Usimshauri ndugu au rafiki asomee uandishi wa habari: ni sekta ambayo inaenda kufa na atateseka sana

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Kuna mdau humu ameposti juu ya changamoto zinazowakumba waandishi wa Azam Mikoani eti wameshushiwa ujira kutokea tshs 500,000 mpaka 300,000 kwanza nikagutuka kwamba wanalalamika kwa kulipwa 300,000?!!

Kama Azam waandishi mikoani wanalipwa 300,000 basi ITV hali ikoje? Je, hizi media ndogondogo za dini mambo yakoje? Kusema kweli hamna tasnia inazaa watu wenye "low self esteem" kama journalism maana ili waishi ni lazima walambe miguu ya watu wengi ili maisha yaende; mnaonaga vile vipaza sauti (mic) vinavyojaa katika press conference za kina Haji Manara na Mwijaku? Basi usishangae kila "mwandishi" aliyetokea kapoteza siku nzima ili akapewe tshs 10,000 tu siku iende

Kwa wanawake hali ndio mbaya zaidi katika kutafuta namna ya kujiongezea kipato

Pia soma:DOKEZO - Waandishi wa Habari Azam wanataabika Mikoani, wanahitaji msaada kulipwa stahiki zao
 
Kuna mdau humu ameposti juu ya changamoto zinazowakumba waandishi wa Azam Mikoani eti wameshushiwa ujira kutokea tshs 500,000 mpaka 300,000 kwanza nikagutuka kwamba wanalalamika kwa kulipwa 300,000?!!
Kama Azam waandishi mikoani wanalipwa 300,000 basi ITV hali ikoje? Je hizi media ndogondogo za dini mambo yakoje? Kusema kweli hamna tasnia inazaa watu wenye "low self esteem" kama journalism maana ili waishi ni lazima walambe miguu ya watu wengi ili maisha yaende; mnaonaga vile vipaza sauti (mic) vinavyojaa katika press conference za kina Haji Manara na Mwijaku? Basi usishangae kila "mwandishi" aliyetokea kapoteza siku nzima ili akapewe tshs 10,000 tu siku iende
Kwa wanawake hali ndio mbaya zaidi katika kutafuta namna ya kujiongezea kipato
Ni kweli ulichoandika,shida kubwa ili vyombo hivyo vifanye kazi ni lazima wapate matangazo ambayo siku hizi hakuna
 
Upo sahihi.

Media zinatarajia zijiendeshe kwa matangazo.

Teknolojia iko advanced siku hizi tangazo linaweza kuwafikia watu wengi Tz nzima ukiliweka FB, Insta, X, Reddit. Ukilisponsor hilo tangazo Litamfikia aliye kazini, nyumbani, gesti, shambani wakati kwa traditional media litamfikia akiwa amewasha hiyo redio au TV na siyo muda wote.

So media nyingi zitakufa kwa sababu hakuna ambaye amesolve utata wa kipato kingine kitatoka wapi.
 
Kuna mdau humu ameposti juu ya changamoto zinazowakumba waandishi wa Azam Mikoani eti wameshushiwa ujira kutokea tshs 500,000 mpaka 300,000 kwanza nikagutuka kwamba wanalalamika kwa kulipwa 300,000?!!

Kama Azam waandishi mikoani wanalipwa 300,000 basi ITV hali ikoje? Je hizi media ndogondogo za dini mambo yakoje? Kusema kweli hamna tasnia inazaa watu wenye "low self esteem" kama journalism maana ili waishi ni lazima walambe miguu ya watu wengi ili maisha yaende; mnaonaga vile vipaza sauti (mic) vinavyojaa katika press conference za kina Haji Manara na Mwijaku? Basi usishangae kila "mwandishi" aliyetokea kapoteza siku nzima ili akapewe tshs 10,000 tu siku iende

Kwa wanawake hali ndio mbaya zaidi maana wengi wao inabidi watumie "uke" ili kujiongezea kipato

Hakuna sector inayokufa, ni utendaji na uniqueness matters!
 
Unajua kwa hapa Bongo uandishi wa habari umekuwa ni tasnia inayofanywa na watu waliofeli kidato (form four au form six) na hii ni tofauti na nchi nyingine kama Marekani ambazo ili mtu uwe mwandishi wa habari itakubidi uwe na shahada ya kwanza ya chuo kikuu.

Matokeo yake ni nini? kwasababu waandishi wengi wa Tanzania wamekosa elimu, inakuwa ni ngumu kwa wao kuweza kuja na habari za kiuchunguzi za manufaa kwa jamii na badala yake wamekuwa wanakuja na habari nyepesi nyepesi ambazo mtu yeyote anaweza kuzipata hata kwa wapita njia.

So, kulipwa kidogo ni reflection ya wanachokizalisha. Ila Trust me, ikitokea mtu akawa mwandishi mzuri wa habari mwenye uwezo wa kuja na habari za kiuchunguzi, malipo bado ni makubwa sana sana kwenye hiyo fani
 
Hakuna sector inayokufa, ni utendaji na uniqueness matters!
Traditional/legacy media inakufa; ukiondoa upande wa michezo sioni kama kuna eneo ambalo huu uhalisia unaenda kubadilika
Azam yenyewe iko afloat mostly kwasababu ya tamthilia, ITV wanajiita super brand kwasababu ya taarifa ya habari ambayo kusema kweli kwa hali inavyoendelea unaweza ukalinganisha na chui wa karatasi
 
Shida kubwa ya waandishi wa habari wa Tanzania,walio wengi hawajitambui nafasi Yao katika jamii.

Kila mwandishi anakimbilia kutoa habari za yellow stories (michezo,udaku nk),Leo hii kupata investigative stories au investigative journalism ni kipengele kigumu sana.
Pia ujio wa citizen journalism ni Kilio Cha media nyingi hapa nchini.Na iwe wazi kwamba moyo wa media house yoyote ni matangazo bila matangazo ni ngumu sana kuendesha shughuli za uandishi wa habari.
Kama ni kweli Azam media wanalipa kiasi hicho Cha mshahara,basi nachelea kusema tuna safari ndefu ya uhuru wa vyombo vya habari nchini.
 
Yellow journalism ni janga la taifa
 
Kuna mdau humu ameposti juu ya changamoto zinazowakumba waandishi wa Azam Mikoani eti wameshushiwa ujira kutokea tshs 500,000 mpaka 300,000 kwanza nikagutuka kwamba wanalalamika kwa kulipwa 300,000?!!

Kama Azam waandishi mikoani wanalipwa 300,000 basi ITV hali ikoje? Je hizi media ndogondogo za dini mambo yakoje? Kusema kweli hamna tasnia inazaa watu wenye "low self esteem" kama journalism maana ili waishi ni lazima walambe miguu ya watu wengi ili maisha yaende; mnaonaga vile vipaza sauti (mic) vinavyojaa katika press conference za kina Haji Manara na Mwijaku? Basi usishangae kila "mwandishi" aliyetokea kapoteza siku nzima ili akapewe tshs 10,000 tu siku iende

Kwa wanawake hali ndio mbaya zaidi katika kutafuta namna ya kujiongezea kipato
acha kukatisha watu tamaa kwa kufeli kwako kupata na kufanya kazi kwenye fani au ujuzi uliosomea.

kijana awaye yeyote.
Nenda shule, na usome kwa bidii ufaulu vizuri, full stop.🐒
 
Back
Top Bottom