Utafiti binafsi: Ukitegesha alarm usiku lazima uamke muda mfupi kabla ya alarm kulia

Utafiti binafsi: Ukitegesha alarm usiku lazima uamke muda mfupi kabla ya alarm kulia

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Hili nimelifanyia utafiti muda mrefu sana toka niko shule

Kila nikitegesha alarm lazima nitashtuka usingizini kabla ya alarm haijaniamsha

Utakuta nimeset alarm ilie saa 10 kamili usiku lakini cha ajabu kwenye saa 10 kasorobo ama saa tisa na dakika 55 nakuwa nimeshtuka kutoka usingizini
 
Autonomic Nervous System (ANS) Ni sehemu ya mfumo wa fahamu ambao huratibu matendo yanayofanyika ukiwa hujitambui au ukiwa umelala, pia huratibu shughuli mbalimbali za mwili kama vile mapigo ya moyo, mmeng’enyo wa chakula, kutanuka na kusinyaa kwa mboni,hamu ya kufanya mapenzi nk nk.

Ubongo hua unafanya kazi kutokana na vile akili yako itaUkomandi. Pindi unaposeti alarm kuamka saa kumi basi unakua umeusisitiza ubongo wako kwamba saa kumi alarm italia so Inabidi uamke Hence Ubongo wenyewe unakua unajua Inabidi uamke kabla ya saa kumi.

Hakuna uchawi hapo ni Saikolojia tu✌️
You're what you think....Fikra zako zaweza kujenga au kubomoa
 
Inategemea na umuhimu wa jambo linalokufanyavuamke muda huo, masaa uliyolala, hali ya uchovu, na mazingira.
Kuna watu wanaweka alarm na bado wanamiss paper. Yaani hapo ni malaika wako tu wanakusaidia kukuamsha
Yaani ulale mpaka umiss paper
 
Hili nimelifanyia utafiti muda mrefu sana toka niko shule

Kila nikitegesha alarm lazima nitashtuka usingizini kabla ya alarm haijaniamsha

Utakuta nimeset alarm ilie saa 10 kamili usiku lakini cha ajabu kwenye saa 10 kasorobo ama saa tisa na dakika 55 nakuwa nimeshtuka kutoka usingizini
Mimi huwa nategesha ila zinalia na mimi nikiendelea kuenjoy usingizi kama kawaida, nikibahatika kuisikia lazima nikaizime na kuendelea kulala.

Sijui kwa nini Alarm ikilia na usingizi unanoga zaidi hapo hapo[emoji3]
 
Hili nimelifanyia utafiti muda mrefu sana toka niko shule

Kila nikitegesha alarm lazima nitashtuka usingizini kabla ya alarm haijaniamsha

Utakuta nimeset alarm ilie saa 10 kamili usiku lakini cha ajabu kwenye saa 10 kasorobo ama saa tisa na dakika 55 nakuwa nimeshtuka kutoka usingizini
GIGO
 
Sijui kwa nini Alarm ikilia na usingizi unanoga zaidi hapo hapo[emoji3]
Mdogo wangu hii ilinisababishia simu niwe naiweka mbali ili kitendo cha kwenda kuizima alarm basi najua usingizi nishaukimbiza.

Mana nilikuwa na tabia ya kurudi kulala huku naongeza dakika tano tano 😂 hadi siku moja nikachelewa kwa Mdosi. 😂
 
Back
Top Bottom