Utabiri kuelekea uchaguzi Ukimya wa Mungu haumanishi mmekubalika jambo kubwa litatokea

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Mungu huweka serikali na viongozi kwa wakati na muda anautaka yeye. Warumi 13.
Najuwa kuna watu hamuwezi kupenda ila leo natamani mjiulize ktk serikali ya hayati Magufuli idadi ya viongozi ndani ya serikali yake walitutoka wakati tukiwa tunategemea uwepo wao. Nani angeamini tungempoteza Magufuli japo Mungu alituonyesha watu wake na tukasema.

Mungu anataka kizazi kipya cha uongozi ktk Taifa sio wale walianza na Magufuli. Hakuna anaweza kuamini hili lakini huwo ndio ukweli mchungu kwa wale wanatamani kuona wanaendelea kuwa viongozi. Nguvu kubwa yaweza tumika na kila mnacho ila Mungu hayupo ktk hizo nguvu anataka mabadiliko na mabadiliko hayo sio madogo mabadiliko makubwa kuliponya Taifa.
Mungu anasema ikiwa mtatumia akili na utashi wenu ataingilia ktk namna hakuna mtu anaweza kuamini. Hivyo hatuna budi kuepuka ghadhabu kwa kukaa pembeni. Nakupisha uongozi mpya
 
Wakati mwingine huwa najiuliza kama kweli kuna moderators? Au ndio uhuru wa kutoa maoni?
 
Awamu ya Tano ilikithiri kwenye kuumiza watu kiuchumi na namna zingine ndiomaana haikudumu,

Awamu ya sita ni chaguo la Mungu, akitoka mama tunampa Nchi Abdul,kwaiyo muandae vidonge vya kutosha vya shinikizo la damu.
 
Nimekusubiria hatimaye sasa umenena, basi na ikawe heri katika kutimia kwake.
 
Mungu atende na afanye MABADILIKO MAKUBWA ZAIDI. Hili naliombea sana.
 
Mungu huweka serikali na viongozi kwa wakati na muda anautaka yeye. Warumi 13.
Acha uongo Wizi wa Kura na kupora masanduku huku mkiteka wagombea na kuua mawakala ni Mungu gani wa hovyo namna hiyo.

We jamaa Upigwe bani kila siku unakuja na nyuzi za kuitisha mamlala iliyoko madarakani.
 
Awamu ya Tano ilikithiri kwenye kuumiza watu kiuchumi na namna zingine ndiomaana haikudumu,

Awamu ya sita ni chaguo la Mungu, akitoka mama tunampa Nchi Abdul,kwaiyo muandae vidonge vya kutosha vya shinikizo la damu.
Sema Abdul akichukua Nchi tutakula bata balaaa
 
Nguvu kubwa yaweza tumika na kila mnacho ila Mungu hayupo ktk hizo nguvu anataka mabadiliko na mabadiliko hayo sio madogo mabadiliko makubwa kuliponya Taifa.
Kuliponya Taifa kwani Taifa linaumwa?
 
Ni ngumu sana kuelewa namna Mungu anayofanya kazi zake. Huachia mambo mabaya yenye kuumiza, kutesa na kuvunja moyo yatokee halafu huja kuyafutilia yote.

Lazima tuelewe kila mamlaka iliyopo Mungu ndiyo aliamuru uwepo wa hiyo mamlaka lakini wale wanaoongoza hizo mamlaka huwa wanafanya mambo kwa utashi na akili zao. Utawala wa Magufuli ulikuwa wenye kuumiza na kupumbaza akili za watu.

Lakini Mungu aliamua kumfutilia mbali huyo Magufuli, akaingia Dr Samia na tunaona bado hali ni ile ile kama ya utawala wa Magufuli na bado wapo wanaosifia, wanatesa na kuondoka uhai wa binadamu we zao still Mungu ameamua kuachia yote hayo yatokee.

Mungu ana kusudi lake na kwa imani yangu wakati wake na kwa hekima yake atatuletea Kiongozi bora mwenye kujali na kumtetea watu wake.

Sijui na sielewi kanuni za Mungu zipo Vipi kwenye hili jambo lakini naamini baada ya haya malalamiko, mauaji, mateso na changamoto za kila namna kwa Watu wake atazikomesha na watu wake watapata furaha na amani kwenye nchi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…