Usipokuwa makini utajikuta unachangia harusi 5 hadi 6 kwa mwezi

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ inaumiza sana. Yaani mtu anaomba mchango kwa nguvuu tena bila aibu duh
 
Kupanga ni kuchagua. Kama unataka kuwa na uhuru, jitahidi uweze kujitawala kwanza. Uwe na uwezo wa kumwambia mtu hili naweza na hili siwezi bila kuvunja mahusiano mliyonayo.
Wakikualika kikao cha kwanza wakati wa kupledge usitokee. Usipokula chakula Chao unakuwa na uhuru wa kuchangia chochote kuliko kuhudhuria na kugonga mwaliko wao.
 
Haya ni matokeo ya sherehe kufanywa biashara, MC alipwe, Ukumbi, Caterer, videographer, mziki, sijui nini nini..

Kuna tatizo gani kwa sherehe za nyumbani? Wanafamilia, nani atashindwa kulisha familia yake?

On the other hand kiuchumi, tumieni pesa ili izunguke 😜
 
Tuko Tanzania mkuu... Haya maneno ni makali mno... Tutauwawa
Hakuna mtu wa kukuua hata kidogo. Mbona kuna watu hawaendi Bar na hawauawi? Na njia nyingine ya kukwepa ujinga kama huu ni kutojiunga na makundi ya whatsup kiholela. Chungu sana sijui kundi la ''mlisoma pamoja'' na the likes.. Kuna kipindi nilijaribu kujiunga makundi matatu tu, wiki moja nikajiondoa. Msg zinaingia kila sekunde na vitu watu wanavyo-share ni vya kijinga jinga tu.
 

Mkuu weka setting ambayo hairuhusu mtu kukuunga kwenye group mpaka akutumie notification uaccept ndo ujiunge.
 
pole sana, nenda settings za whatsapp zuia kuungwa magrup bila ridhaa yako!!hakika shughuli ni nyingi ila jikune unapofikia.
 
Uzuri n kwamba yanabaki kuwa maamuzi yako
Tatizo kuna mtu usimpochangia inakuwa ni nongwa jumla. Unakuta wewe wala ukuchangisha harusi yako. Yaani hilo wanaliingiza hata kwenye masuala mengine kama ya msiba na ugonjwa,wanakukomoa kama hukuchangia harusi uchwara zao.
 
Hakika! Ufahari wa ajabu ajabu na sifa za siku moja zinatugharimu
 
Familia / kamati yako ilichangisha? Kama ndio wanaoku add kwenye hayo magroup maana yake walichangisha.
Si kweli hata kidogo, kuna watu wala huna ukaribu nao hata kidogo, wengine mnafahamiana kawaida tu na hujawahi kuwachangisha. Yaani limekuwa ni janga kubwa sana sasa hivi, tena wengine ni wasomi na wana vipato vyao, wanashindwa kuplan sherehe ndogo wanayoimudu, inabaki kuwa kero kubwa.
 
Inaangalia na WA kuchangia.siyo unaungwa tu na mtu ambaye hamfahamiani hata kidogo unamchangia.hiyo itakuwa ni ujuha kabisa.Na ukiendekeza sana michango utanikuta nyumabi Kila siku utakula maharage.
 
Ndo shida ya watu hiyo, kipindi mtu akiwa ana jambo lake anakuhamasisha sana. Ukimchangia akimaliza shughuli yake ndo hao wa kwanza kulaumu kuhusu michango ya harusi wanajifanya sasa wanajari misiba wakati hata hiyo misiba yenyewe hawachangii.

Hili suala ni simple kabisa, usikusanye michango kwa watu kama wewe hutaki kuchangia. Mtu akikufuata mchane wazi huwa sichangii na wewe ukiwa na shughuli pambana mwenyewe tu, ikibidi usiaalike hata watu maliza peke yako.
 
Wewe ni mpumbavu.
 
Kadi za michango ya harusi πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ!



Cc Smart911
 
Dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…