Usiombe kuacha kazi kisa Forex. Nilivyofilisika na kukimbilia kijijini Tabora

Usiombe kuacha kazi kisa Forex. Nilivyofilisika na kukimbilia kijijini Tabora

hii forex imefilisi watu kadhaa wa karibu ninaowajua
kuna rafiki yangu, hatuna mazoea kivile, ni civil engineer, aliniomba sh. 5000

aisee, nilistuka, nikamwambia unamaanisha sh. 500k
akasema hapana , ni sh. 5k bro

baadaye nikapata info kwamba alikua mdau wa forex
Forex fanya for fun upate ela ya kula Bata na bby

Yani Ile ela uliyo ipanga ukale weekend na mchuchu ndo iweke huko ikiliwa furesh tu
 
Haukumshauri arelease dopamine Ili kupoteza mawazo?😂
 
Unanishaurije mimi ninayetaka kuanza? 😊
Usianze, the markets are 100% rigged, ukishakubaliana na hilo pamoja na uncertainties zake zama tu.

Ila kama we mwoga, zama kwenye Newyork stock exchange ama Dar Es Salaam stock exchange, tafuta stocks zinazofanya vizuri kwa Sasa although kwa Newyork kule wako bearish kinyama so nahisi mpaka December.
 
Ndo tunawaza hapa tuzike au tusafirishe[emoji18][emoji18][emoji18]
Kuleni tu hizo. Ila kama hamuitegemei na mpo tayari kuipoteza, na kama una plan nzuri basi wekezeni ila nitaendelea kuambia, market ina uncertainties, so hakikisha una experience. Experience ndo inawafanya novice traders wadumu sokoni muda mrefu .

Wish you good luck.
 
Forex fanya for fun upate ela ya kula Bata na bby

Yani Ile ela uliyo ipanga ukale weekend na mchuchu ndo iweke huko ikiliwa furesh tu
Kuna watu inawaendesha maisha yao.
Kuna watu wamekuwa mabilionea na mamilionea kupitia forex trading, wakina Paul Tudor Jones, George Soros, Kathy Lien, Jesse Livermore (R.I.P) na Dr. David Paul(R.I.P)
 
Na ukaamua kabisa kujiita Mrforex, anyway hongera kwa uthubutu.
Nilikuwa nimechoka na maisha ya kufanya kazi saa nane kwa siku katika ofisi flani hivi pale posta jijini Dar es Salaam. Ndoto yangu ilikuwa kubwa zaidi kuliko kiti changu cha ofisini na mshahara wangu wa kila mwezi. Nilikuwa na hamu kubwa ya kujaribu kitu kipya, kitu ambacho kingenipa uhuru wa kifedha na fursa za kutimiza ndoto zangu.

Nilitambua kwamba kwenye ulimwengu huu wa kisasa, forex ilikuwa njia inayopendelewa zaidi ya kuwekeza na kupata faida kubwa. Nilivutiwa na hadithi za watu waliojikomboa kutoka kwenye mikono ya ajira na kuwa mabosi wa maisha yao wenyewe kupitia biashara ya forex. Hivyo basi, niliamua kuwa mmoja wao.

Nilipofikiria juu ya kuacha kazi yangu na kujitosa kwenye ulimwengu wa forex, moyo wangu ulijaa msisimko na wasiwasi. Nilisoma vitabu vingi na kujiandaa kwa miezi kadhaa kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho. Nikaamua kuwa huu ndio wakati wangu wa kujaribu kitu kipya, wa kujiletea mabadiliko kwenye maisha yangu.

Kuacha kazi haikuwa uamuzi rahisi, lakini nilihisi kwamba huu ndio wakati sahihi wa kujitolea kwenye safari ya forex. Nilijiandaa kihisia na kifedha, nikiwa na matumaini kwamba ningeweza kugeuza ndoto zangu kuwa ukweli. Niliamua kufungua akaunti yangu ya forex na kutumia akiba yangu kama mtaji wa kuanzia. Safari yangu ya kuelekea uhuru wa kifedha ilikuwa imeanza.

Husikose sehemu inayofuata ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu, labda unabahati upande uo, ila kama unakazi usiache kisa hiyo kitu
Financial markets sio suala la bahati, ni suala la kwamba, je unajua market drivers? Je unajua impacts za world events na geopolitical agendas?

Mfano Vita tu ya Hamas-Israel, imepunguza demand ya dollar na kuleta afueni kwa sarafu zingine na physical gold.

Forex sio kuchora chora madude, michoro yako haimove soko.
 
Usianze, the markets are 100% rigged, ukishakubaliana na hilo pamoja na uncertainties zake zama tu.

Ila kama we mwoga, zama kwenye Newyork stock exchange ama Dar Es Salaam stock exchange, tafuta stocks zinazofanya vizuri kwa Sasa although kwa Newyork kule wako bearish kinyama so nahisi mpaka December.
Naomba ABCD za new York stock exchange mkuu.
 
Naomba ABCD za new York stock exchange mkuu.
Newyork stock exchange ni Pana. Unafanya investment ya kununua hisa za makampuni kama Tesla, Facebook, Twitter, Netflix, Amazon n.k.

Unanunua hisa hizo na kuziacha zimove muda mrefu, uzuri wa Newyork stock exchange kuna liquidity na volatility, wanaoweka pesa na kuziuza ni wengi ukilinganisha na Dar Es Salaam stock exchange so ikitoka habari za earnings, inamove kwa kiasi kikubwa. Ili uwekeze unahitaji upate broker au wakala.

Pia unaweza wekeza pesa zako kupitia bonds(hatifungani), kuna UTT na hata CRDB wanayo Kijani Bonds na returns unapokea Kila mwaka. Mwaka huu ndo ulikuwa mwaka bora wa kununua hatifungani kutokana na kushuka kwa shilingi ya Kitanzania.

Pia unaweza wekeza kupitia Dar Es Salaam stock exchange, kampuni ya NMB chini ya C.E.O mwanamke amekuwa akileta positive returns kila mwaka, unaweza wekeza NMB. Ili uwekeze unahitaji upate broker au wakala.
 
Back
Top Bottom