Usimpigie magoti mwanamke unapomvalisha pete

Demi Kwanini ukumbini wakati bibi harusi anawapelekea keki wakwe zake anapiga magoti? Je, ushawahi kuona mwanaume akifanya hivyo?

Mila ya wanawake kuwapigia magoti waume zao ni kuonyesha kutii mamlaka ya kichwa cha familia! Ila kwenu mafeminist mtapinga maana kwenu Hakuna kichwa cha familia. Kuna vichwa viwili 😀
 
Sijakataa kwamba kupiga goti ni kuonyesha utii. Pia ni kwa baadhi ya mila ndo ipo hivyo..
Kwa sisi wachaga hakuna mahali mwanamke anapiga goti...na wala haifundishwi hivyo.
Unakabidhi cake huku umesimama kama mlingoti😅.

Nilichotaka kusema ni kwamba, tuache kuiga mila za wazungu halafu tunakuja kulumbana wenyewe kwamba sio sawa. Kwao ni sawa na tuache iwe hivyo. Sisi tufanye ya kwetu kama mila zetu zinavyosema.
 
Nimeona wachaga kadhaa wakipiga magoti, huwa najiuliza kwanini wanafake 😀😀😀ili waonekane wema mbele ya ukumbi au?

Ila ukumbi kibongobongo ukitoa keki umesimama Kama mlingoti, 😀😀😀😀@demi usifurahishe ukumbi
 
Huwaga nachukia hichi kitendo hadi mwili huwa unasisimka naona aibu nikiona dume zima limechchuchuma eti linamvisha Pete mwanamke, huwa natama nikamnase kibao, yaani hichi kizazi cha Gen-z bwana daaah!
Mimi nilishawahi kuondoka kwenye party ya engagement baada ya kuona jamaa kapiga goti. Sikuweza kuendelea kuwepo pale maana niliona wanaume tumedhalilishwa
 
Waafrika hatuna utamaduni wa kupiga goti wakati wa kuvishana pete. Iwe kwa mwanume au mwanamke. Huo sio utamaduni wetu. Kila mila ina utaratibu wake wa jinsi ya kuchumbia.
Tatizo letu kuiga tamaduni za watu..
Mambo ya engagement sio utamaduni wetu sisi waafrika tunatuma mshenga barua ikikubaliwa unapewa list ya mahari ila hata ikitokea mmekubaliana kuvalishana pete it makes sense mwanamke kupiga goti ila sio mwanaume.
 
Mambo ya engagement sio utamaduni wetu sisi waafrika tunatuma mshenga barua ikikubaliwa unapewa list ya mahari ila hata ikitokea mmekubaliana kuvalishana pete it makes sense mwanamke kupiga goti ila sio mwanaume.
Mambo ya kuvishana pete sio ya kwetu. Tuachane nayo..
Kama wamasai mdada anavalishwa bangili
 
Wanaiga tu hao. Hakuna utaratibu wa kupiga goti popote pale...
Kitu mlingoti
 
Kweli kabisa.. mie nilipiga goti.. sasa hivi nakoma
 
Kamata masikio ilikua Mikono lazma uipitushe kwa nyuma shughuli yake kiuno kipande juu aloooooh apo kuna fimbo itapita🤣🤣🤣
Yaani maumivu ya fimbo za hapo unayasikilizia puani huyu yakipanda kwa kasi kwenda kwenye ubongo wa mbele.
 
Ni kweli lakini ikitokea exception basi mwanamke ndie apige goti
Hayo ni makubaliano baina yako na mchumba wako. Nyie ndo mnaaamua mtumie style ipi.
Wanaume walioamua kupiga goti acha waendelee...maana wenye utamaduni wao anayepiga goti ni mwanaume.
 
Mwanaume anayepiga magoti huyo hana sifa ya "uanaume"
 
Hayo ni makubaliano baina yako na mchumba wako. Nyie ndo mnaaamua mtumie style ipi.
Wanaume walioamua kupiga goti acha waendelee...maana wenye utamaduni wao anayepiga goti ni mwanaume.
Hakuna makubaliano kwenye suala la utiifu, from the first place mwanamke ndie anatakiwa kuwa submissive kwa mwanaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…