Utabiri: Mwaka huu hautaisha kabla ya Dola ya Marekani kufika 3000Tsh

Utabiri: Mwaka huu hautaisha kabla ya Dola ya Marekani kufika 3000Tsh

Hii nchi watangayika wamepumbazwa na wakapumbazika .

Yaani nchi ina soko la ndani la watu mil. 65. Ina amani, ina raslimali za kutosha, imepakana na nchi Nane na Bahari inayopokea soko lote la Nchi za mashariki halafu Imegeuka kuwa nchi ya wachuuzi wasioweza hata kukusanya pesa za ushuru wa bandari na wa viwanja vya ndege.

Baada ya adui kuteka viwanja vya ndege vya Tanganyika na bandari sasa ipo siku atatuambia kuwa hatuna uwezo wa kujilinda tunahitaji ulinzi wa nchi nyingine kutoka Uarabuni kama ilivyo Ufaransa na baadhi ya nchi za Afrika ya Magharibi.

Haiwezakani mpaka hela ya kenya inapanda thanani wakati wahitaji malighafi na chakula kutoka Tanzania .

Wakenya wanaingia mpaka Vijijini kununua vyakula badala ya waTannganyika wenyewe kununua na kuweka kwenye maghala na kuwaizia wageni ili pesa za kigeni zibadolishwe kwenye mifumo rasmi.

Kelele za waziri wa kilimo ni nyingi lakini hatuoni wakijenga masoko mipakani.

One stop center zinatakiwa kwenye mipaka yote ili wanaoingia mipakani kununua mazao waapate masoko mipakani . Na pesa zipitie mifumo rasimi .

Mikopo Inachukuliwa kila siku halafu inaishia kwenye sadari za nje na ndani za kila siku na misafara mirefu inayotumia mafuta kutoka nje kwa kununua magari ya kifahari kila kukikcha .

Majengo ya serikali yanawekwa Furniture kutoka chini kwa mikopo kutoka ulaya .
Mkuu mbona kodi tunalipa sana tu tena wengine kwa vitisho kabisa!

Sema sasa hivi kila kiongozi anakula kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Nchi ya ajabu sana .
wanatuletea wakulima wa china kulima mihogo badala ya kuwapeleka vijana wetu wakajifunze namna ya kulima mihogo china kisha waje walime kwenye ardhi yetu wenyewe na kisha tuwauzie kwa pesa za kigeni.
Mbona tulishauzwa kitambo mzee?
 
Madhara ya kupata dereva muuza chapati ndiyo haya Sasa.
 
Na bei za nyumba zingebaki hivyo hivyo.

Kwa mantiki yako unanunua ghorofa kwa laki 2.

Wisdom is chasing you but you are always faster.
Mantiki ya hii ni nini?
Sasa tueleze upande wa hiyo $, imebadilika kiasi gani. Je na huko wanakoitumia majengo yao bado yananunuliwa kwa thamani ya miaka 50 iliyopita?
 
Kwanini usiwaletee hao wachina kwenye hizo kata wanazolima mihongo wakafundisha wakulima wetu?
Kweli pale Sokoine hawawezi hata kuwafundisha hao vijana kazi hiyo? Hapana, achana na Sokoine, hivi vyuo vya kati tu, havina uwezo huo?

Lakini tunazungukia mambo haya humo humo, ndani kwa ndani wakati tukijuwa, swala siyo ufundi wa kulima mihogo pekee, ni sekta zote, kila mahali, akili zetu sasa ni kutafuta watu wengine waje wafanye. Sisi hatuna tena moyo wala utashi wa kujifanyia wenyewe kwa manufaa yetu wenyewe.

This is a disgrace. Sijapata kuona viongozi wenye akili mbovu kabisa kama hawa waliomo kwenye serikali hii.
Hawa wanalihujumu taifa letu kwa maksudi kabisa, lakini sisi tupo tu tukiwachekea!

Inasikitisha sana.
 
Ndio maana nikasema kuna uwezekano ikafika 3000tsh ndani ya mwaka huu.
Mimi ngoja niwe "wakili wa shetani", nikidandia kwa hoja ya huyo uliyemjibu hapo.
Mama ana haha kutafuta uwekezaji toka huko nje, huenda katika akili yake ni kwamba akiwapata wa kutosha; hayo ma-$ ya uwekezaji yataipaisha shilingi!

