Usipojua unachokitafuta utaendelea kusema siku yako bado kumbe ilikuja lakini hukuijua mkapishana

Usipojua unachokitafuta utaendelea kusema siku yako bado kumbe ilikuja lakini hukuijua mkapishana

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
471
Reaction score
1,217
Nguvu nyingi wekeza kwenye kujua unataka nini ili usiendelee kusumbuka na kila chaguo linalopita mbele yako kwa sababu unaweza kusema hujaona chaguo lako kumbe tayari lilikuja ukapishana nalo kwa kutolijua.

Wengi tunawekeza nguvu nyingi kwenye kutafuta lakini hatujui tunachokitafuta kikoje ndio maana malalamiko yamekuwa mengi ila ukimuuliza mtu hasa unataka nini ? Hajui


Zipo namna nyingi za kujua kipi unakitaka ila moja wapo ni kujua AINA YA SAFARI YAKO IKOJE

Kama safari yako ni ya kupaa angani jenga urafiki na watu wenye mabawa usisumbuke na wasio na Mbawa watakuchelewesha hao.

Ili kuepuka kuzurura hapa Duniani ni muhimu kujua AINA YAKO YA SAFARI ILI IKUSAIDIE KUJUA UNAVYOVITAKA NI VIPI

#Mwanasayansi Saul Kalivubha.
#Fikia Ndoto Zako.
 
Anaeshauri nijenge nyumba ya bati yeye ana tembe nyumbani kwake.
Ungesema tu kuwa wewe ni mganga wa kienyeji tujae ktk pm yako.
 
Back
Top Bottom