Usipokuwa makini unaweza kujikuta unamhonga mtu anayekuzidi kipato!

Hahaaaa sawa mimi nawashtua wavuja jasho wenzangu
Eleweka mkuu narudia tena eleweka kwenye uzi umeandika unapenda kuhonga sasa hao wavuja jasho wanakuhusu nn tena sisi wenye vipato vya chini kabisa ndio tunahonga sana kama hujui. Unapoteza muda kuwastua swala la mapenzi linamshika kila mtu kwa namna yake
 
Napenda kuhonga wanaonizidi uwezo na kipato ili niwainua hapa na pale
 
sasa kama unahonga kila mwanamke unaekuana nae we si zuzu😂

yaani unajijua umefulia na hutulii
 
hata mwanamke awe katili vipi lazima atakuheshimu tu .bora useme wewe
 
Nakataa huo mstari kuwa eti hata Uhonge kiasi gani huwezi kufirisika, huo ni UONGO.

Ukiendekeza kuhonga lazima ufulie.

Niliwahi kusoma miaka ya Nyuma Ubuyu wa marehemu warumi kuwa kuna mrembo alikuwa analalamika tajiri Mo Dewji kumhonga shilingi laki 1 moja badala ya kumuhonga milioni milioni

Alikuwa anasema yaani Mo akijitahidi sana Kuhonga Basi ni 120k

Kama Mo anahonga 120k Mimi Mkulima ndiyo nitaweza kweli?🤪
 
Kweli ndio Uchimbe Mawe mwenzako akalie Ice Cream Mlimani? Utakuwa huna akili.
Swali la Kwanza kujiuliza ni kwanini uhonge? Halafu ushakutana na anayeenda kuhonga ukamkataza akakuelewa? Jasho la mwanaume linaliwa na mwanamke iwe umeoa, una mpenzi au unaenda kununua dada poa
 
Ni ubinafsi, unyonyaji na roho mbaya za wanawake kutaka kuhongwa na wanaume ambao wamewazidi kipato.

Nna mdogo wangu mmoja alipata manzi anafanya kazi kampuni fulani ya kitajiri inashughulika na maswala ya mafuta na usafirishaji. Binti alikuwa muajiriwa hapo, alikutana na dogo akiwa kwenye harakati za utafutaji wa ajira, sasa binti alikuwaga reception ndo dogo kupeleka maombi wakabadilishana mawasiliano kwa updates zaidi. Chit-chat za hapa na pale zikakolea kwa muda kama wa miezi minne mitatu wakaingia penzini.

Dogo akabahatika kupata kibarua bila mkataba ofisini fulani jijini dar... sasa wakiwa wanatoka na yule manzi akawa anashangaa ku-spend kwake ni tofauti na kipato cha dogo ukiangalia manzi anataka ahudumiwe vilevile (manzi alikuwa anakula salary ya 2m, dogo analipwa 300k kibaruani kwake)

Wakitoka wanawaweza kutumia mpaka 60k+ hapo ni msosi wa kawaida sana mpaka 100k, ukiangalia anasisitiza kuhudumiwa na alikuwa anaishi apartment kali kinyama huyo manzi... haikuchukua round dharau zikapamba moto za hapa na pale, nyodonyodo mwisho dogo akatemana na yule manzi.

Kwa hali kama hii jinsia KE ni wanyonyaji na wenye roho mbaya za kishamba sana! Mapenzi sio biashara
 
Kuhonga hakulipwi na mwanamke kuwa mtumwa wako. Anaweza kutumikia hata kama huna kitu.

Kuhonga kunaonesha steadiness yako ya kiume kwake na kwa jamii nzima inayokuzunguka.



MAGUFULI4LIFE.
 
Kuhonga hakulipwi na mwanamke kuwa mtumwa wako. Anaweza kutumikia hata kama huna kitu.

Kuhonga kunaonesha steadiness yako ya kiume kwake na kwa jamii nzima inayokuzunguka.



MAGUFULI4LIFE.
Sawa si ndio nyie mkiachwa mnawapiga hadinmnawatoa ngeu kisa pesa mnazowahonga zinawauma
 
Akijua kabisa dogo ana hali mbaya. Na dogo naye alikosa akili za kujiongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…