Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Baada ya Rais Samia kuhutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani kwa kutumia lugha ya Kiingereza safi kilichonyooka, kuna wajinga fulani huku kwenye mitandao ya Kijamii, walimpongeza Rais Samia kwa kuhutubia kwa Kiingereza safi na huku wakimponda mtangulizi wake kuwa alikacha kukanyaga UN kwasababu ya lingua, kitu ambacho sii kweli.
Leo katika pita pita yangu, nikatembelea website ya UN, ndio nikakutana na hii kitu ambayo si wengi nyumbani tuliijua
Kumbe Rais Samia alitaka kuhutubia UN kwa kutumia lugha ya Kiswahili ila hii maana yake ni kuwa, sababu zilizomfanya mtangulizi wa Samia asikanyage UN kuhutubia, sio issues za lingua. Mimi mwenyewe, kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, nimehudhuria vikao vya Baraza Kuu la UN mara kibao nikiwa na Ben na JK, kuna viongozi kibao, wanahutubia UN kwa kutumia lugha zao, kitu kinachofanyika ni kwa ubalozi wa nchi husika hapo UN, kuarifu rasmi Secretariat, na kulipia gharama za mkalimani, Rais wa nchi husika, atahutubia kwa lugha yake, halafu kutakuwa na wakalimani wanne, ambao wataitafasiri hiyo hotuba kwa zile lugha 4 rasmi za UN.
Hivyo hata kama ingekuwa ni kweli, Kiingereza cha kiongozi wa taifa lolote, hakijasimama kuhutubia UN kwa Kiingereza, angeweza kuhutubia kwa lugha nyingine yoyote, hivyo naomba kuwahakikishia wajinga hao, sababu za mtangulizi wa Samia kutohudhuria UNGA, ni sababu nyingine tuu na issue sio lugha, eti Kingereza hakipandi kivile!.
Pili naomba kuchukua fursa hii kuwatangazia trends za hotuba ijayo ya Rais Samia kwenye 77 UNGA, itatolewa kwa lugha ya Kiswahili. Kitendo hicho, sio tuu kitaipaisha sana lugha ya Kiswahili kimataifa, bali rais Mama Samia, ataacha a legacy ya kuwa Mtu wa kwanza duniani kuhutubia UN kwa lugha ya Kiswahili na hivyo sio tuu kukipaisha Kiswahili kimataifa, bali kitendo cha kuhutubia UNGA kwa Kiswahili ni kukiingiza rasmi lugha ya Kiswahili kama moja ya lugha za UN na kukifanya Kiswahili kuwa ni moja ya lugha kuu za dunia!. The multiplier effects za kitendo hicho, ni kubwa sana kwa ni create a Kiswahili boom ambayo ita create a big demand ya mahitaji ya Kiswahili kuanzia waalimu wa Kiswahili, hadi various Swahili contents, tena mnaweza msiamini hata Hollywood wakaanza kutoa movies za Kiswahili!.
Hongera sana in advance rais wetu Mama Samia, Chief Hangaya kutaka kuhutubia UN kwa Kiswahili. Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, sasa ndio huu, huwezi kuwa mzalendo, Mkuu wa machifu wa kiasili, halafu uendelee kuhutubia kwa lugha za watu, uzalendo wa kweli ni pamoja na kuuenzi utamaduni wako, na lugha ndio kielelezo cha kwanza cha utamaduni wa jamii.
Kwa sasa Kiswahi tayari ndio lugha ya Afrika, Mama Samia atakipaisha kuwa moja ya lugha kuu za dunia.
2025 Tusifanye Makosa!.
Paskali.