa ambavyo inavyotakiwa iwe.
e.g Umeenda sokoni kununua nyanya. Una mkuta mwuzaji unamwuliza.: Hili fungu la nyanya ni shs. ngapi? Anakujibu: Haya mafungu upande huu ni shs mia tano, hapa ni shs mia mbili na pale mbele ni mia-mia.
Unamsaidia kwa kufafanua: Hili fungu nililosota kidole sh. ngapi? Anakujibu: wee chagua tu hapo fungu ni mia tano-mia tano tuu. Nikupe mafungu mangapi?
Sasa kununua nyanya tu unatumia dk 10 sokoni utaondoka saa ngapi? Kumbe angelisema: Hilo ni shs. mia tano tu - Basi. Uamuzi wa ni mangapi, haumhusu atasikia kwangu.
 
Tusisahaua macho ya husda yapo hamna mtu anataka kuona mwenzake kaendelea
 
Watanzania wengi tunaishi kwa hofu ambayo hatuijui ni nini,
1. Ukianika maisha yako mitandaoni watu watakunyima misaada, kwa nini uishi kwa hofu ya kupata matatizo na kunyimwa misaada? na je hao unaowasema una uhakika gani watakusaidia pindi utakapopata tatizo?
Hakuna mtu atataka kukusaidia ashindwe sababu ya lifestyle ya mitandaoni.

2. Nitanyimwa kazi
Mpaka unanyimwa kazi kulingana na post zako za mitandaoni ni dhahiri huyo mwenye kazi hajakupata kulingana na competence yako, na pia hakuna mwajiri mwenye akili atakunyima kazi kwa hiyo sababu, hapahapa bongo achana na Nairobi watu wana dreadlocks na tatoo mwilini na wameajiriwa kwenye kampuni za maana wanasukuma range ila sisi tumejikita kwenye insecurities za maisha.

Kila mtu aishi maisha inavyompendeza na kama hupendi unaweza usione ndio maana kwenye kila mtandao duniani JAMIIFORUMS.COM ikiwemo kuna ignore/delete/block options, wanaopost hawajawahi kumlazimisha mtu apost ila wasiopost kwa nini mtake wengine wasipost?

Kupost ni furaha, ni kuweka kumbukumbu nzuri, ni motivation kwa vijana wa kisasa katika kufanya makubwa zaidi;
binafsi napenda page za lifestyle Instagram hasa za vijana wa rika langu kwani zinanifanya nijue duniani wanavyoishi maisha na mimi naboresha maisha yangu kila siku.

Half american Leejay49 Infropreneur
 
Sawa kabisa. Siku likikupata la kukupata ndo utawasikia wanafunguka ... na ndo mana wahenga wakaja na msemo huu: "Hujafa hujaumbika" i.e. ukifa watu ndo wanaanza kukuumba: Huyu si ndo aliyekuwa mchepuko wa fulani, huyu alikuwa kibaka wa kutupwa, Madeni yamemsababishia hio Presha ghafla n.k.n.k Wamekuumba.
 
Atleast nimempata mmoja anayejiamini,.

Uzi ungefungwa tu hapa🙌
 
Hapo Nimekupata mkuu🤝
 
Siku moja utahitaji kubadili life style contents zako zitakunyima usingizi📌🔨
 
Uko sawa asilimia Mia,Mimi nakuunga mkono
 
Kuna sababu gani ya kumpost mtoto wako mchanga kwenye mitandao?
Au kula kwako Bata?
Km Ni kupost tupost vitu km biashara ili kupata wateja nk.
Huo ni mtazamo wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…