Huo utabiri sidhani kama kweli upo.
Lakini ninachokiona uongozi wa Tundu Lissu ni shirikishi zaidi ya ilivyokuwa kwa Mbowe.
Kwani ndani ya miaka miwili tu kuna viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chadema ambao hawakufahamika awali wanasikika na wanaonekana wana uwezo mkubwa.
Kama Mwenyekiti wa Bavicha,Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti,Mwenyekiti wa mkoa wa Mara na Njombe nk.
Wana uwezo mkubwa.
Vile vile hata wanachama wa kawaida wa Chadema wanaonekana wanaelewa vema misimamo ya Lissu kwani wanaielezea vizuri Kabisa.