USTAWI WA JAMII WALIVYO HARIBU MAISHA YANGU no# 4...bas akasema ukifika nyumbani ili uamini kwamba mkeo haendi msibani fanya hivi hakikisha unaficha hisia zako asijue unajua chochote mpaka kunakucha atakapo kuwa anajiandaa kwenda huko anako kuita yeye msibani mwambie mkewangu nikusaidie kuchagua nguo za kuvaa msibani kabla hajakujibu Anza kufanya hivyo kwani anaweza kuku katalia Anza kumchagulia nguo za msibani utaanza kumchagulia nguo za kuvaa msibani Kama vile magauni Madera brauzi na vitenge nk. Ukichagua nguo mwonyeshe mkeo Kisha muulize hii vipi? Ukiona anaikataa usimlazimishe weka na uchague nyingine.kwani ukimchagulia nguo za msibani Kama haendi msibani atazikataa na ukimchagulia nguo za kutokea Kama anaenda kwa mwanaume atazipokea basi nikafanya Kama nilivyo ambiwa nikaanza kumchagulia Gauni frani hivi akalikataa"nkachagua Dela kubwa kubwa akalikataa"nikachagua kibode akapokea nikachagua ka mtindo kakubana akapokea 😨😨 nikampa kitambaa Cha kichwani akakataa nikampa kikoi aka kataa""kwakifupi alichagua nguo za kumvutia mwanaume tuu😉😉 mpaka hapo nikawa nime kamilisha upelelezi wangu Basi nikatoka chemba kidogo nikampigia mtaalam wangu nikamwambia kachagua zakutokea tuu bosi wangu Basi akacheeka akaniambia Sasa unacho takiwa kufanya kabla haha Anza safari mwambie mkewangu Kuna Jambo nataka niongee nawewe kabala huja ondoka Basi mtakapo tulia muulize unauhakika kwamba unaenda MSIBANI akisema ndiyo basi baada ya hapo msikilizishe hiyo Audio baada ya Hilo zoezi nipigie.basi wakuu nikafanya hivyo mama chanja akakaa anisikilize nataka nimwambie Nini Nika muuliza he unataka kwenda msibani kweli?akashtuka akaniuliza huniamin nikamwambia hapana sema nitakumiss Sana lakini kabla naomba tuongee Kwanza kidogo kwa Mara ya mwisho.akadakia kwa mala ya mwisho Nani kakuambia tuna achana?nkamwambi hapana simaanishi hivyo namaanisha kabla hujaondoka tuongee Kwanza Basi akatulia tukakaa kwa utulivu huku nikiwa na hasira hatari lakini sura yangu sikuruhusu hata kachembe ka ndita kaonekane Basi nikamwambia niazime simu yako tafadhali kwakinyongo akanipa simu yake huku akionyesha kuwa na Shaka kidogo.baada ya kunuipa Tena simu nikamuuliza umme wait kuishi na mume mwingine kabla yangu?anajibu niwewe tuu baba yangu.nikamuuliza Tena vipi Nini kilikuvutia ukawa na mimi? Akani jibu ushauri wako, unavyo jituma,Huna makundi,uko bize Sana na na maisha, Basi Nika muuliza kingine?akanijibu Huna hasira na kingine hupendi kunikwaza,nikamwambia nikweli Basi Nika mwambia nashukuru kwa kunipenda kwa HAYO hakika Mimi nipo hivyo lakini Devo Kuna kanyimbo unako humu kwenye simu yako nimeka penda naomba ukasikilize Basi wakuu nikaka play kale ka nyimbo kaka Anza na sauti ya mwamba Halo? Basi mama chanja akaitikia kwa unyonge Halo.UKOWAPI WEWE?mama chanja anajibu nipo kwa dada tunduma.UNAKUJALINI MBONA UNAKAZI NGUMU SANA WEWE MWANAMKE?? Mama chanja anajibu nakuja kesho.UNASEMAJE WEWE?? nasema nakuja kesho msibani.UNAKUJA WAPI NANI AMEKUFA??amekufa gwila.NANI AMEKUFA MBONA SKUELEWI?Basi mama chanja aka kataa simu😂😂😝😝NYIMBO NZUULI IKAWA IMEISHA Basi Devo akasimama akanikazia macho akasema itakuja uniuwe wewe mwanaume. Nikamjibu sita kuuwa Ila KITAKUUWA UNACHO KPENDA. Kwani kinacho uwa MTU nikile anacho kupenda NIKACHOLOPOKA Tena chemba Nika mpigia mtaaram wangu nilivyo fanya akacheeka Kisha akaniambia Sasa mwambie mkewangu twende nikusindikize stendi. Nika uliza nimsindikize Tena stendi?akanijibu bado unampenda nikajibu hapana akaniambia nataka akipenda asirudi Mimi nimeona huyo kwako nikifo atakuuwa vipi unaonaje.nikasema hapo sawa Basi akasema fanya hivyo🙄🙄🙄Basi wazee mgonjwa hachagui dawa Cha msingi apone nikaludi kwa mama chanja trip hii alikuwa haniangalii husoni huku akisema ah Ila mm Basi tu" Basi tuu liwalo naliwe"sjui nna mkosi gani Mimi" nikamwambia twende nikusindikize mamaa Basi nikamsindikiza mpaka mpaka karibu na stendi huku akijisemesha njia nzima Ila baasi tu.hii dunia hii.visimu Sio vizuli hivi Basi kabla hatuja fika stendi hatua kama 20 akanisimamisha akaniambia ishia hapa nime fika me killing machine Basi Mimi nikasema sawa mama narudi kibandani. Safari njema nikamkabidhi begi nikageuza nikiwa na maumivu niliona skutendewa haki na doctor wangu skumgusa hata kiganja..... Kesho nisiku pia wakuu tunaendelea