Hebu kwanza: si hapo majirani zetu Kaskazini majuzi tu walikuwa wakisimangwa na huyu huyu mama yetu, kwa ukosefu wa $, na thamani ya Shilingi yao ilikuwa ikiporomoka kama nazi? Sasa ile Ksh. imeimarika, haiporomoki tena, badala yake inapanda dhidi ya $ na hata madafu yetu.
Je, tumejiuliza wao wamefanya nini?
Hebu kawaulize IMF ana WB walichofanya huko. Sasa usiniulize kama ni sawa au siyo sawa. Hilo linabaki moyoni mwangu.

Kama umeuelewa "uwakili wangu kwa shetani", hapo sawa.
 
Nimetoa mfano tu lakini ni kwa kila zao.
wakulima wetu hawana utaalam wa kulima na mazao kwa kowango kinachohitajika.
wasomi wenye elimu ya kilimo sio wakulima .
Wenzetu wanalima kama kazi na ajira ya muda wote . Sisi kwetu wasomi wanalima kwa kusikia kuwa bei imepanda . ikishuka hawalimi. Kumbe ilitakiwa serikali muda wote iwasaidie wakulima ili mazao yasipande sana bei wala yasishuke sana ili majirani wasiweze kushindana kulima zaidi waone soko la uhakika la kununua chakula lipo Tanzania.
watu wanatakiwa wajifunze kulima kwa wingi zaidi na sio kulima kidogo kwa bei kubwa.

Vyakula vikiwa vingi utakua na kuku wengi,ngombe wengi , samaki wengi, nguruwe wengi ,kanga wengi, kondoo, wengi, mbuzi wengi ,punda wengi n.k.
Vyakula vitashuka bei kwenye soko la ndani na mzunguko wa fedha utakua mkubwa ndani ya nchi na kuuza nje pia .
Mkuu '1000 digits', nimekusoma mabandiko yako toka mwanzo hadi hapa, nikawa nasita kuku'quote'.

Unayosema/andika hapa kuhusu kilimo chetu, hali iko hivyo hivyo katika nyanja zote - bandari, ujenzi, usafirishaji, na mambo mengi mengine ambayo tungepashwa tuwe tunayafanya sisi wenyewe.
Badala yake mtindo sasa umekuwa ni kutafuta watu waje wafanye, kwa sababu sisi hatuwezi!
Sasa kama taifa, tutakuwa taifa la namna gani hili ambalo watu wake hakuna wanachokiweza?

Kwani tatizo ni nini hasa?
Watu kweli hawawezi kulima mihogo kwa ufanisi? Hawa waChina wao walizaliwa wakiwa na 'gene' za kulima mihogo, ambazo sisi hatuna?

Nchi yetu sasa hivi kuna tatizo litakalotugharimu sana. Uongozi wa aina hii tulionao sasa hivi siyo uongozi unaolijali taifa hili na watu wake.
Ngoja niachie hapo.
 
Dola ni product ya USA,wameamua kuipandisha thamani kwa kuifanya kuwa haba,hata baba yako angekua ikulu bado Dola ingepaa tu
United States federal reserve /Benki kuu ya Marekani waliraise interest rates ili kupambana na mfumuko wa bei mwaka huu na results Ndio hizo kwamba mitaji na investments denominated in US dollar inakimbia mataifa mengine na kwenda Marekani kununua US government bonds Maana magawio yake ni makubwa
 
Dola ni product ya USA,wameamua kuipandisha thamani kwa kuifanya kuwa haba,hata baba yako angekua ikulu bado Dola ingepaa tu
Ila kuna factor nyingine pia kama import - export trade imbalance (ukosefu wa mizania katika uwiano wa biashara ya kuuza nje na kuagiza bidhaa na huduma toka nje ya nchi ) ,mfano mzuri ni Tanzania nchi ambayo inanunua bidhaa na huduma kwa wingi toka nchi za nje tofauti na inavyouza nchi za nje .
Ukosefu huu wa mizania ndio husababisha pia pesa nyingi za kigeni hasa US dollar kwenda sana nje ya nchi kununua bidhaa kama magari ,mafuta ,madawa ,nguo , mitambo nk
Sababu nyingine ni uongozi mbovu na ufisadi wa serikali ya nchi husika , kwenye huu mdororo wa uchumi unaoendelea duniani , ni rahisi sana kuzifahamu nchi zilizotawaliwa na ufisadi na uongozi mbovu katika kumanage pesa za umma .
Na Tanzania ni mfano mmoja wapo .
Nchi inayotembeza bakuli kila siku ni nchi mfu inayoongozwa na corrupt politicians
 
Back
Top Bottom