Hii hali siyo nzuri kabisa wanasiasa wanavipaka bure matope vyombo vya dola .Tatizo lilikuwa dogo sana,alitakiwa mtu mwenye busara sana amshaurri Raisi mapema kuwa ,huu uamuzi wakufanya chaguzi kijanja janja sasa unafikia ukingoni , Angalau kuna vitu vinatakiwa viwekwe sawa,Kweli nchi inavyombo vya dola vyenye nguvu na uwezo ila vipo kwa ajili ya nani? Sidhani ni jambo la busara hivi vyombo vikatumika kuwagandamiza wananchhi ambao wanadai haki zao.Hata hao wana CCM wakawaida hawako tayari kuwapata viongozi ambao hawakupita kwa matakwa yao.Wabunge na watu wengine wanao parilia huu moto ,jnaweza ukawaunguza.Ajenda ya CDM No reform no election imesambaa Tanzania nzima na waliyo wengi waliiunga mkono hata kabla haijatangazwa. Si busara kipindi cha uchaguzi kukawa na makundi hasimu mawili ,moja linapinga uchaguzi ,moja ambli linafaidika na huo uchaguzi na fedha za uma zinaunga mkono uchaguzi.Tanzama pesa za nchi zinavyo tapanywa hovyo hovyo , Raisi anaweza kutoa mamilioni ya fedha kwa mtu au taasisi yoyote anayo itaka bila kujulikana hizo fedha zinatoka katika bajeti gani.kuna mabilioni ya fedha CAG anasema zimetumika bila mpangilio je ndiyo hizo amvazo Raisi anawagawia watu na taasisi mbali mbali kila siku.Nishauri nchi yangu Tanzania ,twende kwenye uchaguzi tukiwa wote tukiwa na wito mmoja uchaguzi ulio huru na haki.Chaguzi,,i hizi zinatumia kodi zetu lazima tuwe na uchungu na fedha zetu wananchi.Hii hali ya maisha kuwa juu sababu kubwa ni maswala ya kisiasa,Kama fedha nyingi zingepelekwa kwenye miradi ya maendeleo wala Tanzaa tusingekuwa na shida ya ajira na majirani zetu wengi wangekuja kutafuta ajira kwetu uwezo huo tunao,Tanzania kuwa kama Texas inawezekana kabisa tena ndani ya miaka 5 tu.Tunauwezo kabisa wakupandisha pato la taifa kutoka trilioni mbili mpaka trilioni kumi kwa mwezi,bila kumuumiza mwananchi yoyyote kama tutatumia rasilimali zetu vizuri na VAT ikashuka kutoka 18% mpaka 10% . Tunapaswa kuwekeza sana ktk kilimo na kujenga mahusiano mazuri na jirani zetu,Mazao ya chakula na ya biashara yanasoko kubwa sana kwa jirani zetu hata humu nchini ,tunaagiza ,ngano,mafuta ,sukari ,mahindi ,michele kutoka nje wakati tunauwezo wakuzalisha bidhaa hizo na kuwauzia nchi jirani kwa mwaka mzima.kama zao la korosho,Pamba,tymbaku,mawese,kakao,kahawa,lingewkewa mkazo ,usingewaona mami,,ia ya vijana wakimachinga wakizurula mjini,wala waha wakiangaika kukopesha vyombo,wala wanyamwezi na wasukuma wakitafuta vibarua mjini.Viwanda vyetu vingepata malighafi kwa bei raisi na kiasi kinachobaki kingeuzwa nje.tungekuwa na akibwa kubwa ya fedha za kigeni na fedha yetu ingeongezeka thamani na mfumuko wa bei ungeshuka chini.Sisi tunaweka kipaumbele kwenye kununua V8 ,msafarsa una magari 200 unategemea kupata maendeleo kwenye hiyo nchi hii yote ni kwasababu chaguzi zetu siyo huru na haki na viongozi wanaopatikana hawapatikani kwa riadhaa za wananchi kwahiyo vipaumbele ni matumbo yao siyo tija kwa wananchi wao.