Usipokuwa makini utajikuta unachangia harusi 5 hadi 6 kwa mwezi

Yataka moyo, hongera watu wako ni waelewa sana
 
Siku nikuchangia kwenye harusi more than 100k wakiachana watanilipaaa
 
Tatizo ni pale unachangishwa hadi michango ya harusi ya Mjomba wake na rafiki yako duh!

Kama walikuchangia kipindi cha harusi yako na wewe wachangie kipindi cha harusi zao .

Kama hawakukuchangia katika harusi yako na wewe usichange harusi zao...........

Mwisho kabisa katika maisha jifunze kuwa na msimamo sio leo hii unawakataa watu wa karibu alafu kesho kutwa unawahitaji kipindi una jambo lako
 
Bwana wee nashangaa sana sasa burudani upate wewe kero tupate sie...haya basi tukichanga na sie tumuonje bibi harusi na bwana harusi 🤣🤣🤣🤣
Ila michango inakera kweli kweli. Wacha tuu.
 
Watu wa kaskazini muache harusi za showoff maana marafiki zangu wanaotokea kaskazini na wahaya ndio wanapenda sherehe za kuchangiwa .

Oeni kimya kimya , kuchangiwa ni ushamba , unakaa unapigia simu usiku missed call hata 6 ili uombe mchango .

Hata iwe vip lakini kuomba michango ni aibu kubwa , kila siku ni nyie kuomba pesa .
 
Inakuwaje mtu unachangisha mchango wa harusi?, ina maana unataka jambo kubwa kuliko uwezo wako kwa gharama za watu wengine. Hii haipo sawa.

Wewe fanya jambo lako kwa usawa wa uwezo.
Watu wa kaskazini ili wafanye showoff ndiowanapenda sana , kwa kweli ni aibu kuomba michango harusi ni private tena kimya kimya kishkaji unamaliza kazi .

Unakuta mtu anatuma kwa kila mtu meseji hiyo hiyo mpaka kero .
 
Hivi inakuwaje mtu furaha yake binafsi aliyo ipanga kwa muda mrefu anataka watu wamchangie pesa ?
Mnamchangia mtu akale mbususu.
Unatoa 50 000,unapewa vipilau vimepwayapwaya na kibawa na tubia tuwili baasi.
Hapo,safari za kanisani ukumbini li program lireefu.
Then mnapigiwa wimbo wa aurlus mabele mnaagwa.
Mbaya zaidi mwaka tu wanakuja kuomba ushauri.
Pumbavu sifanyi ujinga huo.
 
Kuna jamaa mmoja aliwaingiza mkenge wachangiaji wa harusi yake. Ilipofika siku ya kufunga ndoa akaenda kufungia bomani bila kufanya sherehe na hakufungia ndoa kanisani kama alivyopanga awali. Fedha za michango akazigeuza mtaji wa kufungua duka.
 
Kuna jamaa mmoja aliwaingiza mkenge wachangiaji wa harusi yake. Ilipofika siku ya kufunga ndoa akaenda kufungia bomani bila kufanya sherehe na hakufungia ndoa kanisani kama alivyopanga awali. Fedha za michango akazigeuza mtaji wa kufungua duka.
😂😂😂naunga mkono hoja
 
Ni zaidi ya ushamba mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…