Ni ngumu kunielewa ukilitazama hili swala kwa jicho la kujihami ila ukitoka huko mtaani hautatumia nguvu nyingi kuona ninachokwambia. Okay nitakupa mwanga kidogo.
Wanawake ndio wanaongoza katika kuwafanya watoto wao nao wawe single mothers sababu ndicho kitu wamekua nacho na ndicho wanakielewa. Anaweza tamani mtoto awe na baba wa kumjali ila nikuulize swali, kuna baba wa kumjali mtoto bila mama ambaye ni wife material kwa mumewe?
Ili baba bora wa watoto apatikane ni lazima mama mtoto awe alikulia makuzi ya kumuandaa kuwa mke bora na partner mzuri kwa mwanaume wake, akifanikiwa hilo ni rahisi kuvutia mwanaume bora wa kuwa baba wa familia na kwa watoto. Sasa is that the case kwa mabinti ambao wamezaliwa familia ambazo mama ni Barmaid, mdangaji, hajatulia, aliyezaa before marriage etc?
Turudi kwa wanaume. Mfano wewe na hayo machungu uliyo nayo juu ya malezi ya watoto unaotamani kuwa nao ili ujenge familia bora ila unasahau kwamba wewe huwezi kuwa baba bora na kujenga familia ya Baba, mama na watoto kama hauna kaliba ya kiume ya kuvutia wanawake wenye makuzi na malezi ya kuwa mke imara. Mwanamke mwenye kaliba ya kike huwa anakwenda na mwanaume imara ambaye anazimudu changamoto za maisha, hisia za mwanamke wake, anaweza kuwa kiongozi, anaweza kuwa mfariji, anaweza kumudu mahusiano of which hizi sifa ni nadra uzikute kwa mtoto wa kiume aliyelelewa na mama yake tu bila baba sababu wengi ndani ya mioyo yao mama ndio first priority kabla ya mke.
Unaona Diamond platinum ingawa ana pesa na uwezo ila ana struggle kusettle na kutengeneza familia ya mke m'moja na watoto wake anazaa tu hovyo but yupo karibu zaidi na mama yake. Hii sio udhaifu kwa upande wake ni life style ya kulelewa na mama tu, but je kwako ipo sawa?
Kimsingi unachotakiwa kufahamu ni kuwa mtu anayezaliwa na kulelewa na mama tu au baba tu huwa inampa wakati mgumu sana kublend na wale waliolelewa ndani ya ndoa takatifu na kuishi kwa misingi ya kuheshimu na kutumikia ndoa.
Ataweza kuwa huru na kujiona binadamu katika maisha ya kuishi na watu baki wasioendana na mfumo wa Ndoa au ambao wanaishi nje ya mfumo wa ndoa hapo atakuwa normal ila akiingia huku kwenye ndoa itataka jitihada binafsi sana kuweza kucope na mazingira.