Watanzania wengi tunaishi kwa hofu ambayo hatuijui ni nini,
1. Ukianika maisha yako mitandaoni watu watakunyima misaada, kwa nini uishi kwa hofu ya kupata matatizo na kunyimwa misaada? na je hao unaowasema una uhakika gani watakusaidia pindi utakapopata tatizo?
Hakuna mtu atataka kukusaidia ashindwe sababu ya lifestyle ya mitandaoni.
2. Nitanyimwa kazi
Mpaka unanyimwa kazi kulingana na post zako za mitandaoni ni dhahiri huyo mwenye kazi hajakupata kulingana na competence yako, na pia hakuna mwajiri mwenye akili atakunyima kazi kwa hiyo sababu, hapahapa bongo achana na Nairobi watu wana dreadlocks na tatoo mwilini na wameajiriwa kwenye kampuni za maana wanasukuma range ila sisi tumejikita kwenye insecurities za maisha.
Kila mtu aishi maisha inavyompendeza na kama hupendi unaweza usione ndio maana kwenye kila mtandao duniani JAMIIFORUMS.COM ikiwemo kuna ignore/delete/block options, wanaopost hawajawahi kumlazimisha mtu apost ila wasiopost kwa nini mtake wengine wasipost?
Kupost ni furaha, ni kuweka kumbukumbu nzuri, ni motivation kwa vijana wa kisasa katika kufanya makubwa zaidi;
binafsi napenda page za lifestyle Instagram hasa za vijana wa rika langu kwani zinanifanya nijue duniani wanavyoishi maisha na mimi naboresha maisha yangu kila siku.
Half american Leejay49 Infropreneur