Usije Dar Es Salaam niagize hasa hasa soko Posta na Kariakoo, kwa uaminifu mkubwa sana

Na wewe ni mwoga mbona hutaki kunitumia mzigo Sasa eti adi nitume hela
Kuna wengine ni waoga sana lakin Kuna wengine wanatuma tu pesa wala hawana hata shida kabisa

Lakini cha ajabu wale waoga ni wale wenye kuhitaji mzigo wa thamani ndogo sana
 
Ndugu yangu toka nibandike hilo bandiko humu ndani nimefanya kazi watu waziozidi 30

Lakin kati hao kama yupo ambaye nimemzurumu bas alete ushuhuda
Hii unaongea tu, huwezi fanya biashara kienyeji Kama vile ni ndugu zako wanakutuma. Mbona mie hutaki kunitumia mzigo na hutodhulumiwa unacheza na akili za watu ili uonekane, watu wanakupa challenge za kukusaidia ukue
 
Pambana na uzidi kuwa muaminifu
Nina kijana mmoja nilitambulishwa ni muaminifu sana, amejenga jina lake na kulikuza
Nimemtumia sana sana
Anatia huruma maana wanaomtumia wengine hawampi cha ziada
Wamemfanya kama ndugu yao
Ila na wewe uwe muwazi kwa bidhaa unazotumwa kwa bei zake
Ukipandisha cha juu ipo siku utaumbuka tu maana wafanyabiashara wanapeana habari
Weka bayana kila kitu
Mzigo kiasi fulani, usafiri kiasi fulani na wewe unakula ngapi simple
 
Hii unaongea tu, huwezi fanya biashara kienyeji Kama vile ni ndugu zako wanakutuma. Mbona mie hutaki kunitumia mzigo na hutodhulumiwa unacheza na akili za watu ili uonekane, watu wanakupa challenge za kukusaidia ukue
Anaogopa kudhulumiwa,kwanini wewe usimtumie pesa?
 
Anaogopa kudhulumiwa,kwanini wewe usimtumie pesa?
Hilo swali na yeye muulize ama kama ndio jibu unadhani kuwa namie Niko tofauti Naye, yaani anadhani ni kienyeji tu mtu anatumiwa hela kisa kuweka namba na kutaja jina la yesu uwahadae watu wawe wajinga kwa kuwarubuni, hata hao watu 30 anasema hawapo ni zuga tu kucheza na akili yako ili ufanye biashara na uaminifu, Mana hajajibu swali, akikimbia,akifa, akiugua hela yako ndio utaanza kuambiwa ndugu nisamehe , yaani watu ulimwengu wa sasa wanafanya biashara kizamani.
Jiulize y mtu anatumia mabilioni china na mzigo analetewa
 
Hili lilikuwa jaribio la kukupima uungwana na ustaarabu wako. Umeishia kutukana na kuiharibu haiba yako. Muungwana hujibu kwa upole hata anapochokozwa au kuonewa
Akampime mumewe sio mimi,
JF unahangaika kupima watu ili iweje?
 
Dogo nitumie mzigo basi mie ni muaminifu mbona wengi mno wameshanitumiaga mzigo na ukifika ndio nalipa hela, mie sidhulumu mtu.
Ama niweke namba yangu hapa ili uzidi kuniamini.
Mie kwanza naogopa kutenda dhambi
 
Hii ili uaminike uwe na ofisi physical maana watu wa Daslam hamuaminiki kabisa
 
Blaza maelezo hayajajitosheleza..ntaamini vipi wewe sio tapeli..toa kitambulisho chako Cha nida na certification ya kuwa verified
 
Binti umehamia huku? Mbona unahangaika kiasi hicho?

Nilikua sijui kua kumbe hii ndio ID yako nyingine.
Kua❌
Kuwa✅

Mi nikishaona tu mtu hajui kutofautisha maneno mepesi kama hayo naona hapa hamna mwanamke na mawasiliano nakata. Maana utanichosha kukuelekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…