Utabiri: Mwaka huu hautaisha kabla ya Dola ya Marekani kufika 3000Tsh

Ukitaka kula na mjinga msigie huo ni usemi wa uswahilini na wanakula nae vzr kwakua njia za kupiga maisha hazina kizuizi just proposal watu wanakula hela and maisha yanasogea,itafika 3000 kwakua nchi inakopa zaidi kuliko kuzalisha vitu na kuuza nje
 
Tangu 61 tupo kwenye maandishi na kulalamika kwenye keyboard
Natumaini jibu lake umelielewa barabara, kwani kakujibu vizuri sana hapa:

 
Seme balance of payments
I know all this,Kuna punguwani nilikua nalielewesha
 
Umesahau diesel na petrol kufika 4 000!

Your browser is not able to display this video.
 
Siyo kweli, 1961 ilikuwa $1 = Tsh 7. Kama iliwahi kuwa Tsh 5, itakuwa ni wakati wa ukoloni!
Sina kumbukumbu hivyo ila mara ya kwanza nasafiri na mzee ilikuwa miaka ya 70 na alichenji $1000 ila sikumbuki ilikuwa sh ngapi
 
Siyo kweli, 1961 ilikuwa $1 = Tsh 7. Kama iliwahi kuwa Tsh 5, itakuwa ni wakati wa ukoloni!

$35,000 si haba; kwenye madafu takriban 105 hivi!
Uta'accumulate' hadi lini?
Hizo zipo tu zina mpango wake nasubiri few years zingine boss
 
Black market hapa tunduma tunachenji 2800 and I'm sure December lazima ifike 3000 manake wafanyabiashara watanunua sana nje kuliko kuuza nje.
 
na mimi naongezea ka 100 kangu. itakua 3100
 
Ukweli kupanda kwa bei ya dollar against tz shilling ni indicator kubwa ya uchumi WETU kuchuka

Tatizo serikalini kumejaa wanasiasa na machawa hakuna watendaji, na cha kushangaza uchawa umekua kazi rasmi sikuhizi

Nilishangaa kuna chama kimoja Sijui kama kimesajiliwa kinaitwa 👉CHAWA WA MAMA TANZANIA kifupi chake kimenitoka kuna jamaa yupo kwenye hicho chama na wanapata Hadi Safari za matukio mbalimbali ya serikali

Mfano mei mosi iliyopita walikwenda hawa vijana na wapo kuanzia ngazi ya kata Hadi taifa na posho na gharama za Safari wanalipiwa na maradhi yote na wanalala hoteli 🙆🏻‍♂️😢

Hizi zote ni kodi za watanzania viongozi wameacha jukumu lao mama la uwajibikaji wamehamia kwenye kuwekeza kwenye uchawa inasikitisha sana

Uchumi unahitaji utendaji na Sio siasa
 
Kwa namna tunavyo elekea, ulicho project kinawezekana sana mkuu
 
Mfano mei mosi iliyopita walikwenda hawa vijana na wapo kuanzia ngazi ya kata Hadi taifa na posho na gharama za Safari wanalipiwa na maradhi yote na wanalala hoteli
Mkuu 'Muramwaito', mimi nina mashaka sana na hizo pesa kuwa ni za walipa kodi; ingawa hata hilo halitupi nafuu yoyote.
Hizo pesa ni za hawa waarabu wanaotununua sasa. Hivi vi-nchi vya kiarabu vyenye ukwasi mkubwa sasa wanatumia pesa zao kutununua mazima mazima..
Mama kapewa hayo mahela anunue uongozi ili wafadhiri wake waendelee na mipango yao hapa kwetu.
Hata hao wamasai wanaohamishiwa Handeni, hizo hela za kuwajengea vijumba usifikiri mama kaziokota tu mahali, ni kutoka huko huko, ili wenye pesa zao watumie hilo eneo wanakohamishwa wamasai bila ya kubughudhiwa.

Watu ni muhimu tuelewe haya maswala vizuri, ili tunaponunuliwa tuwe tunajuwa hata kama hatuwezi kufanya lolote.
 
Hatuna viongozi tuna majangili tupu
 
Dollar haishindani na TZS inashindana na Yen, Pound, Russian Ruble.

Dollar inaweza ikashuka ila TZS inaweza ikashuka pia. Tuombe tuh EWURA watusaidie na bei za mafuta.
 
MAMA ANAZIDI KUPAA NA MADERA YA CCM
 
Umeskia kuhusu BRICS mzee!
Wale mpango mkakati wao ( wa kisiri )ni kuiondoa dollar kwenye utawala wa biashara za kimataifa
Vikwazo vya kiuchumi Marekani alivyomwekea Urusi ni ushindani wa kiuchumi (kati ya mashariki na magharibi)
Mkuu unajua taifa la Marekani hata katika biblia kwenye kitabu cha ufunuo 13 limetajwa ni vile inahitaji ufahamu kutambua

Kwaiyo taifa la Marekani lipo kimkakati Mkuu Ndio maana linanguvu na litaendelea kua na nguvu ya kiuchumi Kwaiyo hakuna jumuia yoyote inaweza kuiondoa Dollar kwenye utawala wa Dunia bali dollar na uchumi wake wa Marekani vitazidi kuimarika na kuimarika kila Leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…