Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia

Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Baada ya Rais Samia kuhutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani kwa kutumia lugha ya Kiingereza safi kilichonyooka, kuna wajinga fulani huku kwenye mitandao ya Kijamii, walimpongeza Rais Samia kwa kuhutubia kwa Kiingereza safi na huku wakimponda mtangulizi wake kuwa alikacha kukanyaga UN kwasababu ya lingua, kitu ambacho sii kweli.

Leo katika pita pita yangu, nikatembelea website ya UN, ndio nikakutana na hii kitu ambayo si wengi nyumbani tuliijua



Kumbe Rais Samia alitaka kuhutubia UN kwa kutumia lugha ya Kiswahili ila hii maana yake ni kuwa, sababu zilizomfanya mtangulizi wa Samia asikanyage UN kuhutubia, sio issues za lingua. Mimi mwenyewe, kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, nimehudhuria vikao vya Baraza Kuu la UN mara kibao nikiwa na Ben na JK, kuna viongozi kibao, wanahutubia UN kwa kutumia lugha zao, kitu kinachofanyika ni kwa ubalozi wa nchi husika hapo UN, kuarifu rasmi Secretariat, na kulipia gharama za mkalimani, Rais wa nchi husika, atahutubia kwa lugha yake, halafu kutakuwa na wakalimani wanne, ambao wataitafasiri hiyo hotuba kwa zile lugha 4 rasmi za UN.

Hivyo hata kama ingekuwa ni kweli, Kiingereza cha kiongozi wa taifa lolote, hakijasimama kuhutubia UN kwa Kiingereza, angeweza kuhutubia kwa lugha nyingine yoyote, hivyo naomba kuwahakikishia wajinga hao, sababu za mtangulizi wa Samia kutohudhuria UNGA, ni sababu nyingine tuu na issue sio lugha, eti Kingereza hakipandi kivile!.

Pili naomba kuchukua fursa hii kuwatangazia trends za hotuba ijayo ya Rais Samia kwenye 77 UNGA, itatolewa kwa lugha ya Kiswahili. Kitendo hicho, sio tuu kitaipaisha sana lugha ya Kiswahili kimataifa, bali rais Mama Samia, ataacha a legacy ya kuwa Mtu wa kwanza duniani kuhutubia UN kwa lugha ya Kiswahili na hivyo sio tuu kukipaisha Kiswahili kimataifa, bali kitendo cha kuhutubia UNGA kwa Kiswahili ni kukiingiza rasmi lugha ya Kiswahili kama moja ya lugha za UN na kukifanya Kiswahili kuwa ni moja ya lugha kuu za dunia!. The multiplier effects za kitendo hicho, ni kubwa sana kwa ni create a Kiswahili boom ambayo ita create a big demand ya mahitaji ya Kiswahili kuanzia waalimu wa Kiswahili, hadi various Swahili contents, tena mnaweza msiamini hata Hollywood wakaanza kutoa movies za Kiswahili!.

Hongera sana in advance rais wetu Mama Samia, Chief Hangaya kutaka kuhutubia UN kwa Kiswahili. Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, sasa ndio huu, huwezi kuwa mzalendo, Mkuu wa machifu wa kiasili, halafu uendelee kuhutubia kwa lugha za watu, uzalendo wa kweli ni pamoja na kuuenzi utamaduni wako, na lugha ndio kielelezo cha kwanza cha utamaduni wa jamii.

Kwa sasa Kiswahi tayari ndio lugha ya Afrika, Mama Samia atakipaisha kuwa moja ya lugha kuu za dunia.

2025 Tusifanye Makosa!.

Paskali.
 
Kiingereza safi kilichonyooka? Sio kwamba alikuwa akisoma mahali? Anyway ni kitu gani kilimfanya ashindwe kuhutubia kwa lugha ya kiswahili ama ni kwamba kurugenzi ya mawasiliano haikujipanga kwa hili kuandaa mtafasiri?
 
Eeehee! Ikawaje baadaye? Mabeberu walitupilia mbali lugha yetu adhimu? Mbona Rais alikuja kuhutubia kwa lugha ya malkia? pascal Mayala
 
Nilitaka niseme kitu ila nikakumbuka wewe ni mwanasheria, unamhukumu au kumsifia mtu kwa kukusudia. Hapo nikaishiwa cha kusema.

Lakini kuna Rais yeye hata hakukanyaga UNGA, katuma tu video iliyorekodiwa watu wakasikiliza ukumbini.

Kama Chief alikua na nia na alidhamiria kuhutubia kiswahili na hajatekeleza, tubirie siku akifanikisha hiyo adhma.

JPM alikua na mapungufu yake mengi tu, lakini ikifika jambo la kuonyesha msimamo wake alikua vizuri sana kwenye hilo eneo.

Bila kujali msimamo wake uko hasi au chanya ila alijitahidi kuhakikisha msimamo wake unajulikana bayana.

Binafsi napenda mtu mwenye maamuzi na kusimamia maamuzi yake ( shida yanapokua na matokeo hasi).
 
Eeehee! Ikawaje baadaye? Mabeberu walitupilia mbali lugha yetu adhimu? Mbona Rais alikuja kuhutubia kwa lugha ya malkia? pascal Mayala
Kuna vitu vingine ni ujinga wa hali ya juu. Eti atakipaisha Kiswahili, atakipaisha kwenda wapi? Yaani kama angetumia tu Kiswahili kuhutubia, basi tayari kingepaa.

Kichina kimetumika miaka mingapi kuhutubia UN? Kichina kimepaa kufika wapi? Hivi hapa Tanzania kwenye shule zetu, tumeanza kufundisha Kichina kwa sababu wachina wanakitumia kuhutubia UN?

Hoja za kijinga kabisa kufikiria unaweza kuifanya lugha ya nchi yako itumike na mataifa mengine kwa vile tu Rais wa nchi ametumia lugha hiyo kuhutubia UN au AU.

Mayala mpaka leo hii hajui vitu vilivyokuwa na mchango mkubwa kwa lugha fulani kutumika na mataifa mengi?

Ukoloni - mataifa yaliyoweza kuwa na makoloni (Uingereza, Ufaransa na Ubeligiji, Hispania, Ureno), biashara ya utumwa (nchi za Uarabuni), dini (Warumi, Waarabu).

Kwa sasa hakuna lugha yoyote itakayozizidi lugha za English, Spanish, French na Arab kwa kuongewa nabmataifa mengi Duniani. Kama unahitaji kuwa mfaidika mkubwa wa fursa za Dunia, hizo ndizo lugha za kujifunza. Hutaki acha. Mwenye akili huifuata Dunia. Wewe kaa usubirie Dunia ikufuate.

Mwalimu Nyerere, pamoja na uzalendo wake, aliwahi kunena, ni lazima tujitahidi kukifahamu Kiingereza maana ni Kiswahili cha Dunia.
 
Nilitaka niseme kitu ila nikakumbuka wewe ni mwanasheria, unamhukumu au kumsifia mtu kwa kukusudia. Hapo nikaishiwa cha kusema...
Unapokuwa na msimamo chanya na UN ni bora ujitoe, ukiwa memba wa JF kisha unamsimamo chanya na JF ni bora ujitoe.

UN si mali ya marekani ni mali ya nchi wanachama, unapoisusa huku ukiwa mwanachama maana yake nini! Jitoe.
 
Nimefurahishwa sana na hotuba kutoka kwa raisi wa taifa la Ghana. Ni hotuba iliyokuwa na muunganiko tofauti sana na hotuba ya mama yetu. Walioandika io hotuba bado sana.
 
Back
Top Bottom