Usipende kununua magari yaliyotumika Tanzania

Asilimia sio ishu, mtu gari si unakagua. Shida yetu tunapenda kitonga mtu hela hana anafosi kununua gari flani.

Gari zinajulikana vimeo na gari kweli, gari nyingi za namba mpya unakuta bado nzima tu provided ziko kwa watunzaji.

Unakuta mtu anataka Crown Athlete ila ana million 7. Gari hio ili uipate yenye viwango unaipata kwa 13.5M ila mtu anang'ang'ana mwishowe unauziwa gari namba DE huko gari imesajiliwa 2015 bongo miaka 7 nyuma mtu aliingiza mjini kashaifuja na kuiuza imeuzwa zaidi ya mara moja wewe unakuja kuveshwa gari imechoka ina poor economy ya wese ila alimradi una wenge na 👑 Athlete.
 
Wakati mwingine kama hujawah kuagiza gari nje ya nchi utulie ufatilie wazoefu wanasemaje ,siyo kujifanya mjuaji Ili uonekane tu na ww unajua.


Mtu unamuuliza swali kama umewah kuagiza gari nje ya nchi ulilipia Hilo gar kwa njia gan!? Anajibu et nilituma kwa M-pesa

Hebu tuwe wa ungwana hata kidogo

Najua badiko hili huenda likawahalibia watu biashara zao lakin angalia na upande wa pili watu wanaumizwa sana na magari yaliyotumika ndan ya nchi hii.
 
Mmh kwenye magari nitapunguza ujuaji. Ila gari ya bei hiyo mkononi sichukui. Hiyo ni personal interest japo wengi wanafanya
Sawa mkuu, inategemea na value na uhitaji. Huwezi pata gari ya juu kwa less than 15M hasa hizi unazoona Harrier, Vanguard, Prado na Toyota wenzao. Labda uuziwe VW Touareg mbovu, au Nissan wakawaka aka Dualis. Xtrail na vimeo vengine.
Mmh kwenye magari nitapunguza ujuaji. Ila gari ya bei hiyo mkononi sichukui. Hiyo ni personal interest japo wengi wanafanya
Sawa mkuu, inategemea na value na uhitaji. Huwezi pata gari ya juu kwa less than 15M hasa hizi unazoona Harrier, Vanguard, Prado na Toyota wenzao. Labda uuziwe VW Touareg mbovu, au Nissan wakawaka aka Dualis. Xtrail na vimeo vengine.
 
Milioni 6.7 mpaka bandarini. Ukilipa na ushuru ni 12 to 13m hilo.
Kiufupi sikuhizi ushuru ni uwezo wa kulinunua hilo gari mara 2! Kama bei ya kulifikisha bandarini ni 6M basi andaa 6M ingine ya wakulungwa pale TRA.
 
Hahahahahah jamaa kauziwa corrolla ltd ya 1.8M imemtesa anakuja kusumbua watu humu na story za kutunga 🤣🤣🤣!
 
Hahahahah Carina iliokaza ni 7.5M sasa wewe ununue gari 3M si unatafuta balaa.
 
Hiyo gharama ya ushuru ambayo mtu anaiona kubwa anakuja kufidia kwenye gharama za kurekebisha hiyo gari. Na mimi nilishajiaminisha kuliko kununua gari used kutoka mkononi kwa mtu kwa zaidi ya millioni 15 bora uagize japan.
Hahah sawa kama una 15M ya ziada agiza. Watu sio machizi kununua gari za mkononi unakuta mtu mkono haufiki huko. Chukulia una budget ya 18M ila unataka gari unakuta unatakiwa 35M.

The same car ilioko registered bongo ni 18M unaenda kubadili kadi tu kwa gharama isiozidi laki 5. Iko in good shape well maintained na namba sio ya zamani lets say ni less than 2 years toka isajiliwe na unataka gari utaiacha kweli?
 
Sijakubishia ila kuibahatisha hiyo nzima ndo changamoto. Kuna mtu kanunua gari juzi ambayo used japan ni 32 yeye aliibahatisha bongo kwa 18. Ni kubwa ila sasa hadi anaanza kuitumia kagharamikia zaidi ya milioni 7. Mambo ni mengi ila nnayokumbuka ni steering rack kanunua mpya, gear box ilikua na kipengele, pump ya mafuta iliwakomesha na hapo alikua na fundi wake kabisa waliikagua wote. Hapo sijasemea vile vitu alivyokua anataka yeye kama seat cover mpya maana za mwanzo zilikua sio nzuri, rangi kapaka nyingine. Tairi za mbele. Yani ndugu yangu kwa nliyoyaona sijaona wa kuni convince. Ndo maana bado nasisitiza.. MIMI yaani MIMI. Gari ikizidi 15 m siichukui mkononi kwa mtu. Sijasema hazifai nimesema MIMIIII SICHUKUI😅
 
🤣 Mimi pia sichukui ila wapo wanaozichukua. Bila shaka hio ni tako la nyani iliomfunza adabu🤣🤣🤣! Ntajie namba ya usajili ni D ipi? DE au DX?
 
🤣 Mimi pia sichukui ila wapo wanaozichukua. Bila shaka hio ni tako la nyani 🤣🤣🤣
Wapi ndugu yanguu😂sio tako la nyani nikiitaja hapa lazima wahusika wata connect dots ila eee nikasema tu yale yale. Magari haya ni changamoto. Uzuri aliekua analitaka kalipata na kafurahia wala hajalalamika gharama nikaishia kukaa kimya tu😅
 
Fundi kamchomesha itakuwa alilambishwa asali. 🤣🤣🤣, Hio gari haiwezi kuwa ya namba za mwishoni mwa D!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…