LGE2024 Usipojiandikisha na usipopiga kura, hutakuwa na haki hata ya kusema nimeibiwa kura

LGE2024 Usipojiandikisha na usipopiga kura, hutakuwa na haki hata ya kusema nimeibiwa kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Yaani hukujiandikisha na hukupiga kura halafu ulalamike umeibiwa, ukiulizwa unajibu umeibiwa kura,
Wakiitafuta hiyo kura yako hata hawaioni,

Tuacheni dharau, twendeni tujiandikishe ili tuwe na pa kuanzia, vinginevyo tukae kimya sasa na hata baada ya uchaguzi
Ni uchaguzi wa kipuuzi kama upuuzi mwingine. Suala la kuwa kura zinaibiwa wala halina mjadala, na hakuna mtu anayejitambua atajitokeza kushiriki huo uchaguzi wa kihuni.
 
Kwani ukisema nimeibiwa kura itasaidia nini? nyie ibeni tu mbona kama mnajiogopa wenyewe
Yameanza kuwa na wasiwasi yana ogopa vivuli vyao.

Wao waibe tu kama miaka yote wafanyavyo waache makelele kupigia watu kujiandikisha katika hilo daftari la wajinga
 
Yaani hukujiandikisha na hukupiga kura halafu ulalamike umeibiwa, ukiulizwa unajibu umeibiwa kura,
Wakiitafuta hiyo kura yako hata hawaioni,

Tuacheni dharau, twendeni tujiandikishe ili tuwe na pa kuanzia, vinginevyo tukae kimya sasa na hata baada ya uchaguzi
Lisikieni hili taira
 
Back
Top Bottom